Mbekenga
JF-Expert Member
- Jun 14, 2010
- 3,262
- 8,144
Sijajua kwa nini Arusha ni jiji. Ukiona nyumba yoyote imeangalia lami nenda nyuma ya hizo nyumba utakuta nyumba za udongo, tena sio mbali we anzia Sanawari, mianzini, Kwa Iddi kote huko nyuma ya nyumba nzuri unakutana na za udongo na hii hali huwezi kuikuta Dar wala Mwanza. Hivi hiyo barabara ya clock tower kwenda Kisongo unaiweka kwenye viwango vya barabara za Dar na Mwanza?
Hizo Hotel zinazoongelewa zinadaiwa maana zilishafilisika ni majengo yamebaki. Si unajua anguko la Snow crest, Impala, Ngurdoto, ile ya Sanawari yenye vioo vya bluu. Nenda Mwanza uone jinsi wenye Hotel na guest house walivyo wakarimu wanakupeleka hotelini au guest house na kukurudisha stand kwa gharama zao. Hili huwezi kulikuta Arusha wala Dar na hakuna hoteli iliyofilisika.
Hivyo viwanja vya Ndege angalia takwimu za abiria kwenye viwanja vya Tanzania uone ni uwanja gani unaingiza pesa nyingi.
Angalia stendi ya mabasi ya Singida na ya Arusha ipi bora, Soko la Kilombero na la Magomeni lipi bora?
Nafikiri ungeangalia takwimu na kutembelea nchi hii kwanza la sivyo hoja bila takwimu ni kufurahisha jukwaa.