Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Muheshimiwa rais ameshikwa na kigugumizi baada ya kuulizwa swali kuhusu kampuni ya Richmond na Dowans aruka swali kiusanii aonyesha zairi kwamba serikali yake inaubia na kampuni hizo jamani wengine mlioko bongo ninatumaini mumeona live tuambieni ilikuwaje? mkutano uliyo chukuwa zaidi ya masaa mawili...
 
Wale wapenzi wa JK naomba mje na majibu tafadhali .Maana si mmeona LIVE ?
 
Siye yetu macho tu!

Maulid Ahamed, Dodoma
HabariLeo; Friday,February 02, 2007 @00:06

WABUNGE wa chama tawala, CCM, jana walikutana kwa faragha mjini hapa, kujadili masuala mbalimbali, huku suala la kampuni iliyokuwa imepewa tenda ya kuzalisha umeme, Richmond iliyouzwa kwa Dowans, likichukua nafasi kubwa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho ambacho Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa, zilibainisha kuwa suala la Richmond lilizungumzwa kwa kina, huku waziri wa sasa wa Nishati na Madini, na aliyemtangulia, wakitakiwa kutoa maelezo kuhusu kilichosababisha kampuni hiyo kukwama kuzalisha umeme, kwa mujibu wa mkataba.

Mawaziri hao ni Dk. Ibrahim Msabaha aliyekuwa waziri wa wizara hiyo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika mabadiliko ya Oktoba mwaka jana, na aliyemrithi, Nazir Karamagi.

Hata hivyo, mtoa habari ndani ya kikao hicho alieleza kuwa suala hilo lilionekana kuwakera wabunge wengi wa CCM, na baadhi yao wakaonyesha wasiwasi wao kuhusu kwa nini Dk. Msabaha atoe maelezo wakati amekwisha kuondoka katika wizara hiyo inayosimamia nishati nchini.

“Wabunge wengi waliuliza kwa nini Msabaha ajieleze wakati amekwisha kuondoka wizara ile. Wanahoji kuwa kwa utaratibu wa Serikali, Waziri anapoondoka, anayemrithi ndiye anayewajibika kwa suala husika kwa wakati uliopo.

“Wanahoji kuwa kama Msabaha hakupaswa kulizungumzia suala hilo na badala yake, Karamagi pekee ndiye mwenye jukumu la kulielezea. Je, leo Rais mstaafu Benjamin Mkapa, aitwe kujieleza kwa mambo yaliyofanyika wakati wake?” alieleza mmoja wa wabunge wa CCM aliyeshiriki kikao hicho.

Inaelezwa kuwa Dk. Msabaha alipewa fursa ya kueleza hali ilivyokuwa hadi kampuni hiyo ikashinda tenda ya kuzalisha umeme huo, lakini ikakumbwa na matatizo na kusababisha minong’ono mingi kuwa kampuni hiyo inahusika na baadhi ya vigogo katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Hata hivyo, licha ya wabunge hao wa CCM kuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli kuhusu kampuni hiyo ambayo ilipaswa kuzalisha megawati 100, lakini ikazalisha megawati 20 tu, dukuduku lao litabidi lisubiri kwa muda ili kujua ukweli.

Imeelezwa kuwa sasa suala hilo linasubiri ripoti ya Kamati ya Uwekezaji na Biashara ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), ambayo iliamua kulivalia njuga kutaka kujua ukweli. Hata hivyo, haijajulikana ni lini wabunge hao watakutana tena kuzungumzia ripoti hiyo, ingawa inaelezwa kuwa itakuwa kabla ya kumalizika kwa kikao cha sasa cha Bunge, Februari 16, mwaka huu.

“Tumeelezwa kuwa suala hili tusubiri ripoti ya Kamati ya Uwekezaji na Biashara, na baada ya hapo, tutakutana tena kabla ya kumalizika kwa kikao hiki cha Bunge. Inaweza kupangiwa siku za Jumamosi au Jumapili, au muda mwafaka ukipatikana,” alisema mmoja wa wabunge hao wa CCM aliyehudhuria kikao cha jana mchana. Alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mradi huo jana jioni, Waziri Karamagi alisema tatizo lililoikumba kampuni hiyo ni mvua, hali iliyofanya ishindwe kuweka mitambo hiyo.

Kutokana na sababu hiyo, Kampuni hiyo haitapewa adhabu ya kulipa fidia.
 
wazee leo bunge linakaa kama kamati kikao cha siri kujadili hii kashfa ya richmond...wameamua hivyo i think wanayojadili are not for public consumption
 
wazee leo bunge linakaa kama kamati kikao cha siri kujadili hii kashfa ya richmond...wameamua hivyo i think wanayojadili are not for public consumption

Hao wanawekana sawa namna ya kupinga hoja yoyote itakayokuja bungeni kuhusu hii mada. Hamna lolote hapo linaloendelea zaidi ya kupanga mikakati ya kulindani ndani ya bunge.
 
Hao wanawekana sawa namna ya kupinga hoja yoyote itakayokuja bungeni kuhusu hii mada. Hamna lolote hapo linaloendelea zaidi ya kupanga mikakati ya kulindani ndani ya bunge.

yebo*2 ,ukisikia kuzika demokrasia ndio huku ,hakuna kitu mbaya kama kuminya uhuru wa wabunge kujadili kwa kutumia kivuli cha bunge kukaa kaMA Kamati ya chama,..bora lile bunge la chama kimoja lilikuwa na msisimko..kina tuntemeke sanga,njelu kasaka,semindu pawa ets walikuwa wanarusha mawe si leo watu wanangoja per diem tu....
 
Ama kweli TZ .Yaan kamati ya siri kwenye hili ?
Kazi kubwa tunayo kwa kweli.
 
Wana chemsha!!! kweli kweli!!!....Sasa na rada je?
 
Wengine wanataka tume, wengine wanataka mjadala wa wazi sasa hivi. Nani atashinda?

Jinamizi la Richmond Dodoma

na Irene Mark, Tanzania Daima, Feb 8, 2007

KAMATI ya Uwekezaji na Biashara ya Bunge, imemwandikia Spika wa Bunge ikimtaka aunde tume ya kuichunguza Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya Richmond Development (RDC).

Hatua hiyo ambayo tayari imeonekana kuzusha minong’ono miongoni mwa wabunge, inachukuliwa wakati kukiwa na shinikizo la chini kwa chini la kutaka kampuni hiyo ijadiliwe katika kikao cha sasa cha Bunge.

Wabunge wanaotaka kujadiliwa kwa kampuni hiyo ambayo tayari imeshauuza mkataba wa kuzalisha umeme wa megawati 100 kwa Kampuni nyingine ya Dowans Holdings, wanaliona pendekezo la kuundwa kwa tume kuwa ni mbinu ya kutaka kuifanya hoja hiyo kutojadiliwa hivi sasa, kinyume cha matakwa yao.

Taarifa ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza kwamba, barua hiyo kwa Spika inataka kuona tume hiyo ikiundwa kabla ya kikao cha Bunge kumalizika kesho Ijumaa.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, kuundwa kwa tume hiyo kutamaliza msuguano kati ya wabunge na wajumbe wa kamati hiyo kuhusu uhalali wa Richmond kupewa kazi wasiyoiweza.

“Barua tuliyoipeleka (jana) juzi kwa Spika inamtaka kuunda tume itakayohusisha wabunge katika kupata ukweli kuhusu Richmond, kwa kuwa, hii inaonekana wazi ni ‘dili’ linalotiliwa mkono na wakubwa na sisi hatukubali hadi tujue mwanzo na mwisho wa hiyo Richmond.

“Sasa wabunge wenye misimamo wanataka kujua ukweli halisi kuhusu Richmond...haiwezekani iingie mkataba halafu muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mkataba, ikauza kazi kwa wengine.

“Sisi kama wawakilishi wa wananchi tunataka kuwaeleza wananchi kilichotokea, ili wajue kulikuwa na ubabaishaji katika mkataba wa Kampuni ya Richmond...pesa nyingi za walipa kodi amepewa huyo Richmond halafu kashindwa kazi,” kilisema chanzo kingine cha habari.

Taarifa zinaeleza kwamba, kabla ya barua hiyo, mmoja wa wabunge wanaounda kamati hiyo, alitaka kupeleka hoja binafsi ya kutaka kuchunguzwa kwa kampuni hiyo kwenye kikao cha Bunge kutokana na mkanganyiko uliojitokeza kuhusu suala hilo kati ya wabunge hao.

Siku chache kabla ya kuanza kwa kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini hapa, kamati hiyo ilitembelea eneo la mradi wa Shirika la Umeme (TANESCO) na kushuhudia matengenezo ya mahali panapotarajiwa kuwekwa mashine za Kampuni ya Dowans.

Baada ya ziara hiyo, wabunge hao walieleza kutoridhika kwao na mkataba wa kati ya Serikali na Richmond uliogharimu dola milioni 172, na mabadilishano kati ya Richmond na Dowans Holdings, ambayo hati hiyo haikuonyesha dalili za kuweza kutimiza masharti ya mkataba kwa wakati.

Kampuni ya Richmond inadaiwa kumilikiwa na kijana wa Kitanzania mwenye maskani yake Houston, Marekani.
 
Nadhani haya yote yanafanyika kwa manufaa ya wachache tuu.

Kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya Nne, wengi wetu tuliamini kwamba mambo yangeweza kubadilika na kuwa mazuri kwa kiasi fulani (to improve) kutoka hali tuliyokuwa nayo. Lakini mambo hayakuwa hivyo. Mtanzania wa kawaida ameendelea kunyanyasika na kutaabika kuliko hata ilivyokuwa awali. Hii ni hatari sana!

Maji na umeme (vitu ambavyo ninaamini ni muhimu na vya lazima kwa maisha ya sasa) vimeendelea kutokupatikana ama kupatikana baada ya kujiminya na kujituma sana.

Mwanzoni wa utawala wa awamu hii ya Nne, tulikumbwa na tatizo kubwa tuu la umeme. Likazaa matatizo mengine mengi pamoja nalo. Lakini wakubwa zetu, akiwemo mtaalamu wa mambo ya uchumi, mkubwa wa Benki ya Tanzania (Bw. Daudi Balali) walidiriki kusema hayo ni mambo ya mpito tuu na hayana madhara kwa uchumi wetu! (Hili linafaa kujadiliwa! Yaani umeme unapatikana kwa saa nane tu tena za usiku kwa karibu miezi nane ( na kusiwe na madhara yoyote kiuchumi? hasa uzalishaji!)

Mnakumbuka kusainiwa kwa mkataba wa miaka 20 (20 years Power Purchase Agreement) kati ya Tanesco na IPTL? "deal" iliyoliingiza taifa kwenye matatizo makubwa sana ya kiufundi na zaidi sana kiuchumu!

Katika kufikiri kwamba nikutatua tatizo la umeme, mikataba mingine "feki" (worthing multi-million $) ikasainiwa tena kwa niaba yetu kati ya serikali na kampuni feki (Richmond). Mziki ukawa mkubwa ukapelekea ku-reallocate na kubadilisha kampuni Richmond - to - Dowans, ambayo nayo hadi leo haijaweza ku-deliver, japo muda waliopewa umeshapita sana! Haya yanaonekana na hakuna anayewajibishwa! Na tungoje tuone, japo tunaumia, lakini hatuna jinsi.

Tanesco wakaomba kupandisha "bills" za umeme wao (ambao siyo reliable) na wakakubaliwa.
DAWASCO nao wameomba, soon will be implemented; Songas nao wanataka kupandisha gharama za gesi yao,EWURA wanawafikiria nao; na sisi Watanzania tunawasikilizia. Kwenye madaladala kila kukicha kuna kesi nyingi tuu za makondakta kugombana na wateja wao kwasababu ya kujiamualia nauli wazipendazo wao. He! Hii waerevu huiita "punda afe, mzigo wa Bwana ufike" kwani machungu yote haya yanaishia mabegani kwa Mtanzania wa kawaida tuu, pasi na wawakilishi wetu kusema chochote.

Simnakumbuka ambavyo Waheshimiwa Wabunge wetu walivyotumia muda na pesa nyingi sana (100 M TZS) eti kujadili jinsi mtu anavyotumia vyombo vyake vya habari? (Sakata la Bw. Mengi na Mh. Malima) .....Tutaliongelea
I
nasikitisha sana.

Watanzania tuamke sasa, tumelala sana, tunaonewa sana.
-------------------
 
Sitta: Tutaijadili Richmond

na Irene Mark

HATIMAYE sakata la Kampuni ya Richmond Development, iliyoshindwa kutekeleza mkataba wa dola za Marekani milioni 172 wa kuzalisha umeme wa megawati 100, litajadiliwa katika kikao kijacho cha Bunge.

Spika wa Bunge, Samuel Sitta, jana aliithibitishia Tanzania Daima kwamba suala hilo la Richmond lililozua maneno mengi na wasiwasi miongoni mwa wananchi litajadiliwa katika Kikao cha Saba cha Bunge kitakachoanza Aprili.

Mbali ya hilo, na bila ya kuingia katika undani, Sitta alisema kikao hicho cha Bunge kitajadili pia miradi mingine kadhaa ya serikali ambayo imezua utata.
Sitta alisema, anachosubiri ni barua kutoka kwenye Kamati ya Uwekezaji na Biashara ya kumuomba suala hilo lijadiliwe ndani ya Bunge, ili aanzishe mchakato wa kuwezesha mjadala huo kati ya wabunge na serikali.

“Wanachotakiwa ni kukamilisha taarifa yao baada ya kuelewana. Hadi tunaondoka bungeni hawakuwa tayari…walitakiwa kukubaliana juu ya mapendekezo waliyoamua kwenye taarifa yao ndipo waiwasilishe bungeni.

“Suala hapa si Richmond peke yake, yapo mambo mengi ambayo kama Kamati ya Uwekezaji na Biashara inatakiwa kuyajadili…wamedai iwepo sera ya Nishati ya Taifa kwa miaka 10. Sitta alisema kamati hiyo ina mambo mengi ya msingi inayotakiwa kuyatolea mapendekezo bungeni ili yapate muda wa kujadiliwa kwa kina.

Alisema baada ya mjadala huo, iwapo serikali itashindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu suala hilo la Richmond, basi Bunge litalazimika kuunda kamati maalumu kulifuatilia. Alisema kilichotokea wakati wa kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni, ni mgongano kati ya wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kuhusu suala la Richmond, jambo lililowafanya washindwe kufikia uamuzi wa pamoja.

Alisema wabunge hao hawakuelewana na walikuwa na taarifa ndefu kuhusu suala hilo. “Wao walikuwa na rasimu, Bunge linapokea taarifa iliyokamilika na yenye mapendekezo ndani. Na lazima serikali ipewe muda na nafasi ya kufanya mambo yake. Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri inaeleza kuwa, kazi ya Bunge ni kusimamia kamati, lakini uundwaji wa kamati hizo unatokana na majibu yasiyotosheleza ya serikali kuhusu jambo lolote linalojadiliwa bungeni,” alisema Spika Sitta.

Hata hivyo, ingawa kauli hii ya Sitta imefungua ukurasa mpya kwa wabunge kuweza kuhoji na kupata ukweli kuhusiana na kampuni hiyo, kwa upande mwingine imezaa utata, kwa vile inapingana na kauli ya mwanzo ya wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara. Awali wajumbe wa kamati hiyo walidai kumpelekea barua Spika Sitta, iliyokuwa ikimtaka kuunda kamati maalumu ya kuchunguza mkataba wa Richmond uliogharimu mamilioni ya fedha za serikali.

Wajumbe wa kamati hiyo walilidokeza gazeti hili kuwa, barua waliyomwandikia Spika ilikuwa inataka kuona tume hiyo ikiundwa kabla ya kikao cha Bunge kumalizika, hatua ambayo haikutekelezwa. Walidai kuwa, walimkabidhi Spika barua hiyo Februari 6, wakiwa wameeleza nia yao ya kutaka kuundwa kwa kamati hiyo haraka, ili ichunguze na kupata ukweli kuhusu zabuni iliyopewa kampuni hiyo.

Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili walimlaumu Spika kwa kuchelewa kuundwa kamati hiyo, kwa kile kilichoonekana kuwa ni kubaini kwake kuwa inaweza kubaini mambo ambayo yatawatia baadhi ya wakubwa katika matatizo. Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, aliyezungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, alithibitisha kwa mara nyingine kwamba, walikwisha kumkabidhi barua Spika.

Mbunge huyo alisema hawezi kuzungumza mengi lakini akaahidi kutoa maelezo kuhusiana na suala hilo mara tu atakaporejea jijini.

Uchunguzi zaidi za Tanzania Daima umebaini kuwa, kumeibuka mvutano miongoni mwa wabunge kuhusu Richmond, huku kukiwa na madai ya kukingiana kifua kutokana na kile kinachoonekana kuwa mchezo mchafu uliofanywa na baadhi ya viongozi serikalini wakati wa kuipa mkataba kampuni hiyo, ambayo baadaye iliuuza mkataba kwa Kampuni ya Dowans.
 
mtaijadili lini >?? au ndio mnadhani wadanganyika watasahau ili mpete ! halafu huyu sitta mie nashindwa kumuelewa, kwanza yeye anatakiwa kujua HANA chama chochote cha siasa, sio ccm wala cuf, lakini yeye ana-base sana ccm kw ahao jamaa zake waliomuweka ! anatia kinyaa huyu mzee..
 
Heshima yako mzee Kada,

Nafikiri niiangalie posting yako kwa issue mbili,

(a). Spika Sitta na suala zima la kuijadili hiii deal ya Richmond, kwa nchi yoyote iliyostaarabika na yenye Rule of Law and Order, hiii ilitakiwa kuwa big news! Lakini the record au history ya bunge letu it is not so, Sitta aliahidi kujadili vyeti vya viongozi na mpaka leo hatujasikia kitu, kwa hiyo why should we trust him this time arround? Bunge letu halijawahi kuwa ni kwa ajili ya kuwakilisha wananchi, bali ni kuwakilisha agenda za serikali, na hiii ni toka tupate uhuru,

hapa ndipo ninaposema kwamba pamoja na mazuri yote Mwalimu aliyotuletea, bado tuna matatizo makubwa sana na yale ambayo hakutuletea, na hili ni mojawapo, la kuwa na bunge ambalo ni rubber stamp ya serikali. Hakuna cha kutegemea kutoka kikao hicho cha bunge, maana mawaziri au viongozi waliohusika wameshahamishiwa sehemu nyingine na rais wa Jamhuri, meaning kwamba rais ameridhika kuwa makosa yao haya-amount to the level ya kuwa dismissed au kushitakiwa mbele ya sheria kama hayo makosa yapo kweli, sasa leo bunge au kamati zake zitafanya nini tofauti?

Hapa pia napenda kuwalaumu wabunge wa upinzani, kwa kutokuwa aggressive enough na kutumia "any means necessary", kutafuta ukweli behind the whole issue, matokeo yake kuwaacha wananchi wakiyumba hewani! I mean kamati ya bunge itafanya nini? Hivi karibuni kuna viongozi wakubwa wawili wa serikali waliokuwa wakihangaika hapa JF kutafuta ukweli wa hiyo deal, na wakaniomba niwaforwardie data zote zilizotolewa hapa, kwamba huenda wakaweza kuunganisha darts kwa kutumia data za hii forum, now we are talking about bunge la wananchi wa bongo, kama hao viongozi wajuu hawajui je sisi wananchi itakuwaje?

Kwa hiyo you might have a point kwenye hili, isipokuwa una-raise a good question, unaposema wanataka tusahau! maana tutasahau nini wakati mpaka sasa tuna-deal na hadithi tu? Ukweli so far haujulikani ni upi na nani ni nani?

(b). Unakuwa unfair, unapomlaumu Spika wa bunge la nchi anapokuwa ana-side na chama chake cha siasa, kwa sababu ni lazima afanye hivyo na hiyo ni tabia ya siasa za dunia nzima, si kweli kwamba spika wa bunge la Kenya ata-side na wabunge wa KANU yaani upinzani, au Mama Pelosi ata-side na wabunge wa Republican, haijawahi kutokea na haitakuja kutokea! Simply because, Spika huchaguliwa na chama chake kusimamia utekelezaji wa agenda na sera za chama kile kama kile chama kilivyowaahidi wananchi wakati wa uchaguzi,

Majuzi Democrats wameshinda uchaguzi wa bunge la US, kwa kuwaaahidi wananchi kumaliza vita vya Iraq, sasa leo Spika atafanya nini wabunge wa Democrats wakidai kumaliza vita? Republicans watasema kwamba Spika ni unfair? Hapana! Spika ni lazima afuate maagizo ya chama chake, na ndio maana CCM ikaamua Spika wa bunge ambaye ni mwanachama wao lazima awe mjumbe wa kamati kuuu ya CCM,

Kwa hiyo kwenye hili humtendei haki Mzee Sitta!
 
Good points Mzee!

Patamu zaidi ni hapa:-
Bunge letu halijawahi kuwa ni kwa ajili ya kuwakilisha wananchi, bali ni kuwakilisha agenda za serikali, na hiii ni toka tupate uhuru
 
Heshima yako mzee Kada,

Nafikiri niiangalie posting yako kwa issue mbili,




Hapa pia napenda kuwalaumu wabunge wa upinzani, kwa kutokuwa aggressive enough na kutumia "any means necessary", HAWA WABUNGE WAKIWA AGGRESIVE WANAAMBIWA HAWANA NIDHAMU MFANO. KABWE NA WENGINE, UNAONA SASA MPAKA NDESAMBURO MZEE WA WATU WAMEMHARIBU KISIASA ! NDIO MAANA WANAAMUA KUKAA KIMYA

Kwa hiyo you might have a point kwenye hili, isipokuwa una-raise a good question, unaposema wanataka tusahau! maana tutasahau nini wakati mpaka sasa tuna-deal na hadithi tu? Ukweli so far haujulikani ni upi na nani ni nani?

(b). Unakuwa unfair, unapomlaumu Spika wa bunge la nchi anapokuwa ana-side na chama chake cha siasa, MZEE SITTA ANA KILA SABABU YA KULAUMIWA !

Majuzi Democrats wameshinda uchaguzi wa bunge la US, kwa kuwaaahidi wananchi kumaliza vita vya Iraq, sasa leo Spika atafanya nini wabunge wa Democrats wakidai kumaliza vita? Republicans watasema kwamba Spika ni unfair? Hapana! Spika ni lazima afuate maagizo ya chama chake, na ndio maana CCM ikaamua Spika wa bunge ambaye ni mwanachama wao lazima awe mjumbe wa kamati kuuu ya CCM,

Kwa hiyo kwenye hili humtendei haki Mzee Sitta!

HUO MFANO WA DEMOCRATS MAREKANI NA CCM TZ NADHANI NI VITU VIWILI TOFAUTI, KWANZA STRUCTURE ZA UONGOZI KATI YA HIZI NCHI 2 NI TOFAUTI SANA TENA SANA! NA SIDHANI KAMA TUTASEMA SPEAKER WA HOUSE ( NANCY PELOSI ) ANAKOSEA KUSTOPISHA REPUBLICANS NA IDEA YAO YA KUWA IRAQ KWA MAANA KWAMBA DEMOCRATS HATA KABLA HAWAJACHAGULIWA WALIKUWA WAMESHA-LAY OUT PLAN YAO NA KUSEMA KWAMBA LAZIMA WAPULL PUT OF IRAQ, NA NDIO EXACTLY WANACHOFANYA HIVYO HAWANA SABABU YA KULAUMIWA. TURUDI KWA SITTA, HUYU MZEE AMEWEKEZWA TU PALE KUANGALIA MAKOSA YA KILA LOWASSA KUNYAMAZISHA BUNGE NA YEYE ( SITTA ) AWE ANAITIKIA TU UTADHANI LOWASSA NDIO SPIKA WA BUNGE WHICH IS NOT RIGHT.
 
Pia soma katika hiyo quote hapo pia nimetoa maandiko yangu !! katika hiyo post ya juu !!
 
haya wale viongozi shupavu ndan ya CCM nadhani wengine ni wabunge na wengine ni wana Siasa pekee wako wapi ?Maana kama Upinzani hawawezi basi kuna chaguzi zinakuja mbeleni je CCM hawaoni hatari ama wanajua wana Polisi , Usalama wa Taifa na Jeshi wataiba na kulazimisha kura na kuendelea kutunyonya hawa makupe wakubwa ?
 
Nitakupa pass, kwenye kutolinganisha mabunge mawili, ingawa binafsi ninaamini kuwa the point ni functions za Spika wa bunge bila kujali nchi ni wapi na system yake politically ikoje, lakini for the sake of argument nitakupa pass,

Lakini kwenye mitsari yako ya mwisho, ni kwamba Waziri Mkuuu ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serkali bungeni, na pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama chake, kama alivyo Spika Sitta, wote wawili wanaingia kwenye kamati hiyo ya chama chao ambayo ni Supreme, only kutokana na kazi zao na sio kuchaguliwa kama wajumbe wengine, kwa hiyo wao kwenye kamati hiyo hawana sauti kabisaa ni watu wa kusikiliza na kuambiwa cha kufanya,

sasa kuwaalumu wanapokwenda bungeni kutekeleza waliyotumwa na chama chao ambacho ni chama tawala kilichochaguliwa na wananchi waliozikubali sera zao, na wakati sheria ya Jamhuri inwaweka viongzi hao wawili yaani PM na Spika kwa ajili ya kukisaidia chama tawala kutekeleza ahadi zake kwa wananchi ambao ndio taifa lenyewe sidhani kama unakuwa fair kwa wananchi na taifa kwa ujumla!
 
Kwa maana nyingine kama wananchi waliichagua CCM kutokana na sura za wagombeahilo lenu .
CCM wanajua kwamba ni sera zao zilizowavuta wananchi ikiwa ni pamoja na kuuza nchi!

Mjinga nani?
 
Mjinga na wajinga ni wananchi walio leta mambo ya sura mbele na ushabiki wa kijinga .
 
Back
Top Bottom