Safari za Rais Samia nje ya nchi

Hao unaowaita wataalamu ndiyo watu wa hovyo kabisa kuwahi kutokea.

Kama ndiyo hao wanao engineer safari za nje basi kama taifa tunapigwa sana.

Niliwah kusikia kipindi cha Jiwe kuwa kuna watu walikuwa wanamuandalia ziara ili nyuma wapige deal zao. Na walikuwa wanafurah akiwa ziaran huko kwan walijipigia kadri wawezavyo.

Naunganisha dots. Hii isije ikawa ni mbinu yao ya kuendelea kupiga deal na actually wanakula kodi mambo ya Per diem si hatar hiyo mkuu...

Enewei hizo safari za nje sioni tija yake kabisa. Maji hakuna , umeme ndo usiseme kwa saa moja unakuta unakatika hata mara 10 halafu mtu unamhie habar za safari za nje???????


Tuamke!
 
Najiskia vibaya sana nikiona maandiko yako wa jina. Najikuta mwenye aibu sana nikiona jina la kitume linaandika habari za kichawa.

Rekebika. Nchi haina maji wala umeme, sukari ndo kabisa halafu ww unahangaika kusifia watu walioshindwa kutatua kero hizo?

Huenda una shida kubwa tumboni mwako lkn nakuhakikishia, dawa ya maumivu haiwezi kuponesha hilo tumbo lako. Unahitaji kumuona daktari bingwa wa magonjwa kama hayo aweze kukufanyia matibabu ya haraka kama ikiwezekana hata kwa opareshen. Hayo madawa ya kutuliza maumivu yatakuletea shida kwenye utumho mpana kaka.

Tafuta daktari bingwa atakayeponesha hilo tumbo lako na siyo kuhangaika na famasi na duka za dawa ya maumivu ya tumbo.

( Wanafasihi watakuwa wamenielewa vyema! )
 
Enewei hizo safari za nje sioni tija yake kabisa. Maji hakuna , umeme ndo usiseme kwa saa moja unakuta unakatika hata mara 10 halafu mtu unamhie habar za safari za nje???????


Tuamke!
Nadhani ni Tanzania tu ambapo watu wanaweza kuwavumilia watu waliokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 60 na kushindwa kabisa kutatua changamoto nyepesi kama hizo ulizozianisha hapo.

Na ni aibu sana kwa kweli.
 
Siku ambazo anakuwa hajasafiri huwa unapata tija gani? Tuanzie hapo.
Mambo mengine yana wivu wa kike
 
Huna akili
 
🤣

Leo yuko Namibia kuhudhuria mazishi!

Mwezi huu kasafiri kwenda nje mara ngapi vile?

This woman is worthless.
 
🤣

Leo yuko Namibia kuhudhuria mazishi!

Mwezi kasafiri kwenda nje mara ngapi vile?

This woman is worthless.
Diplomasia ya kimataifa inaendeshwa kwa kanuni za reciprocity.

Kanuni za kurudishiana fadhila, kurudishiana madhila.

Rais wetu alifariki, watu wa nje wakaja kuzika. Marais.

Rais wa Namibia amefariki. Kwa nini rais wetu asiende?

Yani tunataka watu waje Tanxania kwenye misiba lakininsisi tusiende kwenye misiba yao?

Samia kuna safari za kumsema, lakini si safari za misiba.

Hao Wanamibia wengi wamekulia Upanga tunawajua, wengi wamekulia kwenye kambi za wakimbizi Tanzania wakati wanapigania uhuru.

Tumekuwa nao karibu miaka mingi sana mpaka wanapata uhuru, leo wamepata uhuru ndiyo tuwatupe mkono?

Hata kwenye diplomasia za uchumi hilo litakuwa ni ujinga.
 
Marais wote wa dunia walikuja? Marais wote wa Afrika walikuja? Marais wote wa SADC walikuja?

Kazi za kuhudhuria misiba mara nyingi huwa ni za makamu wa Rais.

Ndani ya miezi miwili iliyopita huyu bibi anasafiri tu.

Lini anakaaga ofisini?
 
Marais wote wa dunia walikuja? Marais wote wa Afrika walikuja? Marais wote wa SADC walikuja?

Kazi za kuhudhuria misiba mara nyingi huwa ni za makamu wa Rais.

Ndani ya miezi miwili iliyopita huyu bibi anasafiri tu.

Lini anakaaga ofisini?
Namibia si some random country, kuna uhusiano mkubwa kati ya Tanzania na Namibia, wa Namibia wamekaa sana Tanzania wakipigania uhuru.

Rais Museveni wa Uganda alihadithia jinsi alivyokaa Upanga wapigania uhuru wa SWAPO.

Samia ana kazi ya ku repair some of the damage done by Magufuli during his isolationist era.

Rais wa nchi ana kazi yenye sura ya ndani ya nchi na nje ya nchi.

Na hata kama anatakiwa apunguze safari, si busara kukata safari za mazishi kwenye nchi yenye uhusiano mzuri nasi kama Namibia.

Aliyefariki Namibia ni head of state, ni rais, si VP. Ki itifaki rais anatakiwa kuzikwa na ma rais wenzake, ukimpeleka VP ni kama umem slight.
 
Haya, sawa. Aende tu.
 
Haya, sawa. Aende tu.
Kwenye msiba mimi sina lawama.

Na hata hizo safari nyingine zinazoweza kuwa na tija, zikifanywa vizuri, siwezi kumlaumu.

Rais hatakiwi kutapanya fedha kwa safari zisizo na tija.

Lakini pia, rais si mwali ajifungie nyumbani tu.

Unaweza kulalamika rais kafanya safari ya kutumia dola milioni moja, ukasema hizo ni pesa nyingi sana. Lakini, kama hiyo safari imeleta faida ya dola bilioni moja, then it is justified.

Kuna namna ya ku balance kusafiri na kukaa ndani.

1. Safari ziwe na cost benefit analysis nzuri. Tujue rais anaenda kufanya nini, anaenda ku represent intetests gani za kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia.

2. Safari ziwe na uwazi. Tujue gharama, tujue sababu, tuweze kupima.

3. Safari ziwe na jumbe ndogo zinazolipiwa na serikali, zikiruhusu wajumbe wengine watakaoandamana na rais, kama wafanyabiashara walioidhinishwa, kuwa katika msafara wa rais, kwa kujilipia wenyewe gharama zote.

Mimi huwa namsema sana Magufuli, vibaya. Lakini, katika hili la tatu, Magufuli aliweza kudhibiti vizuri sana ukubwa wa jumbe za Tanzania hususan kwenye mikutano ya UN New York City.

Jumbe za Tanzania nje kabla ya Magufuli zilikuwa zinafanya kufuru.

Nakumbuka niliona ripoti moja ya TV ya New York City (local news), walifanya expose ya mabalozi wa nchi/ UN delegations za kiafrika walivyokuwa wanatanua kwenye hoteli za bei mbaya za New York City, na kufanya shoppings za kufa mtu.

Lakini, walitoa mfano mmoja mzuri wa ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri Augustine Mahiga ulivyokuwa mdogo na ulivyokaa kwenye hoteli za bei nafuu sana.

Tunaweza kufanya hizi safari kwa tija tukakataa rais kutokuwa na safari kabisa kwa upande mmoja na kusafiri sana kwa upande mwingine.

Tatizo moja naliona Tanzania tunakuwa sana watu wa "all or nothing at all".

Mtu kama Magufuli aliona tatizo la rais kusafiri sana, akatuletea tatizo lingine la rais ambaye hasafiri kabisa.
 
Unadhani uhaba wa dola unatokea wapi?
Unatokana na hizi safari, mamilioni ya dola yanatumika.
Hatuna raisi, tulipigwa
 
Unadhani uhaba wa dola unatokea wapi?
Unatokana na hizi safari, mamilioni ya dola yanatumika.
Hatuna raisi, tulipigwa
Mkuu,

Kama nchi inamaliza dola zake kwa safari za rais tu, hiyo nchi haistahili kuwa nchi.
 
Mimi sina tatizo kabisa na safari za nje. Sipingi Rais kusafiri kwenda nje.

Ila kwa huyu mama naona kumezidi.

Si majuzi tu hapa alikuwa Norway, Indonesia, Ethiopia,Vatican, sijui Congo, na leo yupo Namibia…..in a span of maybe 2 months.

Hata kwenye uapisho wa Bola Tinubu alienda 😀.

Alishindwa hata kumtuma Dkt. Mpango?

Kuna safari zingine unaona kabisa makamu wa Rais angetosha.

Btw, Rais Magufuli alipokufa, Rais wa Namibia hakuja kwenye msiba.

Just thought I’d throw that in there since you mentioned reciprocity.

Narudia tena, sipingi safari za nje kwa Rais. Lakini kutumia busara na kuchagua safari zipi za kwenda na zipi za kutuma mwakilishi, maamuzi mazuri.
 
Naona kuna tatizo la uwazi serikalini, kiasi kwamba inakuwa vigumu kuitetea serikali, hata ikiwa serikali inafanya safari zenye tija.

Mpaka leo kimsingi Ikulu haina bajeti maalum ama bajeti haikaguliwi.

Yale mapesa rais anayogawa ovyo barabarani, au ya kununua magoli, huwa hayana bajeti wala ukaguzi. Anaweza kiyapeleka kununua saa ya $44,000 na watu wasijue.

Na kwa kweli kukosa uwazi huku kunatafsirika kama mbinu maalum ya kuepuka utawala bora na kutaka kufanya mabaya, ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa mali ya umma.

Kuna dhana kwamba kukosa uwazi huku si kwa bahati mbaya, ni mpango maalum wa kuficha matumizi.

Ni vigumu hata kuilaumu serikali objectively with facts and figures, kwa sababu hatupati factual and data driven reports kuhusu safari hizi. Ingawa circumstantial evidence haioneshi kuwa tuna watu wenye akili au hata kujali hapo Ikulu.

Labda tujikite hapo kwanza kwenye data kwanza. Hivi Tanzania hatuna some sort of "Freedom of Information Act" ya kuomba hizi data? Hii ni haki ya kikatiba.

Utaitetea vipi serikali ikiwa serikali yenyewe haina uwazi wa kuonesha cost benefit analysis?

Sishangai Magufuli hata rafiki zetu hawakuja kumzika, he was an ignoble country bumpkin isolationist buffoon. Sasa kampa kazi kubwa sana Samia ku repair damage, inawezekana Samia anaonekana anasafiri sana kwa sababu anafidia mpaka safari za Magufuli.
 
Safari za Samia [na watangulizi wake] zitaonekanaje zina tija ilhali huduma za msingi kama maji, umeme, n.k., bado ni changamoto?

Wamekaa madarakani zaidi ya miaka 60 lakini hadi leo bado tunahangaika na ukosefu wa umeme!

utanishawishije mimi Mnyantuzu wa Ikungulyabashashi kwamba safari zao zina tija ilhali huduma za msingi tu zimewashinda?

Ungeniambia labda Samia anaenda kutafuta power companies huko nchi za nje waje kuanza kutoa huduma ya umeme maana serikali imeshindwa, na kweli hao watu wakaja na kuanza kutoa huduma ya uhakika, guess what?

Nisingelalamika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…