SAIDA KAROLI : “Sizalii Mwanaume, Kila Mtoto Wangu Ana Baba Yake”

SAIDA KAROLI : “Sizalii Mwanaume, Kila Mtoto Wangu Ana Baba Yake”

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwanamuziki nguli wa nyimbo za asili nchini, Saida Karoli, amewashangaza na kuwagusa wengi baada ya kufunguka kwa uwazi kuhusu maisha yake ya uzazi, mahusiano, na sababu zilizomfanya apate watoto na wanaume tofauti tofauti.

Akizungumza katika mahojiano maalum, nguli huyo aliyewahi kutamba na vibao vilivyobeba ujumbe mzito kama Melisa na Kaisiki, ameeleza kuwa changamoto kubwa aliyokumbana nayo katika maisha ya kimapenzi ni kujikuta akiwa kwenye mahusiano na watu ambao hakuwa na hisia za dhati za mapenzi nao.

Hata hivyo, Saida alibainisha kuwa pamoja na kukosa mapenzi ya dhati kwenye mahusiano hayo, hakuwahi kufikiria au kuchukua hatua ya kutoa mimba, akizingatia pia maadili na ujumbe wa nyimbo zake ambazo zimekuwa zikitetea uhai na kukemea kitendo hicho.

"Kila mtoto wangu ana baba yake. Changamoto zinazokuwa zinanikumba ni kwamba, sina mapenzi na wale watu ninaokuwa nao kwenye mahusiano. Lakini naona kutoa mimba wakati mimi ni msanii ambaye nilishaimba Melisa, Kaisiki, huwa ninavumilia. Ninajizalia mimi watoto sizalii mwanaume. Kwahiyo ninajikuta tayari nina watoto na wanaume tofauti tofauti," alisema Saida Karoli.
Kauli hiyo ya mwanamuziki huyo imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki pamoja na wadau wa sanaa mtandaoni. Wengi wamempongeza kwa msimamo wake wa kulinda uhai na kutokutoa mimba, huku wengine wakimsifu kwa ujasiri wake wa kuongea ukweli kuhusu changamoto za maisha bila kuogopa kukemewa au kuhukumiwa.
1788767039683.png
 
Anaweza kuongea hivyo ukadhani anafurahia ila deep down anaumia Sana kwasababu jamii yetu huwa inahukumu Mwanamke mwenye watoto ambao Baba tofauti
 
Back
Top Bottom