Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Salaam,
Nimeona mijadala mingi humu ikizungumzia sakata la kocha wetu ambaye amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini kuhusu sababu za yeye kuondoka kambini.
Kwa upande wa klabu bado hatujasema chochote, taarifa yetu ya awali tulitoa kuhusiana na yeye kuondoka kambini kwa sababu zake binafsi. Ni kweli aliondoka bila kueleza sababu kwahiyo kwetu bado tunaziona ni sababu binafsi.
Maswali machache yakinifu ya kujiuliza;
1. Je, kwanini ndani ya muda mfupi baada ya kuondoka kambini akakimbilia kujieleza kwenye vyombo vya habari? Lengo ni nini?
2. Je, ana uthibitisho wowote wa tuhuma alizozitoa? Ni kipi kinathibitisha kuwa aliyoyasema yote ni ya ukweli?
3. Amekiri hakupangiwa kikosi kabla na wakati wa mechi, kwanini alalamike kupangiwa kikosi? Kipi?
4. Madai ya kupangiwa kikosi yanachekesha: Amecheza mechi moja tu na kikosi si alipanga mwenyewe, aliingiliwa wapi?
5. Kama ni kweli aliitwa kikaoni na waajiri wake kuhojiwa, kwanini asitoe majibu ya kiufundi yeye akiwa kama mtaalamu?
6. Anasema ameutaarifu uongozi kuwa ameacha kazi, kwanini anakuwa mgumu kuandika barua rasmi kama anaamini ana sababu za msingi?
Kimsingi Sisi bado tunasubiri barua yake ya kuacha kazi au kujieleza kwanini hayupo kambini. Mambo ya utoro kazini hatutaki. Kama amepata kazi sehemu nyingine aseme, sio kwenda kutuchafua kwenye vyombo vya habari kutafuta visingizio. Kwa sasa tumechagua kakaa kimya, tuna mechi ngumu na Future FC Oktoba Mosi kule Misri. Autumie muda huu vizuri kujitafakari na kufanya maamuzi kwa kufuata utaratibu rasmi.
Pakiwa na jambo lolote klabu itatoa taarifa rasmi!