Sahihi kusema Arusha ndio Jiji bora Tanzania?

Sahihi kusema Arusha ndio Jiji bora Tanzania?

Home thweeet home
IMG_20210830_122927_4.jpg
 
wamepaboresha mno sasa hivi barabara nyingi ni lami tu
kuanzia mjini hadi ngusero
mjini hadi njiro atomic
chekereni hadi usa
barabara zote za levolosi ngarenaro na makao mapya sasa ni lami tu
karibu tena Arusha hakika utapapenda sana

Arusha kwenye barabara tu mko vizuri. Kwingine huko ushuzi m2pu. Mjini vinyumba vya kizamani bora hata ya kahama
 
Cha kwangu kama hakikidhi siwezi cfia,,,lakini wa kaskazini most of them ni kucficfia tu, mara oh moshi inastahili kuitwa jiji [emoji1787][emoji1787][emoji1787] mnalijuwa jiji ninyi!!! Na kahama iitweje?
Kahama ni utopolo mtupu
 
Ukiondoa hali nzuri ya hewa, Arusha ni jiji la ovyo kabisa. Nyumba za ovyo zipo hadi ndani ya CBD, barabara ni nyembamba na hazina hadhi. Barabara nyingi hazina lami nenda makao mapya uone vumbi la ugoro. Arusha ndani ya miaka 60 ya uhuru inafaa kuitwa squalor of Africa
Lami ishapigwa huko kitambo
 
Cha kujivunia ni climate peke yake otherwise ndio Jiji la watu washamba na wasiojielewa
Mtu akinunua IST na simu kubwa anajiona yeye ni bonge la tajiri
Anafunga Barabara mpaka amalize kuongea na simu yake nyie mko hapo nyuma mnapiga honi tu
 
Barabara ya kilimahewa to nyasaka.
Barabara ya sabasaba buswelu via kanyerere
Barabara ya kisesa usagara
Barabara ya nyakato busweru to kahama
Barabara ya iseni to sauti
Barabara ya mkuyuni butimba nk nk

Zipo barabara nyingi sana mwanza
Kwa hiyo hizo ndio barabara za mitaa ya Mwanza sio? 😂😂

Acha kukurupuka
 
Mimi nimefika Arusha ila sioni maajabu. Zaidi ya serikali kulazimisha kuufanya mji wa utalii na makao makuu ya EAC hakuna kingine kipya.

Soon inapitwa hata na Dodoma.

Nielekezeni basi niende wapi ila nijue kweli Arusha ni hatari.
Mkuu kama sio Awamu ya Tano hiyo miji ingepitwa hata na Makambako
 
Sijajua kwa nini Arusha ni jiji. Ukiona nyumba yoyote imeangalia lami nenda nyuma ya hizo nyumba utakuta nyumba za udongo, tena sio mbali we anzia Sanawari, mianzini, Kwa Iddi kote huko nyuma ya nyumba nzuri unakutana na za udongo na hii hali huwezi kuikuta Dar wala Mwanza. Hivi hiyo barabara ya clock tower kwenda Kisongo unaiweka kwenye viwango vya barabara za Dar na Mwanza?

Hizo Hotel zinazoongelewa zinadaiwa maana zilishafilisika ni majengo yamebaki. Si unajua anguko la Snow crest, Impala, Ngurdoto, ile ya Sanawari yenye vioo vya bluu. Nenda Mwanza uone jinsi wenye Hotel na guest house walivyo wakarimu wanakupeleka hotelini au guest house na kukurudisha stand kwa gharama zao. Hili huwezi kulikuta Arusha wala Dar na hakuna hoteli iliyofilisika.

Hivyo viwanja vya Ndege angalia takwimu za abiria kwenye viwanja vya Tanzania uone ni uwanja gani unaingiza pesa nyingi.

Angalia stendi ya mabasi ya Singida na ya Arusha ipi bora, Soko la Kilombero na la Magomeni lipi bora?

Nafikiri ungeangalia takwimu na kutembelea nchi hii kwanza la sivyo hoja bila takwimu ni kufurahisha jukwaa.
Nina makazi arusha, mwanza, na dsm. Unasema kweli kuhusu nyumba za udongo kuwepo ndani ya jiji. Nimeona hilo ungalimited, sakina kibanda maziwa, kona esso, kona Nairobi, soko mjinga, Ostabei, daraja mbili, bwawa la mavi, olasiti, maeneo ya radio safina, etc
 
Arusha nimeshindwa kuwaelewa! Barabara nzuri ila uchafu sasa! Mwanza itaendelea kuwa juu!
 
Uko sahihi. Mkoa wa Arusha ulitakiwa kujengwa zaidi lakini naona kama mashamba ya kahawa yamesogelea sana jiji. Mji ulitakiwa upanuke kuelekea Ilboru, Elkinding'a n.k. Tatizo ni kwamba watu wengi wanafikiri wanaojenga mji ni wazawa wa lile eneo lile. Mji unajengwa kwa kuwekewa miundombinu na Serikali halafu wanakuja wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Mashamba ya kahawa yako karibu na jiji kabisaaa yaani unashuka kwenye ndege unakutana na Mashamba. Hii imefanya mji kuwa mdogo. Arusha uzuri wake hali ya hela ila kuna vumbi balaaaaa. Sekta ya hotel kwa sasa imeshuka kwa mimi ninavyoona Nadhani wanasiasa na corona wamechangia hilo. Nasikia na soko la madini wamepeleka madini yanakotoka (manyara) kama kweli basi hili nalo ni pigo kwa sekta ya hotel.
 
Dar es Salaam/Mwanza nk imepimwa kigamboni/ Nyasaka na maeneo mengine kwa njia ya kukopa Bank na limefanyika kwa mafanikio makubwa sana. Serikali ikainingila kati na kulisimamisha.
Ni kweli nyasaka imepimwa inapendeza kwa kiasi chake kuanzia nyasaka center, zenze, nsumba, hadi PPF kiseke alikokuwa anaishi John Mongela. Huko kigamboni dar es salaam ndo usiseme nadhani dar kwa sasa kigamboni wamejitahidi
 
Mashamba ya kahawa yako karibu na jiji kabisaaa yaani unashuka kwenye ndege unakutana na Mashamba. Hii imefanya mji kuwa mdogo. Arusha uzuri wake hali ya hewa ila kuna vumbi balaaaaa. Sekta ya hotel kwa sasa imeshuka kwa mimi ninavyoona Nadhani wanasiasa na corona wamechangia hilo. Nasikia na soko la madini wamepeleka madini yanakotoka (manyara) kama kweli basi hili nalo ni pigo kwa sekta ya hotel.
 
Back
Top Bottom