Sakata la Kakoko wa TPA kudaiwa kuweka nyumbani begi lenye USD 1,625,800. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha

Wangekuwa wakosoaji mitandaoni wangeingia lupango kwa kisingizio cha uhujumu uchumi lakini wanaohujumu uchumi hawaguswi.
 
Hii habari ingekuwa imeweka chanzo cha taarifa ingekuwa ya kuaminika.
Ila pamoja na yote chini ya uongozi aa Hayati,kuna kikundi cha watu walinufaika sana.
Ole Sabaya katuhumiwa mara kibao kuwanyanyasa wafanyabiashara ili wampatie pesa. Lakini alikingiwa kifua.
Makonda kaingia studio na wanajeshi wakiwa na silaha alikingiwa kifua mpaka alipojitumbua mwenyewe.
Kwa kuwa palikuwa na double standards za kutosha,hivyo tutegemee kuna ufisadi wa kutisha ulifanyika.
Jiulize pamoja na mazuri yote aliyokuwa anayafanya kwa nini hakutaka CAG awe huru kufanya kazi zake.
Kwa nini hakutaka wakosoaji waingie bungeni.
Kwa nini hakutaka watu wahoji chochote zaidi ya kumsifia yeye tu.
 
Hivi mnaijua 9 billion..πŸ˜…
 
Viongozi wote waliopitia bandari ni majizi tokea miaka ile tukiwa wadogo somebody "Janguo" waliishi maisha ya raha kuliko Raisi
 
Hivi mnaijua 9 billion..πŸ˜…
Ni ela nyingi kwa hohe hahe ila ya kawaida kwa watu kama hao. Kama mtu anaweza kununua nyumba au kiwanja osterbay kwa zaidi ya bilioni moja na nusu we wadhani ana ukwasi kiasi gani?
Hao ni sawa na akina rugemalira aliyempa mama tibaijuka bil 2, akampa yule padri 1.5 bil. Ruge bwana, akiwa bukoba alimwandikia mzee flani cheque ya mils 10 eti ela ya bia πŸ˜‚
 
Ni ela nyingi kwa hohe hahe ila ya kawaida kwa watu kama hao. Kama mtu anaweza kununua nyumba au kiwanja osterbay kwa zaidi ya bilioni moja na nusu we wadhani ana ukwasi kiasi gani?
Nachoshangaa mtu anapiga hela yote hiyo walikuwa hawajui au Kuna uzembe ama vipi.. mkuu billion sio ukwasi mdogo huo hicho ni kitita Cha maisha..πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…