hiyo ni miratul muhammad...alimuweka mkao gani a'sha? kijamaa kwa uchu noma..hahahahaaa..
Usi panic, mbona uozo wa wachungaji upo mwingi tu, pata na hii:
FRIDAY, 19 JULY 2013
Na Kelvin Lameck
JESHI la Polisi Kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam linamshilikia kwa uchunguzi Mchungaji wa Kanisa moja la Kilokole (jina tunalihifadhi) kwa tuhuma za kuwalawiti kwa nyakati tofauti watoto watatu.
Mbali ya mchungaji huyo kushikiliwa katika kituo hicho, wapo watuhumiwa wengine wawili mmoja akiwa ni mdogo wake mtumishi huyo wa Mungu na msichana aliyekuwa akiwapeleka watoto hao kufanyiwa unyama huo. Vitendo hivyo vinadaiwa vimekuwa vikifanywa na mchungaji huyo kwa nyakati tofauti maeneo ya Ukonga Moshi Bar jijini Dar es Salaam.
Endelea...
Ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi wa kituo hicho aliyejitambulisha kuwa ni mkuu wa utawala hakuwa tayari kuthibitisha tukio hilo zaidi ya kusema hajui chochote kutokana na kituo hicho kuwa na matukio mengi.
“Sijui chochote kuhusiana na tukio hilo. Hapa kituoni kuna matukio mengi na mimi si msemaji,” alisema ofisa huyo.
Akizungumza na Jambo Leo, Polisi Jamii aliyeshiriki kuwakamata watuhumiwa hao (jina tunalihifadhi) alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa watatu wanashikiliwa katika kituo hicho.
“Tukio hilo lipo, juzi tulimkamata msichana mmoja (jina tunalo) aliyekuwa akimpelekea watoto hao mchungaji huyo ili akawalawiti,” alisema polisi jamii huyo.
Alidai kuwa mchungaji alianza vitendo hivyo muda mrefu, ambapo mwanzoni mwa mwaka huu, alimfanyia msichana huyo ambaye anashikiliwa katika kituo hicho akidaiwa kuwapeleka watoto hao kwa mchungaji huyo.
Polisi huyo alidai kuwa katika tukio hilo la kwanza, lilisuluhishwa na wahusika na kumalizwa kimya kimya, ambapo aliendelea kufanya vitendo hivyo kwa watoto wengine.
Aliweka wazi kuwa kukamatwa kwa mchungaji huo kulitokana na watoto hao kuvujisha siri hiyo baada ya kubanwa na kukiri kufanyiwa mchezo huo mchafu.
Juzi na jana gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala ili athibitishe tukio hilo, lakini hazikuzaa matunda baada ya kupigwa simu yake mara kadhaa ambapo alikuwa akisema apigiwe baadaye yupo msibani.
Naye Abdallah Amiri, anaripoti kutoka Igunga kuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, linamshikilia Timotheo Elikana (41) mkazi wa Kijiji cha Mwanzugi, Kata ya Igunga kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 15.
Akiwa kituo cha Polisi cha Igunga, Maria Philipo ambaye ni mama wa mtoto huyo, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 15, 2013, majira ya nne usiku wakiwa nyumbani kwao.
“Nilimuona mume wangu akinyata taratibu na kuingia katika chumba ambacho alikuwa amelala mtoto huyu akiwa na mdogo wake. Baada ya kufika chumbani alianza kumbaka mtoto,” alieleza Philipo.
Alisema baada ya mtoto huyo kupiga kelele, mtuhumiwa huyo alitoka katika chumba hicho akiwa utupu na kurudi katika chumba ambacho hulala na mkewe.
“Sikujua anakwenda kufanya nini, kwa sababu mume wangu huwa anatabia ya kuingia katika chumba cha watoto wakiwa wamelala, hivyo sikuwa na mawazo kwamba anakwenda kufanya unyama huo.
“Hili ni tukio la pili kwani wakati tukiwa Wilaya ya Kiomboi mkoani Singida pia mume wangu alimbaka mtoto huyu na nilikwenda kulipoti kituo cha polisi, polisi walipokwenda kumkamata alikimbia.
“Mume wangu amemkatisha mwanangu masomo ya shule ya msingi. Kwani mwaka juzi alikuwa anasoma Shule ya Msingi Kiomboi darasa la sita na angehitimu mwaka jana, lakini kwa sababu ya kufanyiwa kitendo hicho na baba yake aliamua kutoroka na kwenda kuishi Dar es Salaam.
“Mimi nimechoka na vitendo vya kinyama anavyovifanya mume wangu kwa binti yangu huyu mdogo, hivyo naomba sheria ifuate mkondo wake ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi na pia asirudie,” alisema mama huyo huku akitiririsha machozi.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Igunga, Abeid Maige alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili akajibu tuhuma zinazomkabili
meck lameck at
13:28