Ushoga ni sehemu ya haki ya kujiamulia mambo ya mtu binafsi.
Ni haki ya binadamu na haki ya kikatiba iliyo ndani ya haki ya kujiamukia mambo ya mtu binafsi.
Serikali imesaini mikataba ya kimataifa kuhusu suala hili ama moja kwa moja ama kwa kuzunguka.
Kwa kuelewa jambo hili, ndiyo maana Paul Makonda alivyoanzisha vita dhidi ya mashoga na kusema atapita nyumba kwa nyumba kuwatafuta, watu wa kwenye serikali wanaoijua dunia wakamkana na kusema hiyo ni kauli yake binafsi, si kauli ua serikali.
Na hiyo ilikiwa serikali ya wakagi wa Rais John Pombe Maguguli. Jiwe mbabe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa muda huo, Dr. Augustine Philip Mahiga, alitoa msimamo huo wa serikali.
Ushoga ni lifestyle tu watu wamechagua, kama hupendi hulazimishwi kuwa shoga na wewe una haki ya kuishi unavyotaka.
Yani wewe kumshambulia mtu aliyeamua kuwa shoga kuhusu ushoga wake ni vibaya sawasawa na shoga kukushambulia wewe kwa sababu umeamua usiwe shoga.
Fikiria.
Wewe ungekuwa unaishi dunia ya mashoga, hakafu mashoga yanakulazimisha uwe shoga, usipokuwa shoga yanakuandama, wakati wewe hupendi ushoga, ungejisikiaje?