Said Lugumi avunja ukimya kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoikabili kampuni yake

Sasa mbona wameishia kukanusha tu hawajatuwekea ukweli wenyewe?huu ni ujinga mwingine tena
 
Taarifa haina mashiko,shilingi ngapi lugumi imelipwa,utekelezaji mpaka sasa ni asilimia ngapi?kazi ilipaswa kuisha lini?
 

Mambo magumu sana....kampuni zinakufa kwa style hii hii
 
Watu wengine ni wa ajabu kabisa Watu wanakuja utetezi dhaifu kama kwenye maswala mazito
 
Lugumi hachomoi.....naye atajibu sichomoi kwani nilichomeka nini?.....Nukuu za baba Riz
 
Hawa wanatuona watanzania mazezeta, yani unasema tuendelee na ujenzi wa taifa, wakati unatuhumiwa kuiba vitendea kazi vyetu vya ujenzi wa taifa. Na kwa taarifa hii kama kweli imetolewa na hao Lugumi basi pasi na shaka wanausika na ufisadi moja kwa moja mana hajakanusha kuhusika kwao na hela za walipa kodi, sana sana wanaturingishia kwamba huyo lugumi hata kukamatwa hajakamatwa. Ila nothng will stand forever, Kuna wale wa macontainer ya bandarini hawakuwahi kuwaza kwamba kuna siku watayalipia ila wameyalipia.
JPM anaweza akawasahau ila kuna atakayekuja mwenye uchungu zaidi atawatumbua tu kama sio nyie basi vizazi vyenu vitalipa jasho la watanzania, its matter of time tu.
 
Kwani taarifa ya CAG imeshawekwa hadharani kwa public?
 
Huuu ndio ule mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika City Lounge ..kwa bwana Juma Pinto ..swahiba wa Riziwani
 
Tunaomba CIA waje na ile ripoti yao. The Lugumi is more than what we think
 
Watanzania wengi wana wivu wa kike,wanataka watu wote wawe masikini
 
Kwanini nilizaliwa mtanzania?


Una haki ya kujuta. Taarifa zile zote kuhusu Lugumi ni upotoshaji kama ni hivyo basi vyombo vya habari na kamati ya bunge ni wendawazimu.
Naona hii ishu inapinduliwa live.

Hapa wasitake kutulaghai inawezekana zile taarifa za kwenda nje zilikuwa kweli labda alikwenda kuchukua vifaa baada ya kupata presha.

Nahisi watakuja na taarifa kwamba mradi ulichelewa kidogo ila vifaa vyote vipo imebaki kuvifunga. baada ya bosi kwenda kuvinunua fasta.
 
hapa Lugumi kaja kumchongea IGP kuwa mkataba haujatekelezwa na yeye yuko kimya ingawa madudu haya kayarithi kutoka kwa baba mkwe Said Mwema.
 
Kweli wewe ni mtu wa propaganda!!
Waliosema Saidi Lugumi katoroka nchi nahisi ni hivyo hivyo vyombo vya ulinzi na usalama.Jana au juzi niliwasikia takukuru wakisema wakimaliza uchunguzi wao watalifikisha suala hili mahakamani.Sasa aliekurupuka toka ofisi ya Lugumi na kuandika hiyo barua ambayo sidhani kama ina tarehe wala reference no na wala cheo cha mwandishi kwenye kampuni hiyo ni nani?

Muda wote toka yaibuke haya walikuwa wanajipanga tu jinsi ya kuandika barua na kukanusha?Mbona barua haitaji idadi ya mashine waliyotakiwa kuuza,idadi iliyowasilishwa na kiasi cha malipo waliyopokea?Najua wapo watetezi watakaokuja na hoja kuwa vyote vipo kwenye mkataba na kama huo ni utetezi ya nini barua tena?kwa maana kama ni mkurugenzi kuwepo nchini tungearifiwa na polisi na sio mfanyakazi wa ofisi ya Lugumi.

Mihuri na hata hizo headed paper unaweza kutayarishiwa ndani ya lisaa limoja pale mnazi mmoja ukitaka.Tunajuaje uhalali wa barua hii.Toka 2011 hadi 2016 kabla ya mambo haya kuwekwa hadharani kwa nini hawakutujuza au wanatafuta utetezi na kinga kwa mtumbua majipu?Najua uzito wa jipu hili kwa mtumbuaji kwani linahusisha pia vigogo wakubwa linahitaji moyo wa kujitoa kwani linahusu mabillioni ya shilingi kama hasara kwa taifa.

Na hata hivyo sitashangaa kama uchunguzi wa sakata hili ukimclear Lugumi au DPP kushauri haipo haja ya kulifikisha mahakamani suala hili na bila hata kutoa sababu yoyote.Sheria za nchi hii ya ajabu zinamruhusu. AJABU!!!!!!
 
Mkuu hata mimi nashindwa kuwaelewa!!! Wanataka kusema nini? Kwamba kwa kuwa Wizara ya mambo ya ndani haijalalamikia chochote kuhusu mkataba huo basi hata taarifa ya ukaguzi hazina maana au?

Huu utetezi wa Lugumi Enterprises Ltd ni dhaifu sana. Wangeonyesha wamefunga mashine ngapi, wapi zinafanya kazi ngapi na wapi labda tungeweza kuwaelewa kidogo. Hati jamaa mbona hawaja lalamika-sasa kama wote ni wapiga deal sio tumeliwa kwa style hiyo. Inaelekea wote watoa tender na watoa huduma lao moja-ni majipu haswa!!!!!
 
Pongezi kwa maswali yako murua na ya kizalendo kwani kwa maswali uliyouliza kwenye mistari michache yanauzito kuliko hiyo barua yao ya kurasa mbili.Kama haya maswali yakijibiwa kwa usahihi basi umma utawaamini bila shaka.
 
Kwa mbali barua hii inafanana na ile ya kukanusha umiliki wa UDA baada ya magazeti kuihusisha na mtoto mmoja wa kiume!
Ukiondoa hii tender ya billion 37, kazi ambazo hii kampuni imeshapewa ni nyingi na za thamani kubwa na malipo yao yanatoka huko huko serikalini. Hivyo ku-clear doubt wangeitisha japo press conference na kuruhusu maswali hata 100 ili kila mwenye mashaka aridhike. Lakini kuja na karatasi zisizo na tarehe wala cheo, Wallah wameongeza maswali hata yaliyokuwa hayajadhaniawa! ...lakini jamani, mbona watz wengi wanajua hii kitu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…