Nadhani kama nchi, lazima tulishafanya study ya saikolojia na tabia za kabila, wilaya, mkoa wa nchi yetu. Hii inasaidia kiongozi akifika huko, anajua jinsi ya ku-deal na watu wa upande aliopo.
Hivi karibuni nilimsikia TAL akilalamika jukwaani, kabla ya kulalamika, ailikuwa akitoa historia ya jinsi JPM alivyomshughulikia kweli kweli, na wakati akitoa maelezo hayo, baadhi ya wananchi walikuwa wakitoa sauti za vicheko. Lissu akahoji, kwamba mimi ninawasimulia madhila niliyopata halafu mnacheka, akauliza kuna jambo la kuchekesha na kifurahisha hapo?
Hili hata mimi lilinitia huzuni, jambo la mtu kupigwa risasi linatakiwa kusikitisha na kuhuzunisha pale linaposimuliwa. Watanzania wanacheka, sasa jambo gani litamfanya mtanzania asikitike?
Tumekuwa tukiona hata majukwaani, inapotokea kiongozi kaonyesha ukatili, wananchi humshangilia, mpaka leo watanzania wakikumbushwa ukatili wa JPM, wao hukataa, wanaamini kwamba wale waliookotwa kwenye viroba, utekaji, na mengine machafu, kwa sio "issue".
Nini kimetufikisha hapa? Nani ana wajibu wa kusimika wema katika nchi? Kwa nini watu makatili wanafurahiwa sana na watanzania?