Hakuna mtihani usio na matokeo na hakuna matokeo yasiyo na namna mbadala. Kweli yamekupata sio ndoto, yamekukuta kweli, badala ya kuwaza kwanini mimi, jiambie wewe ni mkubwa kuliko matokeo yako.
Jipe mwenyewe mtihani mpya, kwamba utafaulu mara kumi ya matokeo yale, utakuwa mkubwa kuliko ulivyokuwa, mitihani ya maisha haipaswi kukukatisha tamaa, inapaswa kukutia hasira kuwa wewe ni mkubwa kuliko wanavyofikiria.
Ukitingwa na mawazo na hofu na wasiwasi na changamoto za maisha, toka nenda uwanjani kacheze mpira au kaangalie sinema au nenda usikilize nyimbo unazozipenda au nyanyua begi kacheze gofu, fanya chochote ambacho kitakupa furaha, maisha haya ukiwaza sana unaweza ukafanya mambo ya ajabu, usikate tamaa ni mapito tu.