Source: Youtube-wakiliTv, taarifa ya Wakili Dickson Matata
Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.
Sasa watanzania wataingia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha kumuita tapeli wakati hana hukumu ya mahakama iliyompata na hatia ya utapeli, na kumharibia jina na biashara zake.
Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.
Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.
Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.
Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa