Iko hivi, Marekani kwa kutaka kuikomoa Urusi wakapata mawazo ya kugomea kununua mafuta Yao. Lakini kabla hawajafikia muafaka wa kugomea mafuta ya Urusi wakaona watafuta chanzo mbadala Cha mafuta. Hapo ndio wakapata wazo la kuiomba Venezuela kwa Raid Maduro waweze kuànza téna kuchukia mafuta huko ambako mwanzo waliyagomea kwa kutokumtamvua Rais Maduro badala yake wakaamua kumtambua mpinzani wake aliyekuwa ameshindwa vibaya kwenye uchaguzi aitwaye Guaido.
Wakaona ni afadhali wameangukie Maduro kuliko kuendelea kununua mafuta ya Urusi. Ili kutekeleza sdhima hiyo, Marekani ikayuma ujumbe mzito kwa Rais Maduro wa Venezuela ambaye aliwaambia hakuna shida njoni tuyajenge (si unajua kwenye siasa hakuna sdui wa kudumu au rafiki wa kudumu, kinachoangaliwa ni maslahi!).
Kweli ujumbe mzito ukaenda na Rais Maduro akawapokea kwa bashasha na tabasamu la kufa mtu. Akawaambia hakuna shida mafuta nitawapatia. Wageni hao wa Rais Maduro wakarudi Marekani na moto wa kugomea mafuta ya Urusi maana wameshapata mafuta mbadala. Walipofika tu Marekani, Rais Biden wa Marekani akatoa amri ya kupiga marufuku ununuaji wa mafuta Toka Urusi.
Maduro akasubiri siku mbili Kisha akaioiga mkwara Marekani:
1. Nitawauzia mafuta lakini kwa masharti yafuatayo:
(i). Itabidi mnitambue rasmi kuwa Mimi ndiye Rais halali wa Venezuela tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
(Ii). Wakati nawaauzia mafuta Hilo halitaathiri ushirika wangu na Urusi na nitabaki mwamininifu kwa Nchi ya Urusi!!
Hayo masharti yakawa magumu Sana kwa Marekani na akashindwa kuyatekeleza wakati tayari ameshatangaza kugomea mafuta ya Urusi!! Bei ya mafuta Marekani ghafka ikapanda juu Sana!!
Rais Biden akaamua aiombe Saudi Arabia waongeze uzalishaji wa mafuta Ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya Marekani lakini mfalme wa Saudia akamchunia na hakukubali kupigiwa simu na Biden!! Sasa hivi huu ko Marekani Biden anahaha!
Kaingizwa mkenge na kiburi hakimruhusu kuyakubali téna mafuta ya Urusi. Mtamuua Babu yetu jameni