Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Lordtical Jnr,

Umesahau kuwa walioipiga kura 80% , 90% yao hawana na wala hawatakuwa na umeme toka Grid ya Taifa!!.

Mi nasema hizi kele za umeme, hazimnyimi SISIEM kulala, Bob Mkandara kawaeleza sana Wapinzani cha kufanya lakini wapi..................

ndio maana naona bora Forums hizi zinafanya kazi nzuri ya kupigia kelele maovu kuliko hivyo vyama vya Upinzani.
 
Nyeti nilizopata kutoka Bongo zinatonya kuwa ile kampuni iliyonunua mkataba wa Richmond, Dowans, shareholders wake ni pamoja na Rostum Aziz na Karamagi. Kama kuna mwenye zaidi mwageni hapa.
 
Jasusi,
Usisahau kisichowezekana duniani kote kinawezekana Tanzania. Haya ndiyo matunda ya kufadhili wagombea na chama; lazima watu warudishe mapesa yao waliyotumia ati. Wakati walalahoi wakiendelea kukwapua kila kinachoonekana kuwa ni chuma chakavu, jamaa huko juu wanaendelea kukwapua kodi inayopatikana kutokana na hizo shughuli za hatari hatari za walalahoi.
 
Jasusi,
Unakumbuka yale ya Richomnd pindi ilipotokea?... watu walianza kutafuta makao yao makuu huko Houston. Ikaonekana kuwa ni kiwanja kitupu na mdosi toka Bongo mchapishaji magazeti kuchukua tender ya Umeme. sasa hivi nimefanya uchunguzi wa hii kampuni ya Dowans Holding nayo napata taabu sana kufahamu lolote kuhusu hawa jamaa!..
Kisha hilo neno Holding kidogo linanipa picha tofauti, kuwa hawa jamaa ni wawekeshaji tu,kibaya zaidi hawa jamaa pia hawana tovuti yao.
Marafiki zangu wakazi wa Dubai na Sharja wamenambia hawafahamu kampuni ya nguvu ya umeme yenye jina hilo!..mmmmhhhh!
Nafikiri next week nao watakuwa na tovuti yao, kamba zilezile za Richmond!...
 
Mkandara

Mimi hapa nilipo tayari nina list nzima ya Kampuni zote zilizosajiliwa UAE. Mpaka December 2006 Ofisi ya Economic Development iliyopo kwenye Economy Ministry (ambao ndio huhusika na usajili wa Kampuni UAE) ina idadi ya kampuni 0317 na katika List hiyo hamna Dowans

Kitu kingine ni kwamba kwenye Madaftari ya BRELA (Business Registration and License Agency) hawana makaratasi ya hii Kampuni. Kisheria Kampuni yo yote ile lazima ipate kibali kabla ya kufanya Kazi Tanzania.

Jambo la mwisho mimi huwa naogopa pia kampuni zinazoanza na Messrs unakumbuka Richmond ilijulikana kama Messr Richmond Development Company na hii ya sasa ni Messrs Dowans Holding Company.
 
Duuuhhh!! hii kali

ahaahah today I almost collapsed after receiving some inside info. here is what is @ stake.

Richmond contract was signed in June 2006 for a period of 2 yrs @ a cost of 172 million USD, which means the contract ends June 2008.

Now all the dams are filled to capacity and Tanesco engineers have concluded they will not buy any power from IPTL< SONGAS< Aggreko for the next 12 months. At most they will buy very little from those 3 companies Jan 2008-june 2008 if rains are bad ( which is highly unlikely).

Now RDC (Dowans) are not needed whatsover. >>><<<<>>>>><<<>>

Which means Wabongo wamepigwa bao la dola 172 million.

I know it sounds kama mazingaombwe but these are facts.

Only in Bongo.

nguvu sina ndugu zanguni!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ila Mheshimiwa amesema alizuia malipo?...hapo mwanzoni.. je hivi sasa wamelipwa?
 
Ninachoona Mimi Jk Pamoja Na Udhaifu Wake Ila El Ni Mafia Wahali Yajuu,matatizo Yote Haya Anapaswa Kujibu Kwa Vile Ulafi Wake Umezidi Kipimo.kwa Kweli El Ni Tajiti Sana,ni Juzi Tu Amefanya Arusi Ya Mwanawe Kubwa Sana ,imagine Kwenye Kamati Za Arusi Ni Akina Ra Ndio Wanaalikwa,kwenye Kutoa Nasaha Unamkuta Makamba Ndio Amepewa Atoe Maono Kwa Watoto Wanaooana,haya Mwamyekiti Wa Kamati Ya Arusi Ni Ole Naiko.tell Me Kuwa Haya Mazagazaga Yo Yataisha Kweli??watu Wameshibana Sana Mpaka Kwenye Shughuli Za Kifamilia.sasa Hapo Bado Unaambiwa Januari Makamba Ndio Yuko Na Jk Beneti.
Nyingine Kali Zaidi Ni Kuwa Mtoto Wa El Msichana Wa Pili Ambaye Anasomea Udaktari Muhimbili Ni Mchumba Wa Mtoto Wa Huyu Bosi Wa Utalii Ambaye Diallo Amemfukuza Bila Mafanikio.inasemekana Familia Hizi Zimeshibana Sana.

Na Huyu Aliyeolewa Juzi Ndio Msichana Wa Kwanza Ambaye Ameolewa Na Mtoto Wa Naibu Waziri Wa Kazi,huyu Baba Mmoja Ambaye Anatokea Hukohuko Arusha.arusi Ilikuwa Sio Kubwa Kama Send Off,el Alifanya Kufuru Kwa Sherehe Hiyo Ya Mwanawe.

Ninachotaka Kuonyesha Hapa Ni Kuwa Kulindana Kupo Kwenye Hii Serikali Ya Jk El Na Itatukosti Sana Huko Baadae.
 
Ila Mheshimiwa amesema alizuia malipo?...hapo mwanzoni.. je hivi sasa wamelipwa?

RDC walipewa conditions na whoever supplied them with the GENERATORS kwamba wafunguliwe (suppliers) irrevocable LC. CRDB Bank Ltd know the rest.
Maelewano ndani ya LC hiyo lazima yatakuwa yanampa ahueni supplier kwamba mzigo ukitua tu nakatiwa changu.

His Excellency uttered those words thinking that woote wanamkubalia na kumwamini anachoongea1 May be he himself can not clarify words like BL, AWB, CIF, C&F, irrevocable LC, non-transferable LC nk. maneno ambayo yamatumika sana katika mikataba ya namna hii. Sidhani kama anajua pia kwamba ndani ya LC mnaweza kukubaliana kulipana 50% down payments?

Bado uwezekano wa RDC kuwa wamelipwa ni mkubwa!
 
It is pity how the country is being plundered!
 
Rais alisema amezuia hayo malipo. Je sasa itakuwaje kwani Tanesco hawahitaji umeme wa Richmonduli, ataendelea kuwalipa? kiasi gani ambacho atalipa hadi huu mkataba umalizike?
 
Kama alizuia malipo ilikuwaje Msanaha akawapa more than 20% ndiyo ukawa mwanzo wa reshuffle kwa jina lake la kiinimacho?
 
Hivi hawa wakina Chadema, NCCR na CUF etc kwa nini wasifanye MAANDAMANO ya pamoja kupinga mambo kama haya.??

Hawa jamaa kweli wapo kwa manufaa ya wananchi??...issue kama hizi za RDC ndio za kuchukulia ujiko maana kila mtanzania anaelewa na kukerwa na ukosefu wa umeme hivyo ni rahisi kupata watu, wanafunzi, vijana, wakinamama na wazee. Lakini wao aahhhh KALAGHABAHO[/B][/QUOTE]

Hivi hao NCCR,Chadema na CUF ni akina nani?Ni Mwenyekiti na Katibu au ni watanzania?Kama jibu litakuwa ni Watanzania basi ni vizuri tukaelewa kuwa hayo maandamano hayatakuwepo.Nguvu za chama chochote zinategemea sana wanachama na si M/kiti na Katibu.Kama wanachama wako weak na chama kitakuwa weak.Hata ukienda kwenye vyama vya wafanyakazi ambako hakuna upinzani utakuta tatizo ni lilelile.Watanzania hatuko tayari ku-fight for what we deserve and what is our rights.Tunasubiri tufanyiwe.Ni vizuri pia tukaelewa kuwa matatizo tunayoletwa na viongozi wetu hayawaathiri M/kiti na Katibu wa upinzani au wanachama wa upinzani pekee bali yatuathiri watanzania wote.Kinachonishangaza sana watanzania tunajua na kuelewa uozo unaofanywa na viongozi wetu,lakini sijui ni kwa ajili ya nidhamu au woga na ujinga au pengine dharau,tunakubali kila tunachofanyiwa hata kama ni kibaya namna gani.Fikiria kuwa we ndo Mbowe au Mbatia au Lipumba.Utafanya nini kwa hili zaidi ya kuwahutubia wanachama wako ambao hawako tayari kuandamana ili kudai kile wanachostahili?Watanzania ili tufanikiwe tuhitaji kufanya mabadiliko makubwa katika tabia zetu.Tusiwe watu wa ndio au hayanihusu.
 
Watanganyika tumelala sana. Tunasemea uvunguni wakipita twapiga makofi na kutoa sifa kemkem .Je mnategemea wao wafanye nini wakati wamesha jua uozo ulipo ?

Lunyungu nakubaliana nawe 100%It we who create these Monsters by allowing them to survive and flourish on cost of our poverty.

Naaza pia kupata wasiwasi kuwa kuna mpango maalum wa kuifilisi Tanesco ili hatimaye wakabidhiane kwa bei Poaaaaaaa!!
 
Habari za Kitaifa Habari nyingine zaidi!

Watumishi waonja machungu ya Richmond
Halima Mlacha
HabariLeo; Saturday,January 06, 2007 @00:05
KAMPUNI, Dowans South African Ltd, imeanza kazi rasmi kwa kuwatimua baadhi ya wafanyakazi waliokuwa Richmond. Kampuni hiyo ndiyo iliyouziwa zabuni ya kampuni ya umeme ya Richmond ya kulipa umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, kampuni hiyo ya Afrika Kusini imeanza kwa kuwatumia wafanyakazi wake wapya ambao ni pamoja na Meneja Mradi aliyejulikana kwa jina moja la Nelson.

HabariLeo ilibaini kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Richmond ambao wameachwa na uongozi wa kampuni hiyo hususan walinzi, wako hatarini kupoteza kazi zao hasa baada ya kampuni hiyo mpya kusaini mkataba mpya wa ajira na kampuni moja maarufu ya ulinzi ya Dar es Salaam.

“Tayari kampuni ya Dowans imesaini mkataba na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki hii, na kampuni hiyo itaanza kazi muda wowote,” kilisema chanzo chetu. Pamoja na hayo, chanzo hicho kilisema kuwa, mmoja wa wafanyakazi hao wapya ambaye awali alidaiwa kuwa Mhasibu na aliyetambulika kwa jina moja la Bharachandra, kwa sasa ndiye anakaimu nafasi ya ukurugenzi katika kampuni hiyo. Gazeti hili lilipomtafuta Bharachandra, liliambiwa kuwa anashughuli nyingi hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo.


Dowans ni South Africans makubwa haya huo ushahidi utapindishwa sana
 
Dua,
Kwanza walituambia hii ni kampuni ya Uarabuni. Lini tena imekuwa ya Afrika kusini? Mazingaombwe! P.S. Kuna uhusiano gani kati ya hii kampuni na Net Solutions? Ni wale wale?
 
Mnakumbuka mambo matatu unayohitaji to pull o the perfect magic act? start counting friends...
 
Jasusi

Hilo swali hata mimi najiuliza maana wote tulikuwa tunatafuta registration ya hiyo kampuni kule uarabuni sasa hawa Habari Leo ndio wamemwaga vitu hivi.

Nafikiri kama watu tukiwa Courageous kumuuliza JK suali la Richmonduli maana unaweza kunyosha mkono na usichaguliwe kuuliza, hivyo itategemea uwingi na ushujaa wa wengi. lakini kwa mtazamo wangu naona wengi ni waoga hata kutuma e-mail tu kujiandikisha wanaona tabu. Naona wengi ndio wanafunzi au wakimbizi hawana solid base; ndio matatizo hayo.

Ngoja tutayaona lakini kwa mtazamo wangu don't expect too much out of this.
 
Back
Top Bottom