Safari za Rais Samia nje ya nchi

Nimeona Lucas Mwashambwa aliwajibu tija za safari lakini sijaona kama mmemjibu.

Tena nimesikitika kuona mtu mmoja baada ya kujibiwa ameponda majibu kwa kusema "nani atasoma gazeti hili?".

Hapa kuna siasa na uchumi. Kuongelea siasa kwa hisia ni rahisi.

Kuongelea uchumi kwa namba ni kazi ngumu.

Wengi tunapenda kuongelea siasa kwa hisia kuliko kuongelea uchumi kwa namba.

Na kwa kweli siwezi kuwalaumu sana mnaoongelea siasa kwa hisia, kwa sababu, kama nilivyosema hapo awali, serikali yenyewe haitoi data za kuwawezesha kufanya uchambuzi wa uchumi kwa namba.

Bila ya granular cost benefit analysis reports ni vigumu sana kuibishia serikali, kwa sababu wao wanaweza kukuambia tumeenda kuweka mazingira mazuri ya biashara na serikali za ughaibuni, kwingine kuna mikataba wafanyabiashara watasaini.

Na hata wakisaini hatujui tofauti ya MoU na a binding contracts.
 
Akae atulie ashulikie swala la upatikanaji wa sukari nnchin umekuwa si wakurudhisha hata kwa wananchi wa nchin kwa kilo.1 sukari kupanda mkuu wa.nnchi kulisemea.

Waliominiwa Kama mawakala na viwanda vya sukari wanangalia maslah.yao binafs
 
Kuwaongoza Watanzania ni tabu sana.

1. JK alisafiri sana, Watanzania wakakereka.

2. JPM alikataa safari, pia Watanzania wakadai nchi inakosa fursa.

3. Samia anasafiri, wamerudi kule kwa JK kulaumu.

Ni ajabu!
 
anaitwa Flying president
 
Takwimu kwenye makaratasi na uhalisia wa maisha waishiyo watu vikiwa tofauti sana, hata takwimu ziwe nzuri kiasi gani, utapata shida sana kuwashawishi watu kwamba mambo ni mazuri.

Ni biashara ngapi ndogo ndogo zilizoathirika na huu mgao wa umeme uliodumu kwa zaidi ya mwaka sasa?

Halafu kweli takwimu za serikali ya CCM zinaaminika?
 
Hata kama takwimu haziaminiki, ni bora ziwepo iki kuonesha ni za uongo.

Zisipokuwepo tunarudi kubishana bila namba katika jambo linalohitaji namba.

Pia, serikali mara zote inaweza kukujibu kwamba kama huko nyuma tulikosea, sisi awamu yetu inarekebisha makosa.

Hoja hiyo huwezi kuipangua objectively mpaka ukokotoe namba na kuonesha kuwa kwa namba hizi, hata nyie mnarudia makosa yaleyale tu.

Tatizo serikali ina usiri mkubwa hata kwenye mambo ya haki za kikatiba za wananchi kujua.
 
Ukitaka kujua usiri wa serikali, ulizia mshahara wa Rais ni kiasi gani.

Kwanza, raia tu wa kawaida watakwambia hilo wewe halikuhusu kwa sababu mshahara wa mtu ni siri ya mtu.

Sasa unakuta hata huko serikalini kuna watu wenye ujinga kama huo.

Hawaelewi kwamba utumishi wa umma kuna mambo huwa si ya siri.

Leo miaka 17 sasa hapa JF mimi nimeulizia mshahara wa Rais wa Tanzania ni kiasi gani na hakuna jibu lililonyooka.

Kila ajibuye anakuja na kiasi chake, jambo linaloashiria kwamba hakuna chanzo cha uhakika cha hizo taarifa.

Magufuli kafa na watu hata hatuna uhakika kafa lini, achilia mbali kutokujulishwa kuugua kwake!

Usiri huo wa serikali unawezeshwa na ujinga ulio wa kukithiri wa Watanzania.

Hatujui kudai haki zetu. Haki zilizo zetu tunadhani ni hisani ya walio madarakani.

Hapo unategemea kupata taarifa gani za kuaminika toka serikalini?
 
Kiwanda cha Mbole Tanga kilikufa kwasababu gani?
Skiupenda !! nasema sipendi lakini nalazimika kusema pumbavu kabisa nikiwa na sababu.
1. COVID 19 kwa miezi 20 tu wamelipwa zaidi ya Bilioni 32, leo unashangilia Taifa kusamehewa peremende na China

2. Taarifa ya CAG ina zaidi ya Trilioni moja imepotea, yaani mara 30 , leo unashangilia kusamehewa bilioni 31

3. Kodi ya Kiwanda cha BIA ya miezi 5 tu ni sawa na msamaha wa China.

4. Kuna magari 500 ya serikali yamekaa tu yakisubiri dili la kuuzwa, leo unakuja kushangilia bilioni 31

5. Kuna Mikataba 30 imesainiwa China. Hatujui ilihusu nini na kwanini ni siri. Unaweza kuuza ng'ombe ununue kuku halafu useme umefanikiwa

Halafu mtu anakuja kushangalia upuuzi wa Taifa la watu milioni 60 kusamehewa pesa ya peremende

Nauliza, hivi nani anajua BAJETI ya Bunge! lini uliwahi kusikia .


 
Kama ana afya na hana woga wa kupanda ndege sioni shida. Yule dikteta marehemu alikuwa hasafiri kwa kuwa aliwekewa kibiriti kifuani na siyo sababu ya kubana matumizi.
 
Nani wa kumbabaisha Mwenyekiti Chamani ??!!
Nguvu ya Mamba kumayi !!
 
Duh 🙄 !
 
Wewe Sukuma gang unawashwa na kitu gani?
Kwanini msikubali kuwa Rais Samia sasa ndiyo kiongozi wa nchi hii ya JMT?

Jiwe alishaondoka mjomba ebu funga mkanda tusonge mbele na mama Samia.
 
Mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM lkn linapokuja suala la kiongozi wa nchi kusafiri sina tatizo naye.
 
Umeandika pumba kama zote
 
lbdaa maraisi wa developed state ndio wanafanyiwa izo analysis sio kwetu wachumia tumbo, kikwete alikuwa hivi hivi faida gan unaweza kuzipima kwenye maendeleo ya watu kipindi chake ?
 
Anaweza kukaata, Rais sio robot. Wakati mwingine hao wanaoitwa wataalamu, mabingwa na wabobezi huwa wanafanya mambo kwa maslahi yao. Ian Khama wa Botswana alikuwa haudhurii vikao vya Umoja wa Africa(AU) akisema ni kupoteza muda tu huko.
 
kariakoo kwa wakimbia kodii? apo sokoni kila nikidai risiti naambiwa sio lazima kununua apa nafukuzwa maduka karibu kumi toka mwaka juzi December till leo
 
Urais ni taasisi; taasisi ni watendaji. Hata Marekani ni hivyo even more!
Mbona Rais wa Marekani ni nadra sana kumsikia akisafiri kwenda nje ya nchi? Au watendaji wake hawamshauri hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…