Mawakili Alfonce Lusako na Emmanuel Chengula wakishirikiana na wenzao wamefungua Kesi Mahakamani dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipinga 'makubaliano ya mkataba' ulioingiwa baina ya Serikali hiyo na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World, makubaliano yanayolenga uendelezaji wa Bandari Nchini
Katika Kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambao washtakiwa wake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt.Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi,
ambapo Mawakili hao wameeleza kuwa Washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na makosa yafuatayo:
1.) Washtakiwa namba 2 na namba 3 wanashtakiwa kwa kusaini Mkataba wa Kimataifa na kuupeleka Bungeni kwaajili ya kupitishwa bila kushirikisha Umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa Wananchi kutoa maoni yao, kinyume na Sheria ya raslimali za taifa namba 5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2),
2.) Washtakiwa namba 1 na namba 4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza Wabunge vibaya kupiga kura ya "NDIO" badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama Sheria inavyotaka (Natural Wealth and Reasource contract Act) namba 6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6,
3.) Mshtakiwa namba 1 na 4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza Bunge vizuri kufanya kazi yake ya kuishauri Serikali na kusimamia maslahi ya Umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63 (2) na (3) ya Katiba ya Nchi,
4.) Mshtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai wenye vipengere vinavyovunja Katiba, Ibara ya 28 (3) pamoja na Sheria mbalimbali za Nchi,
5.) Washtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa 'hovyo' unaozigawa raslimali za taifa za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya Nchi, kinyume na Katiba, Ibara ya 1, 8 na 28,
6.) Kwamba, Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai una vipengere vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa (National Sovereignty) na 'kuuza' uhuru wa Nchi, kinyume na Ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba, Nk
Washtakiwa wote wameitwa Mahakamani July 03.2023