Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Shikilia hapo hapo jerry.Dawa imeanza kuingia.piga kazi hawa chawa w matapeli wackutishe kabisaa.
Umeshaangalia na upsnde wa hasara Kwa serikali? Au yaleyale ya Awamu ya tano lakini kwasasa hasara kila kona. Tujifunze kitu basi.
 
Hii sasa ni pattern of behaviour inayojitokeza. Watanzania wa twitter republic na wafuasi wa upinzani ni mahodari sana wa kukatisha tamaa viongozi hasa mawaziri wanaojaribu kurekebisha mambo. Same kwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapojaribu kutatua migogoro.

Ilikuwa hivi hivi kwa Jaffo, Gwajima na sasa mnaanza kwa Slaa. Hata sijui mnataka nini, hakuna siku utaamka utakuta mambo yapo shwari tu lazima kuwe na watu wakupambana kuyaweka sawa.
Migogoro na kero sugu ndio mitaji ya wanasiasa....sasa ikitatuliwa watakosa agenda........

Mwanasiasa anaweza kulalamikia uozo pahala fulani hatua zikichukuliwa yeye tena analalamika......
 
Ni ubatili mtupu na uonevu. Tulisema haya mambo iachie Mahakama itoe haki. Jerry Slaa hawezi kutoa haki maana hana mamlaka ya kutoa haki. Anaweza aka-initiate process ya kupatika haki na si kutoa maamuzi kama vile yeye ni mahakama. Mfano kuvunja Ghorofa ya mtu bila amri ya Mahakama.

Sikiliza kisa cha kuhuzunisha cha ukiukwaji Mkubwa wa Haki uliofanywa na Jerry Slaa!

Verry unpleasant kwa mtu wa level ya kwake kufanya alichokifanya

View: https://youtu.be/xTWIKdgZxrQ

Waziri Slaa anafanya kazi kwa kutumwa na bosi wake SSH, na jamii yetu ilishaharibiwa sana na wapigaji kiasi kwamba ni ngumu kumuamini mtu tu kisa anaongea mbele ya kipaza sauti na anajifanya kutetea haki za watu.

Wapigaji pia wanao uwezo wa kuinunua jamii mawazo yake kupitia hizi hizi media zetu. Kuna watu wameonewa sana na wana haki zao na katika hizi vita wanapobanwa wezi na wapigaji wa miaka na miaka, kilio chao pia husikika.
 
Ni ubatili mtupu na uonevu. Tulisema haya mambo iachie Mahakama itoe haki. Jerry Slaa hawezi kutoa haki maana hana mamlaka ya kutoa haki. Anaweza aka-initiate process ya kupatika haki na si kutoa maamuzi kama vile yeye ni mahakama. Mfano kuvunja Ghorofa ya mtu bila amri ya Mahakama.

Sikiliza kisa cha kuhuzunisha cha ukiukwaji Mkubwa wa Haki uliofanywa na Jerry Slaa!

Verry unpleasant kwa mtu wa level ya kwake kufanya alichokifanya

View: https://youtu.be/xTWIKdgZxrQ
 
Kabisa...anaendesha mashitaka yeye, anatoa hukumu yeye, tena siku hiyo hiyo, na siku hiyo hiyo anavunja, kwa nini asitoe hata siku 90 ili mtu ambaye hajaridhika aende kwa Waziri Mkuu, au Rais au Mahakamani?

Kuna issue ya yule mbunge Kamani, kale ka dada, only to find out ni girlfriend wake wa enzi za Uvccm, kapata uwaziri katoka mbio kwenda kumkabidhi baba mkwe wake kiwanja huko mwanza.

Mahakama imeweka mifumo rasmi, unaanza ngazi hii, hujaridhika, unaenda mbele, hujaridhika, unaenda mbele, sasa Jerry ndio Alfa na Omega, anatukana mahakama mbele ya wananchi, sasa serikali moja kwa nini mmoja anatukana taasisi ya mwenzake?

Kitendo cha kuhamasisha wananchi wasiheshimu taasisi ya kikatiba ni uhaini na anapaswa kujiuzuru mara moja. Anabaki kufanya nini wakati aliapa kuilinda katiba, katiba hiyo ndani yake ina mahakama, na yeye anahamasisha uasi wa wananchi dhidi ya mahakama?
Hao wezi wanapoiba na kutaka kuwadhulumu watu hujificha katika kichaka cha sheria na mahakama, unampora mtu haki yake na akianza kuidai unakuja na mlolongo wa taratibu za mahakama!.

Mzee Mushi yupo ndani na siku zote alikuwa na documents feki zenye kuitaja hiyo hiyo mahakama. Huku Mbezi Beach alitaka kuvamia eneo la mtu na wenyewe walikuwepo siku hiyo, risasi zikalia na bahati nzuri hakufa mtu kwani greda lilikimbizwa mapema na yeye akaingia ndani ya pick up yake akakimbia.
 
Nashindwa kuelewa naomi anatokea wapi katika hili sakata
Au alikua mmliki wa mwanzo?
Ila naamini huyo naomi hawezi kidai hicho kiwanja miaka nenda miaka rudi bila sababu yoyote haiingii akilini
Kwanin akidai hicho kiwanja miaka yote?
 
Wameibia sana watu huku mbezi beach na kinondoni nzima kwa ujumla, ni muda wa kuwafunga jela na kuvunja hizo nyumba walizojenga kwa njia haramu.
Ki ukweli
Mtu yoyote anaweza uliza why naomi anadai hicho kiwanja?
Kweli mtu aje tu aanze kudai kiwanja miaka nenda rudi
Au walimpora kweli?
 
Kabisa...anaendesha mashitaka yeye, anatoa hukumu yeye, tena siku hiyo hiyo, na siku hiyo hiyo anavunja, kwa nini asitoe hata siku 90 ili mtu ambaye hajaridhika aende kwa Waziri Mkuu, au Rais au Mahakamani?

Kuna issue ya yule mbunge Kamani, kale ka dada, only to find out ni girlfriend wake wa enzi za Uvccm, kapata uwaziri katoka mbio kwenda kumkabidhi baba mkwe wake kiwanja huko mwanza.

Mahakama imeweka mifumo rasmi, unaanza ngazi hii, hujaridhika, unaenda mbele, hujaridhika, unaenda mbele, sasa Jerry ndio Alfa na Omega, anatukana mahakama mbele ya wananchi, sasa serikali moja kwa nini mmoja anatukana taasisi ya mwenzake?

Kitendo cha kuhamasisha wananchi wasiheshimu taasisi ya kikatiba ni uhaini na anapaswa kujiuzuru mara moja. Anabaki kufanya nini wakati aliapa kuilinda katiba, katiba hiyo ndani yake ina mahakama, na yeye anahamasisha uasi wa wananchi dhidi ya mahakama?
Why complicate matters, kuna watu wanatumia udhaifu wa sheria na kutumia loopholes zake kudhulumu.
Mimi limenipata ndio maana namsupport Waziri Slaa.

Mtu katapeli na ni very clear katapeli, na hati zote ni za kughushi.
Hata akijenga ghorofa 15 . BOMOA TU, si alijua risk za kutapeli?
 
Huko Mbezi Africana, Salasala na maeneo jirani kuna mtandao mkubwa wa watu kuvamia na kupora ardhi na kughushi nyaraka.
Waziri analijua hilo.
Kuna watu wamekufa kwa kupoteza ardhi zao kwa matapeli hao wa ardhi.
Hawa wanaokuja kutetea wezi kwa kuandika threads hawajui uchungu wa kuitafuta ardhi ambayo pengine mtu alitaka kudhulumiwa.

Wanafanya uchawa kama uchawa mwingine wowote ule, wakijaribu kupotosha lengo pana la waziri Slaa.
 
Hii sasa ni pattern of behaviour inayojitokeza. Watanzania wa twitter republic na wafuasi wa upinzani ni mahodari sana wa kukatisha tamaa viongozi hasa mawaziri wanaojaribu kurekebisha mambo. Same kwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapojaribu kutatua migogoro.

Ilikuwa hivi hivi kwa Jaffo, Gwajima na sasa mnaanza kwa Slaa. Hata sijui mnataka nini, hakuna siku utaamka utakuta mambo yapo shwari tu lazima kuwe na watu wakupambana kuyaweka sawa.
Wewe una shida kichwani mwako ya kuchakata mambo reasonably..

Unawaamini hawa viongozi kuliko hata unavyojiamini wewe mwenyewe ukisahau kuwa hawa ni binadamu wenye tamaa na matamanio yao pia wanayoweza kuyapata kwa njia zozote iwe za haki au haramu..

Laiti kana ukimsikiliza huyu wakili mwanzo hadi mwisho bila shaka ungekuwa na maoni tofauti na hiki ulichokiandika hapa..

Sisi wananchi hatuna shida na kiongozi anayefanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ikiwemo sheria kuu ya nchi yaani KATIBA. Shida iko kwa viongozi dizaini ya Jerry Silaa wanaotumia nafasi na madaraka yao kifisadi ili kujinufaisha wao. Kwa hili Jerry Silaa hakuwa anamtetea mnyonge yeyote bali tamaa zake tu..

Na kwa maelezo haya ya wakili huyu juu ya sakata hili, haina shaka yoyote kuwa Waziri Jerry Silaa ame - mess up big time na ni lazima akemewe na kuchukuliwa hatua stahiki za kisiasa na kisheria ili ajutie matendo yake mabaya na viongozi wengine wajifunze toka kwake...

Inawezekana huna bundle la kutosha kuisikiliza maelezo ya wakili huyu anayemtetea aliyeathiriwa na maamuzi na vitendo vya waziri huyu mwanzo mwisho ili umwelewe..

Kukusaidia ni kuwa wakili huyu, ametoa hoja kadhaa kumtetea mteja wake na zikithibitishwa na nyaraka mbalimbali za serikali hii hii aliyomo Jerry Silaa (waziri wa ardhi);

1. Kwamba, huyu aliyevunjiwa nyumba yake (Johnson Mahuru) ana nyaraka halali za umiliki wa kiwanja na nyumba iliyovunjwa..

2. Kwamba, huyu mama (Naomi) anayetetewa na Waziri Jerry Silaa na anayedai ni mmiliki wa kiwanja hicho alishashindwa kuthibitisha umiliki wake kwa kesi mbalimbali alizofungua mahakamani na hukumu za kesi hizo alizoshindwa ziko on record..

3. Na kwamba, Wakili wa aliyebomolewa nyumba anasema kuwa kiini cha mgogoro huu ambao umesababisha Waziri kujiingiza kichwakichwa na kujichukulia sheria mkononi mwake na kubomoa nyumba ya mtu ni ugomvi binafsi wa ndugu Johnson (mmiliki wa nyumba iliyobomolewa) na kamishina wa ardhi wizarani ndugu Nonge (kama sijakosea)..

SASA HEBU JIULIZE MWENYEWE MASWALI HAYA;

A: Mpaka hapo na kwa kiongozi wa level ya waziri na analiyeapa kulinda katiba na kusimamia haki za watu wote, katika situation ya watu wawili wanaogombania kiwanja kimoja busara ingemwongoza kuchukua hatua gani eti kwa akili yako wewe ndugu Mayor Quimby?

B: Na hivi, ni scenario gani inaweza kupelekea jengo kubomolewa? Bila shaka ni lile lililojengwa kwenye eneo lisiloruhusiwa kisheria na mahakama kuthibitisha hivyo na kutoa amri libomolewe..

Kwenye scenario hii ishu iko tofauti kabisa. Huu ni mgogoro wa watu wawili wakidai wote ni wamiliki wa kiwanja. Sasa huyu waziri kwanini akaenda kubomoa nyumba ya mtu?

Katika mazingira haya akikemewa na kukosolewa iweje useme anakatishwa tamaa? Je, huu si kwamba ni ujinga wa waziri huyu na hivyo amejiingiza mwenyewe kwenye tatizo?

Ndugu Mayor Quimby tunataka viongozi wetu wafanye kazi na kutekeleza majukumu yao vyema lakini iwe kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na zaidi sana katiba ya nchi ili kutoa haki sawa kwa kila raia si kama alivyofanya waziri wako!!!
 
Wanaosema mahakama hazitendi haki ndio hao hao wanaotaka mambo yaende mahakamani kwa kuwa hawapendezwi na alipotoka huyo mchukua maamuzi......
Nataka kukuambia ukweli ingawa naogopa kuonekana mbaguzi.
Wengi wa wanao husika migogoro ya ardhi upande wa wavamiaji ni wafanyabiashara tena wana asili ya kule alipotokea mwenyekiti wa chama kinachotetea.
Kundi lingine ni walikuwa askari au maafisa wa kijeshi, polisi au sekta zingine za umma zenye mapato mazuri.
 
Nimemsikiliza wakili mwanzo mwisho ila nimekuwa na hofu kidogo kwa nini huyu mteja wake Kila kiwanja anachonunua kina migogoro? Na ni lazima mahakama ihusike?
Huyo jamaa ana mtandao mkubwa.
Kinachonipa wasiwasi ni kuwa Jerry Slaa bado hajamnasa kamishna wa ardhi. Anaingilika kirahisi sana, naye ana mtandao wake wa assistant commissioners katika manispaa kadhaa Dar es salaam.
Kuna mtandao wa nshomires mimi nishawahi kupambana nao, tena wana senior lawyers wabunge na madiwani (hasa madiwani dar es salaam).
 
Why complicate matters, kuna watu wanatumia udhaifu wa sheria na kutumia loopholes zake kudhulumu.
Mimi limenipata ndio maana namsupport Waziri Slaa.

Mtu katapeli na ni very clear katapeli, na hati zote ni za kughushi.
Hata akijenga ghorofa 15 . BOMOA TU, si alijua risk za kutapeli?
1. I agree with you, that, zipo scenario hizo za watu wenye nguvu kifedha kutumia udhaifu wa sheria kudhulumu watu wengine wanyonge kifedha. Lakini je, hiyo inampa uhalali gani waziri kufanya alichokifanya? Je, unadhani kila mwenye uwezo kifedha na kujipatia mali, basi amedhulumu tu?

2. Katika scenario ya mgogoro huu, na kwa maelezo ya wakili huyu ni kuwa jengo hilo si kwamba lilijengwa ktk eneo lisiloruhusiwa kisheria bali ni mgogoro wa watu wawili (Johnson & Naomi) kila mmoja akidai ni mmiliki halali wa kiwanja kile. Hivi ktk busara ya kawaida na ktk situation kama hii waziri alipaswa kufanya nini? Ni hiki alichokifanya, kubomoa nyumba ya mtu bila hata amri ya mahakama ingalau? Really?

3. Katika mfululizo wa matukio ya mgogoro huu, mtu mwenye kufikiri vizuri anaweza kutambua mara moja kuwa uko msukumo wa rushwa, ufisadi ukihusisha matumizi mabaya ya madaraka upande wa waziri na anaowapambania. Kamwe huu si utendaji wa kazi za kawaida tu za waziri.

Mathalani;

☑Ni kwanini wamkamate wanayedai ni tapeli na kumweka kwenye selo ya polisi kwa siku 6 bila kumfikisha mahakamani?
☑Ni kwanini yeye waziri abomoe nyumba ya mtu bila kibali cha mahakama? Na yeye amepata wapi mamlaka ya kuwa msikilizaji na mwamuzi wa migogoro ya haki za watu badala ya mahakama?

Kwa maoni yangu, Waziri Jerry Silaa amekosea na kama sheria itazingatiwa na kuheshimiwa, basi imekula kwake hiyo!!!
 
Huko Mapinga, Kerege hakufai sitaki eneo hata bure.
Nimepoteza hekari kadhaa wahusika viongozi wa serikali za mtaa/Kijiji na matapeli walikuwa wafanyakazi wa zamani wa ardhi.
Umesema vizuri sana, sasa hapa waziri wa ardhi ndio alitakiwa kusuka mfumo wa kudhibiti ofisi za ardhi za Halmashauri, sio kudonoa donoa. Aunde Tume ya kuupitia upya mfumo wa ofisi za ardhi na uwajibikaji wake, kisha autungie sheria madhubuti kudhibiti uhuni, sio kupambana na watu walioingizwa chaka na maafisa wake.

Zamani kulikuwa na land rangers wanakaa kila kata kutembelea maeneo kudhibiti ujenzi holela na transaction zisizoeleweka
 
Nataka kukuambia ukweli ingawa naogopa kuonekana mbaguzi.
Wengi wa wanao husika migogoro ya ardhi upande wa wavamiaji ni wafanyabiashara tena wana asili ya kule alipotokea mwenyekiti wa chama kinachotetea.
Kundi lingine ni walikuwa askari au maafisa wa kijeshi, polisi au sekta zingine za umma zenye mapato mazuri.
Asante sana kwa taarifa.....hao watani wanajulikana kabisa kuwa linapokuja suala la ardhi hawanaga masihara kabisa.....
 
Back
Top Bottom