Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita (6) wa Tanzania mnamo Machi 19, 2021 baada ya mtangulizi wake Rais John Pombe Magufuli kufariki dunia mnamo Machi 17, 2021
Tangu kuapishwa kwake Rais Samia amefanya mengi ikiwa ni pamoja na ziara katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kukuza mahusiano na mataifa
Hizi ni Ziara alizofanya Rais Samia tangu alipopewa dhamana ya kuwa Rais wa Tanzania
Aprili 11, 2021 – Ziara nchini Uganda
Rais Samia alifanya ziara ya siku 1 – ambapo alifanya mazungumzo ya siri na Rais Yoweri Museveni na kisha kuhudhuria utiaji Saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tannga
Mei 04, 2021 - Ziara nchini Kenya
Rais Samia alifanya ziara ya siku 2 - ambapo alifanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kisha kulihutubia Bunge lilijumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili. Pia, alihudhuria na kuhutubia Jukwaa la Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania kwa lengo la kujadiliana kuhusu fursa zilizopo za biashara na uwekezaji kwa Kenya na Tanzania
J
ulai 16, 2021 - Ziara nchini Burundi
Rais Samia alifanya ziara ya siku 2 - ambapo alishiriki shughuli mbali mbali ikiwemo kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania
Agosti 2, 2021 - Ziara nchini Rwanda
Rais Samia alifanya ziara ya Siku 2 - ambapo alizungumza na Rais Paul Kagame pamoja na kushuhudia utiwaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari
Novemba 10, 2021 - Ziara nchini Misri
Rais Samia alifanya ziara ya siku 3 - ambapo alizungumza na Rais Abdel Fattah Al Sisi kuhusu maeneo kadhaa ya ushirikiano na Tanzania ikiwemo nyanja za dipolomasia, uchumi, elimu, utalii na huduma za kijamii. Pia, alishuhudia usainiawaji wa mkataba mmoja na hati 7 za makubaliano kati ya Tanzania na Misri
Februari 14, 2022 - Ziara nchini Ufaransa
Rais Samia alifanya Ziara - amekutana na kuzungumza na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Pia amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Aundrey Axoulay wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo. Pia, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani
Februari 18, 2022 - Ziara nchini Ubelgiji
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen leo Februari 18, 2022
Februari 24, 2022 - Ziara Falme za Kiarabu (UAE)
Rais Samia alifanya ziara ya siku 3, ameshuhudia utiaji saini hati za makubaliano ya mikataba 36 yenye thamani ya zaidi ya sh. trilioni 17.3 iliyohusisha sekta mbalimbali ikiwemo nishati, madini, miundombinu, kilimo na mawasiliano.
Pia, kuwa Mgeni rasmi na kuhutubia kwenye Siku Maalum ya Tanzania kwenye maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji Dubai Siku ya Februari 26 pamoja na Kuhutubia kwenye Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji Februari 27
Aprili 19, 2022 - Ziara nchini Marekani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo a
shiriki kwenye uzinduzi wa makala maalumu iitwayo ‘Royal Tour’ jijini New York nchini Marekani.
Mei 10-11, 2022 - Ziara nchini Uganda
Rais Samia ziara ya siku 2 - atazungumza na Rais Yoweri Museveni ili kudumusha na kuimarisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii. Marais watajadili kuhusu nishati, bishara, usafiri, maendeleo ya miundombinu na sekta ya afya