Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Siyo atakuwa ameshapatikana..

Alishapatikana wiki 2 zilizopita Rais alipokwenda ziara Dubai..

Mwekezaji huyo anaitwa DP WORLD
Upo sahihi mkuu Raisi alikutana na wakurugenzi wa DP World alipokuwa ziarani Dubai.

Hili suala la ubia tayari tunalo ambapo yupo na TICTS ambao wamepewa gati namba 7-11 wanahudumia meli za containers na Hawa wapo chini ya Hutchinson Holding ya Hong Kong China.

Miaka 2 nyuma Kipindi Cha Mh. Dr Magufuli kulikuwa na tetesi za kuwa mkataba wa TICTS ukiisha ilikuwa hakuna kuongeza na angeleta vifaa huko kurudi serikalini.

Nchi nyingi wamewapa Wabia Port Operators bandari zao Kwa mikataba tofauti, Msumbiji na Somalia wamewapa DP world.

Hii hapa ni list ya port Operators wakubwa Duniani
Tayari sisi tunae Hutchinson Holding (TICTS).Bandari nzima asipewe mbia apewe gati hizo hizo za container hizo nyingine TPA iongeze maboresho kwenye vifaa vya kisasa na technology mpya.
 
Waliwang'oa viongozi wabunifu wakawekwa wa kwao wakaanza kutafuna wameshindwa kuwarejesha wa zamani kwa aibu ndio wanaonelea kuja na mawazo ya mbia!!!
 
Tuna watanzania wazalendo wa kutosha kuendesha bandari zetu zote na zikaleta tija. watu type ya Mchechu NHC wapo tuwatumie kwanza kabla ya kuwapa wageni chakula mezani.
 
I absolutely support this. TPA wameshindwa kuendesha hiyo bandari bora watu wengine wajaribu hatuwezi kuendelea kupoteza muda, nguvu na mapato kwa kigezo cha uzalendo. Ikiwezekana hata TRA wapewe wabia maana wabongo tumeshindwa kazi ndo ukweli mchungu.
 
Wewe ukifanya mwenyewe unakusanya Bil 90 lets say kwa mwezi hapo Bandari - Mwekezaji anakuja anakwambia atakusanya Bil 400 afu wewe atakupatia Bil 300. Mkataba wa miaka 10 with uplift ya 5% kila mwaka , je utakataa ama utakubali ?
Tatizo lao huwa wanasema hivyo hivyo, nitakupa Bilioni 300 lakini nifanye maboresho then nipe Grace period ya 5 years kisha naanza kukulipa, baada ya huo muda anakwambia napata hasara tu siendelei na mkataba. . . akili kumkichwa
 
Wapigaji tu
 
Faiza nakuelewa vizuri sana. Ubarikiwe. Hata Polisi waingie ubia na mashirika mahili ya ulinzi.
 
Mtuonee huruma jamani khaa!
 
Wamekuwa kama mamba hasikii mpaka damu zimtoke...Hakuna hata kimoja chakuonyesha kilifanikiwa kwa mawazo haya mufislisi lakini bado wanataka tu kutuaminisha...Watu wasiojiamini wala kuwa na uthubutu kwa jambo lolote!
 
Haya mawazo ya ovyo ni ya wapigaji tu. Yaani una bandari na kuna mataifa mengine yanatumia ushindwe kuendesha hadi unatafuta ubia? Isitoshe mwenyewe ushagharamika kupanua kwa mabilioni. Haya mawazo ya ovyo kabisa.
Wajinga kama kina madilu nape na makamba ndio watakuja na mawazo kama hayo. Safari za nje za kijinga kwenda kuwafuata eti consultants. Unafikiri washauri wamarekani au waingereza au wengine wowote ukiwauliza siwatawauzia bandari kampuni za kigeni?
Linalotakiwa ni usimamizi mathubuti wa serikali. Rais akiwasikiliza wahuni tutaweka wabia hadi kuendesha jeshi polisi na magereza. Hapo tutakua huru kweli?
 
Hii chuki itakufanya ukose mbingu, angalia dada yangu...Nilikuwa nakuamini sana enzi hizo kwa balanced opinion; haya ya siku hizi daah!
 

It is not a bad thing to look for a partner or a concessionaire to invest and run the Port.

In 1996, I was in the USA, and witnessed the Port of New York looking for a company to manage it. Do you know who won the tender? It was the Port of Dubai.

However, the US Govt later changed its mind and said it was going to repeat the exercise.
 
Sijakuelewa nilete ushahidi wa nini?
 
Hatari sana ! bandari ya Zanzibar nayo atapeleka Mbia ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…