Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeombwa itoe amri ya kuwakamata na kuwashikilia vigogo saba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na John Mnyika kama wafungwa wa madai kwa kukiuka amri ya Mahakama.
Wengine ambao wanatakiwa kukamatwa na kufungwa ni Rose Mayemba, Brenda Rupia, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Gervas Lyenda. Wajibu maombi wengine ni Wasimamizi waliosajiliwa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema.
Maombi ya kukiuka amri ya Mahakama namba 70173, 2025 yamefailiwa mahakamani hapo na Wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini Chadema, Zanzibar Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu pamoja na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, Said Issa Mohamed.
Wanaomba Mahakama itoe amri ya kukamatwa na kushikiliwa kwa wajibu maombi kama wafungwa wa madai kwa kukiuka kwa makusudi amri za Mahakama katika shauri la madai namba 8960 ya mwaka 2025 lililotolewa Juni 10, 2025.
Chanzo: nipashedigital