Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Muda wa mechi ya uefa sio kulala
Mnasubiri kipigo cha USG kwa Mkapa ili mumpakishe ndege Kocha siyo? Na mlivyomsema Morrison hafai sasa imekuwaje Baniani mbaya kiatu chake kimekuwa dawa Niamey? Mhindi amewaroga na zile 20 b alizochikichia hadi leo. Kwa taarifa yenu Manara kaonekana Niamey jana.
 
Kesho tunakwenda Dubei. Kwenye maonesho ya nane nane.
 
Huyu mama ni mshamba, huwezi kuwa Rais na ukas nje for 3 weeks. Anakula kodi yetu. Matunda ya Mwungano hayo
 
RAIS HAZURURI
Lengo la ninachokiandika ni kutaka kuonesha umuhimu wa safari za Rais ndani na nje ya Bara la Afrika kwa maslahi ya Tanzania na katika Umoja wa Nchi za Kusini kwa jangwa la Sahara hususani zilizopo katika umoja wa SADC.

Zipo Nchi ttakribani 8 ndani ya bara la Afrika na Nchi 5 nje ya bara la Afrika hivyo kufanya jumla ya Nchi 13. Zipo Nchi alizozitembelea zaidi ya mara moja mfano Uganda (Mara mbili), Msumbiji (Mara mbili), na Marekani ( Mara mbili).

Orodha ya Nchi hizo ni hii:

1.Kenya
2. Uganda
3. Mozambique
4. Malawi
5. Zambia
6. Egypt
7. Belgium
8. Burundi
9. France
10. United Arab Emirates(UAE)
11. United Kingdom
12. Rwanda
13. United States of America( USA)

KENYA
Safari hii ililenga kuimarisha mahusiano na ujirani mwema kati Tanzania na Kenya, uhusiano ambalo ulikuwa umezorota. Kipindi cha awamu ya sita utawala ulikuwa kama umejitenga kiasi na masuala ya umoja katika EAC. Zipo kumbukumbu za maumivu waliyoyapata m aWakenya mfano mwaka 2018 vifaranga vya kuku takribani 11,000 viliteketezwa kwa moto. Haya majeraha yote wakihitaji tiba.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alisema " ujio wako ametupa nafasi ya kurejesha mahusiano yetu" hii inaonesha mahusiano kati ya Tanzania na Kenya kuna wakati yalizorota. Ziara hii pia iliambatana na utiaji saini wa "liquefied petroleum gas" kutoka bandari ya Mombasa kuja Dar es Salaam.

UGANDA
Pamoja na masuala mengine katika ziara hii suala la mradi mkubwa wa mafuta " Tripatite East Afrucan Crude Oil Pipeline ( EACOP).

MSUMBIJI

Katika ziara hii Rais alihudhuria Mkutano wa Jumumuiya ya Afrika Mashariki "East African Community". Hapa yalijadiliwa masuala mengi muhimu kwa uhai wa jumuiya hii mathalani masuala ya; chakula, ulinzi, jinsia na maendeleo, mwitikio wa jumuiya kupambana na ugonjwa la Ukimwi na janga la UVIKO-19.

MALAWI
Taifa hili ni la kwanza kuwa Rais Mwanamke katika ukanda wa Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania alisema pamoja na maendeleo mazuri yaliyopo katika ukanda huu wa Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) bado hatupaswi kuridhika na badala yake tunatakiwa kupambana na umasikini, kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi, maginjwa, ugaidi n.k..

ZAMBIA

Tarehe 24/8/2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzan
ia alikwenda Nchini Zambia kuhuhudia kuapishwa kwa Rais Hakainde Hichilema aliyemshinda mgombea mwenzake Edgar Lungu. Aliwapongeza namna walivyopokezana nafasi. Hii inaonesha lipo alillojifunza huko.

EGYPT
Hapa Rais alikwenda kusaini mkataba mmoja na makubaliano mengine kati ya Misri na Tanzania. Maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ni; Diplomasia, Uchumi, Siasa,Elimu na Huduma za kijamii.

BELGIUM
Katika ziara hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuomba Umoja wa Ulaya kuisafia nchi ya Burundi kwa kuonesha umuhimu wa umoja huo kwa Nchi ya Burundi. Tarehe 17/2/2022 alimtembelea Tundu Antipas Lisu anateishi uhamishoni tangu mwaka 2017 akikwepa kuuawa. Walijaduliana takribani saa moja.

Itaendelea.......
Hapa inaonesha kuwa Rais amefanya ziara muhimu sana za kuifungua Tanzania na haipo ziara ambayo haina nia njema kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa lugha nyingine ni uvivu tu wa kufikiri, kuamini au kukubali kuamishwa kuwa Rais anazurura.
 
Ziara zote zina tija
Hakuna ziara ameenda kutembea bila faida
Kazi iendelee
 
Mwaka jana kaenda Marekani mara 2 mpaka akutana na Mangi Kimambi na wewe Bashite
 
Mwatamani sana ingekuwa ninyi enzi zenu
 
Zi
Ziara za nenda rudiko ndo shida. Kwa nini safari moja usiainishe vya kujadili vyote? Au wadau wanafurahi kumuona karibu?
 
Kumbuka usije changanya Safari Na Ziara hiyo ya Belgium na ufaransa was the same route , maana huu Uzi baadae utatumika Kama referral ya safari za Rais Ulaya , atahesabiwa mara mbili wakati ilikuwa ya Belgium na France ni same Route


Britanicca
 
kuna ambazo hujaweka. Kuna moja ya mkutano wa tabia nchi (UK) aorund last year kabla ya ziara ya Misri.
 
tatizo lako umeandika na huna data, mbona alihudhuria na mkutano wa SADC? kusina mwa Afrika, vipi kuhusu Mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi UK?
 
Ametembelea mikoa mingapi, vijiji vingapi, kusikiliza matatizo ya Watanzania wengi?

Yeye kajikita kwenye ziara, holiday kila mwezi, shopping kila mwezi, kula bata. Hana muda wa kutatua matatizo ya Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…