Habari za Kitaifa Habari nyingine zaidi!
Watumishi waonja machungu ya Richmond
Halima Mlacha
HabariLeo; Saturday,January 06, 2007 @00:05
KAMPUNI, Dowans South African Ltd, imeanza kazi rasmi kwa kuwatimua baadhi ya wafanyakazi waliokuwa Richmond. Kampuni hiyo ndiyo iliyouziwa zabuni ya kampuni ya umeme ya Richmond ya kulipa umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, kampuni hiyo ya Afrika Kusini imeanza kwa kuwatumia wafanyakazi wake wapya ambao ni pamoja na Meneja Mradi aliyejulikana kwa jina moja la Nelson.
HabariLeo ilibaini kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Richmond ambao wameachwa na uongozi wa kampuni hiyo hususan walinzi, wako hatarini kupoteza kazi zao hasa baada ya kampuni hiyo mpya kusaini mkataba mpya wa ajira na kampuni moja maarufu ya ulinzi ya Dar es Salaam.
Tayari kampuni ya Dowans imesaini mkataba na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki hii, na kampuni hiyo itaanza kazi muda wowote, kilisema chanzo chetu. Pamoja na hayo, chanzo hicho kilisema kuwa, mmoja wa wafanyakazi hao wapya ambaye awali alidaiwa kuwa Mhasibu na aliyetambulika kwa jina moja la Bharachandra, kwa sasa ndiye anakaimu nafasi ya ukurugenzi katika kampuni hiyo. Gazeti hili lilipomtafuta Bharachandra, liliambiwa kuwa anashughuli nyingi hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo.