Sakata la Kakoko wa TPA kudaiwa kuweka nyumbani begi lenye USD 1,625,800. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha

Sakata la Kakoko wa TPA kudaiwa kuweka nyumbani begi lenye USD 1,625,800. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha

Aaaah! Bandari ilikuwa yake! Takataka hii kwa kiasi hiki tu cha fedha aingie lupango kwa makofi ya nguvu. Mbona mitaani kibaka wa jogoo tu anaingia lupango huku ameshavunjwa mikono, sembuse hili jangili la nyala za serikali. Jamani, na sisi pia tuna matumbo ya kulisha, mbona mnatufanya waTz wenzenu mafala hivi? Maisha kwetu magumu lakini kwa huyu chizi na familia yake ni tambarale akitumia nyala zetu za serikali. Tupa jela akiwa na mguu mmoja tu hayawani huyu.
Wangekuwa wakosoaji mitandaoni wangeingia lupango kwa kisingizio cha uhujumu uchumi lakini wanaohujumu uchumi hawaguswi.
 
Hii habari ingekuwa imeweka chanzo cha taarifa ingekuwa ya kuaminika.
Ila pamoja na yote chini ya uongozi aa Hayati,kuna kikundi cha watu walinufaika sana.
Ole Sabaya katuhumiwa mara kibao kuwanyanyasa wafanyabiashara ili wampatie pesa. Lakini alikingiwa kifua.
Makonda kaingia studio na wanajeshi wakiwa na silaha alikingiwa kifua mpaka alipojitumbua mwenyewe.
Kwa kuwa palikuwa na double standards za kutosha,hivyo tutegemee kuna ufisadi wa kutisha ulifanyika.
Jiulize pamoja na mazuri yote aliyokuwa anayafanya kwa nini hakutaka CAG awe huru kufanya kazi zake.
Kwa nini hakutaka wakosoaji waingie bungeni.
Kwa nini hakutaka watu wahoji chochote zaidi ya kumsifia yeye tu.
 
Viongozi wote waliopitia bandari ni majizi tokea miaka ile tukiwa wadogo somebody "Janguo" waliishi maisha ya raha kuliko Raisi
 
Hivi mnaijua 9 billion..😅
Ni ela nyingi kwa hohe hahe ila ya kawaida kwa watu kama hao. Kama mtu anaweza kununua nyumba au kiwanja osterbay kwa zaidi ya bilioni moja na nusu we wadhani ana ukwasi kiasi gani?
Hao ni sawa na akina rugemalira aliyempa mama tibaijuka bil 2, akampa yule padri 1.5 bil. Ruge bwana, akiwa bukoba alimwandikia mzee flani cheque ya mils 10 eti ela ya bia 😂
 
Ni ela nyingi kwa hohe hahe ila ya kawaida kwa watu kama hao. Kama mtu anaweza kununua nyumba au kiwanja osterbay kwa zaidi ya bilioni moja na nusu we wadhani ana ukwasi kiasi gani?
Nachoshangaa mtu anapiga hela yote hiyo walikuwa hawajui au Kuna uzembe ama vipi.. mkuu billion sio ukwasi mdogo huo hicho ni kitita Cha maisha..😅
 
Back
Top Bottom