Hii sasa ni pattern of behaviour inayojitokeza. Watanzania wa twitter republic na wafuasi wa upinzani ni mahodari sana wa kukatisha tamaa viongozi hasa mawaziri wanaojaribu kurekebisha mambo. Same kwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapojaribu kutatua migogoro.
Ilikuwa hivi hivi kwa Jaffo, Gwajima na sasa mnaanza kwa Slaa. Hata sijui mnataka nini, hakuna siku utaamka utakuta mambo yapo shwari tu lazima kuwe na watu wakupambana kuyaweka sawa.
Wewe una shida kichwani mwako ya kuchakata mambo reasonably..
Unawaamini hawa viongozi kuliko hata unavyojiamini wewe mwenyewe ukisahau kuwa hawa ni binadamu wenye tamaa na matamanio yao pia wanayoweza kuyapata kwa njia zozote iwe za haki au haramu..
Laiti kana ukimsikiliza huyu wakili mwanzo hadi mwisho bila shaka ungekuwa na maoni tofauti na hiki ulichokiandika hapa..
Sisi wananchi hatuna shida na kiongozi anayefanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ikiwemo sheria kuu ya nchi yaani KATIBA. Shida iko kwa viongozi dizaini ya Jerry Silaa wanaotumia nafasi na madaraka yao kifisadi ili kujinufaisha wao. Kwa hili Jerry Silaa hakuwa anamtetea mnyonge yeyote bali tamaa zake tu..
Na kwa maelezo haya ya wakili huyu juu ya sakata hili, haina shaka yoyote kuwa Waziri Jerry Silaa ame - mess up big time na ni lazima akemewe na kuchukuliwa hatua stahiki za kisiasa na kisheria ili ajutie matendo yake mabaya na viongozi wengine wajifunze toka kwake...
Inawezekana huna bundle la kutosha kuisikiliza maelezo ya wakili huyu anayemtetea aliyeathiriwa na maamuzi na vitendo vya waziri huyu mwanzo mwisho ili umwelewe..
Kukusaidia ni kuwa wakili huyu, ametoa hoja kadhaa kumtetea mteja wake na zikithibitishwa na nyaraka mbalimbali za serikali hii hii aliyomo Jerry Silaa (waziri wa ardhi);
1.
Kwamba, huyu aliyevunjiwa nyumba yake (Johnson Mahuru) ana nyaraka halali za umiliki wa kiwanja na nyumba iliyovunjwa..
2.
Kwamba, huyu mama (Naomi) anayetetewa na Waziri Jerry Silaa na anayedai ni mmiliki wa kiwanja hicho alishashindwa kuthibitisha umiliki wake kwa kesi mbalimbali alizofungua mahakamani na hukumu za kesi hizo alizoshindwa ziko on record..
3.
Na kwamba, Wakili wa aliyebomolewa nyumba anasema kuwa kiini cha mgogoro huu ambao umesababisha Waziri kujiingiza kichwakichwa na kujichukulia sheria mkononi mwake na kubomoa nyumba ya mtu ni ugomvi binafsi wa ndugu Johnson (mmiliki wa nyumba iliyobomolewa) na kamishina wa ardhi wizarani ndugu Nonge (kama sijakosea)..
SASA HEBU JIULIZE MWENYEWE MASWALI HAYA;
A: Mpaka hapo na kwa kiongozi wa level ya waziri na analiyeapa kulinda katiba na kusimamia haki za watu wote, katika situation ya watu wawili wanaogombania kiwanja kimoja busara ingemwongoza kuchukua hatua gani eti kwa akili yako wewe ndugu
Mayor Quimby?
B: Na hivi, ni scenario gani inaweza kupelekea jengo kubomolewa? Bila shaka ni lile lililojengwa kwenye eneo lisiloruhusiwa kisheria na mahakama kuthibitisha hivyo na kutoa amri libomolewe..
Kwenye scenario hii ishu iko tofauti kabisa. Huu ni mgogoro wa watu wawili wakidai wote ni wamiliki wa kiwanja. Sasa huyu waziri kwanini akaenda kubomoa nyumba ya mtu?
Katika mazingira haya akikemewa na kukosolewa iweje useme anakatishwa tamaa? Je, huu si kwamba ni ujinga wa waziri huyu na hivyo amejiingiza mwenyewe kwenye tatizo?
Ndugu Mayor Quimby tunataka viongozi wetu wafanye kazi na kutekeleza majukumu yao vyema lakini iwe kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na zaidi sana katiba ya nchi ili kutoa haki sawa kwa kila raia si kama alivyofanya waziri wako!!!