Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Hapa chadema iweke pembeni, wote tumeona viashiria vya utapeli unaosaidiwa na mahakama kudhulumu haki za wanyonge,tuunganishe nguvu kupambana na udhalimu huu wa akina mahululu ambao wapo ccm wapo chadema,mwenye haki na aipate haki yake,na siyo tu aipate ila wote tuone ameipata.
 
Na kiwanja amesha kigawa.
Uki fuatilia vizuri una weza kuta huyu dada ana uhusiano na Waziri.
Huwezi vunja nyumba ya mtu bila notisi wala kumsikiliza.
 
kufanya chochote kinachoathiri maslahi haya ya watu kunatakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria. hata rais hayupo juu ya sheria,
Mkuu hoja yako iko kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Kwa katiba yetu rais yuko juu ya sheria. Ndiyo maana hahojiwi wala kishitakiwa na mtu ama chombo chochote hata kama akipora ardhi ama kuwaua watu wa wilaya yako wote.

Jiwe alinyang'anya ekari 33 za mhe. Sumaye alizokuwa anamiliki kihalali kule Mabwepande na ekari 200 za kule Mvomero kukiwa na ng'ombe zaidi ya 500. Jiwe hakufanyowa chochote.

Jiwe alikataza mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani iliyowekwa kikatiba hakufanyowa chochote.

Jiwe alimuondoa prof. Asad ktk nafasi ya CAG wakati katiba imemzuia kufanya hivyo lkn hakufanyowa chochote.

Samia amemuondoa spika Ndugai kiihuni na hajafanywa chochote.

Mifano hii yote inathibitisha kuwa rais wa Tanzania yuko juu ya sheria.
 
Suluhu siyo kutumia ubabe wa kiongozi. Mahakama ndiyo chombo cha kutoa haki.
Mahakama sasa hivi wanatakuwa kujithamini hii trend ya wananchi kukimbilia kutafuta suluhu kwa wanasiasa mihimili miwili inatakiwa ijitathimini kama iko relevant kwenye nchi mihimili hiyo ni ya serikali wale wafanyakazi wa .kudumu walioko maofisini maofisa ardhi na Mahakama

Ikifika mahali wananchi wanawaamini zaidi wanasiasa kuliko wasomi waajiriwa serikalini na mahakimu na majaji jua kuna shida kubwa kwenye nchi ya hiyo Mihimili na wananchi walio wengi hawana imani nao

Wao ndio wajitadhimini

Kifupi serikali performance appraisal ya mfanyakazi ofisa ardhi ihusishe kipimo.cha je kazalisha migogoro ya ardhi ? Kama ndiyo atimuliwe kazi bila kulipwa hata mia na Hakimu au jaji anayesababisha wananchi walio wengi wakose imani na mhimili wa Mahakama watafute namna ya kumtoa kuhukumu kesi awekwe hata kuwa mkuu wa kitengo cha mapokezi au cha kutia photocopy ya karatasi za kesi
Ule mrundikano wa watu kujazana kwa wanasiasa awe makonda au Slaa au waziri mkuu Majaliwa inaonyesha wazi watendaji wa serikali kuna maeneo wamepwaya na mahakama zimepwaya

Hilo ni hatari kwa usalama wa nchi serikali na mahakama zichukue hatua na mahakama ichukue hatua kurudisha confidence za wananchi kwa mahakama confidence ambayo kwa sasa wananchi wengi hawana confidence na mahakama
 
Watanzania wameonewa saana, wamezulumiwa saana Viwanja vyao, ngoja matapeli wa viwanja pia wajue maumivu Waliyokuwa wanapitia Watanzania wanyonge.
 
Watanzania wameonewa saana, wamezulumiwa saana Viwanja vyao, ngoja matapeli wa viwanja pia wajue maumivu Waliyokuwa wanapitia Watanzania wanyonge.
Sahihi hizo mali zao za dhuluma wacha mighorofa yao ipigwe chini na magreda hadi waumwe visukari na na kupata stroke, na pressure ziwapabde juu wafe wapuuzi wakubwa matapeli hao hawana faida kwa dunia wafe tu dunia na Tanzania matapeli wapungue
 
huyo tapeli anataka kushindan na dola ataiweza?
 
Mtoa mada nadhani hujui ukubwa wa tatizo la migogoro ya ardhi,na mara nyingi masikini ndo wanaoonewa sababu hawana uwezo wa kushindana na wenye pesa na connection.
 
Jamaa ni ya tapeli anatafuta kizingizio tuu
 
Acha kutisha watu kijana, sheria zifuate mkondo wake "Nani mmiliki halali wa eneo husika" nani mvamizi, docs zilipatikana kihalali?, hakuna aliyezulumiwa? Historia ya eneo ipoje?, mkale wa eneo alikuwa ni nani?, Yapo mambo ya msingi ya kufuata, docs pekee siku hizi hazitoshelezi, physical witness inasemaje?, majirani wanasemaje? Mtu wa awali kuanza kununua anasemaje juu ya historia ya eneo?, naandika hapa nikiwa na hasira sana ya kudhulumiwa eneo langu, Mbezi beach, goigy plot no. 471,block A.
 


Katiba inampa mamlaka Rais kufanya jambo ambalo haliwezi kuhojiwa mahakamani.. waziri ametumwa na president hivyo anavunja kwa Presidential power.
 
Tulidhani mzee wa Isimani Kaka Lukuvi aliimudu Sana hii wizara, kumbe aliacha migogoro kibao. Alichoweza Ni kutulipisha Kodi ya 1500 kila mwezi regardless ya thamani ya kiwanja.
 
Umeshaacha kunywa pombe za kienyeji.....mataputapu,naona machicha yanaturukia huku
 
Dola ya Samia hamuonei mru, na Silaa ataondoka, take my words, au atakatwa mkia
Kwani kuna mtu kasema ile wizara ni yake.
Ofisi za uteuzi ni za kupita.
Ila hataondoka kwa sababu ya gorofa alilovunja bali kwa sababu ya kugusa interest za wakubwa.
Hasa wenye vituo vya mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…