Safi Sana: Marekani na ujanja wake kaingizwa mkenge na Venezuela kuhusu kuuziwa mafuta

Safi Sana: Marekani na ujanja wake kaingizwa mkenge na Venezuela kuhusu kuuziwa mafuta

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Iko hivi, Marekani kwa kutaka kuikomoa Urusi wakapata mawazo ya kugomea kununua mafuta Yao. Lakini kabla hawajafikia muafaka wa kugomea mafuta ya Urusi wakaona watafuta chanzo mbadala Cha mafuta. Hapo ndio wakapata wazo la kuiomba Venezuela kwa Raid Maduro waweze kuànza téna kuchukia mafuta huko ambako mwanzo waliyagomea kwa kutokumtamvua Rais Maduro badala yake wakaamua kumtambua mpinzani wake aliyekuwa ameshindwa vibaya kwenye uchaguzi aitwaye Guaido.

Wakaona ni afadhali wameangukie Maduro kuliko kuendelea kununua mafuta ya Urusi. Ili kutekeleza sdhima hiyo, Marekani ikayuma ujumbe mzito kwa Rais Maduro wa Venezuela ambaye aliwaambia hakuna shida njoni tuyajenge (si unajua kwenye siasa hakuna sdui wa kudumu au rafiki wa kudumu, kinachoangaliwa ni maslahi!).

Kweli ujumbe mzito ukaenda na Rais Maduro akawapokea kwa bashasha na tabasamu la kufa mtu. Akawaambia hakuna shida mafuta nitawapatia. Wageni hao wa Rais Maduro wakarudi Marekani na moto wa kugomea mafuta ya Urusi maana wameshapata mafuta mbadala. Walipofika tu Marekani, Rais Biden wa Marekani akatoa amri ya kupiga marufuku ununuaji wa mafuta Toka Urusi.

Maduro akasubiri siku mbili Kisha akaioiga mkwara Marekani:

1. Nitawauzia mafuta lakini kwa masharti yafuatayo:
(i). Itabidi mnitambue rasmi kuwa Mimi ndiye Rais halali wa Venezuela tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
(Ii). Wakati nawaauzia mafuta Hilo halitaathiri ushirika wangu na Urusi na nitabaki mwamininifu kwa Nchi ya Urusi!!

Hayo masharti yakawa magumu Sana kwa Marekani na akashindwa kuyatekeleza wakati tayari ameshatangaza kugomea mafuta ya Urusi!! Bei ya mafuta Marekani ghafka ikapanda juu Sana!!

Rais Biden akaamua aiombe Saudi Arabia waongeze uzalishaji wa mafuta Ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya Marekani lakini mfalme wa Saudia akamchunia na hakukubali kupigiwa simu na Biden!! Sasa hivi huu ko Marekani Biden anahaha!

Kaingizwa mkenge na kiburi hakimruhusu kuyakubali téna mafuta ya Urusi.
 
Saudia akamchunia na hakukubali kupigiwa simu na Biden!! Sasa hivi huu ko Marekani Biden anahaha!
Msaudi naona katangaza kuiuzia China mafuta kwa ¥uan badala ya $ na pia kagomea kabisa kupokea simu za Biden chanzo ikiwa US kufufua makibaliano ya nuclear na Iran & kushindwa kumuunga mkono kwenye vita yake isiyo na mwisho kule Yemen
 
US wanakwama sana, wao kamawalivyo sema hawamtambui maduro sasa walienda kuongea nae kama nani.

Mimi ningekuwa Maduro ningewaambia wakaongee na Guaidoa ambae wanamtambua kama rais wa Venezuela.

Safisana Maduro na team yake.
 
Unaweza ukaweka summary!?
Kama ni mvivu wa kusoma pita tu kimya kimya!! Kuna taarifa zinazohitaji context vizuri Ili kueleweka. Sasa kwa mvivu anayesoma mstari mmoja tu wa Biblia huangukia kwenye Imani potofu maana bila context lazima maana itapotoshwa, na context inataka usome mazingira yote ya kabla na baada ya habari lengwa! Kwako hata maelezo haha mafupi utaona ni marefu Sana, pole!!
 
Aisee.. Noma sanaa

Niliiona hiyo ya Saudia kuwachunia ku pickup simu zao ila kuhusu venezuela sikujua kabisa..

No way itabidi akubali masharti ya venezuela tuu...
Unajua mtego wa Rais Maduro katika upana wake uko hivi :
1. Wakiamua kumtambua kuwa ndiye Rais halali tangu uchaguzi mkuu uliopita maana yake ni kuwa pesa zote za Venezuela zilizotokana na mauzo ya mafuta yake huko Marekani, zilizokuwa kwenye akaunti ya Marekani (mabilioni ya Dola) ambazo Marekani wakiamua kumpatia Guaido ambaye ndiye wanayemtambua, hayo maamuzi ni batili na itabidi wazirudishe zote!! Hilo Marekani hawezi! Pia Uingereza iliamua kutaifisha Tani kadhaa za dhahabu zenye thamani ya mabilioni ya paundi.
2. Wakimtambua Maduro maana yake wamtose rasmi kipenzi wao Guaido!! Unajua kuwa Akaunti ya nje ya Venezuela anaimiliki Guaido, na wanamtumia kuipora Venezuela, na hawana namna ya kurudisha Ile waliyopora Hadi Sasa! Na wanampango wa kuendelea kuipora!! Kwa mujibu wa Marekani na washirika wake Serikali rasmi ya Venezuela inaendeshwa na "Rais Guaido" na Ina makao yake uhamishoni Marekani. Kuna Baraza la mawaziri na mabalozi Nchi za nje. Wote wanapata mishahara kutoka Akaunti ya Venezuela iliyoshikiliwa huko Marekani, Uingereza nk. Huu uovu kuukiri Marekani hawezi!!
 
US wanakwama sana, wao kamawalivyo sema hawamtambui maduro sasa walienda kuongea nae kama nani.

Mimi ningekuwa Maduro ningewaambia wakaongee na Guaidoa ambae wanamtambua kama rais wa Venezuela.

Safisana Maduro na team yake.
Hayo mafuta yenyewe ya Venezuela hata akiuziwa still bado mrusi lazima Kuna percent itakuwa anachukua cuz alimsaidia Maduro kubaki madarakani Ni lazima Kuna mikataba itakuwa waliingia ili Maduro Apewe backup
 
Kama ni mvivu wa kusoma pita tu kimya kimya!! Kuna taarifa zinazohitaji context vizuri Ili kueleweka. Sasa kwa mvivu anayesoma mstari mmoja tu wa Biblia huangukia kwenye Imani potofu maana bila context lazima maana itapotoshwa, na context inataka usome mazingira yote ya kabla na baada ya habari lengwa! Kwako hata maelezo haha mafupi utaona ni marefu Sana, pole!!
Msamehe tu TIKTOKER kule hawaaandikagi kitu
 
Back
Top Bottom