Sakata la Kocha: Singida tumechagua kukaa kimya, tuna kazi kubwa mbele yetu

Ndugu, kama una ujasiri basi ujitahidi tu kuwashauri viongozi wako kuacha uswahili na ubabaishaji kwa watu wenye ngozi nyeupe.

Mambo ya uswahili na ubabaishaji, wafanyieni waswahili wenzenu. Wenzetu wazungu wanataka mambo yanyooke! Na siyo kupinda pinda kama mnavyotaka nyinyi.

Kirahisi tu, kocha na akili zake timamu aondoke kambini na kwenda kuwachafua kwenye vyombo vya habari nchini kwake!!!
 

Yaani Meidndrop kumtaja mwigulu ni kutafuta attention?[emoji38] yupo nchini ndani ya week 2 ameanza vipi kujua mwigulu anahusishwa na umiliki wa singida fountain gate mpaka amtaje , ukweli siku zote unabaki kuwa ukweli .

“The truth is incontrovertible.Malice may attack it, ignorance may deride it, but in the end ,there it is “ alisema waziri mmoja makini nenda kamwambie waziri wako wa kuunga unga hili jambo aelewe tu ukweli unabaki kuwa ukweli.
 
Ulitaka asiseme ukweli?
 
Mbona Simba baada ya kutoridhishwa Phiri kuweka benchi mashabiki walivunja ukimya na sasa anapewa nafasi?

Hawa wazungu msiwababaikie sana kwa kudhani kila kitu wapo sahihi.
 
Kwahio mmiliki ni Mwigulu? Naona mengine umejibu kasoro hili, au hili ndio la "kuikalia kimya?"
 
Tuache mambo yote. Je kwenye hicho kikao, Waziri alikuwepo na alikuwepo kama nani? Mbunge
 
Mbona Simba baada ya kutoridhishwa Phiri kuweka benchi mashabiki walivunja ukimya na sasa anapewa nafasi?

Hawa wazungu msiwababaikie sana kwa kudhani kila kitu wapo sahihi.

Hili sina uhakika nalo na silijuii vizuriii ila nikuulize match ya jana huyo phiri alianza ? Na ile match ya zambia alianza kama first 11? Na hata kama ameanza kipi alichofanya cha maana zaidi ya watu kukariri jina ukweli utabaki kuwa as long as coach ndo amepewa majukumu aachwe afanye mbinu anazojua yeye.

Mashabiki wanajua nini hasa mashabiki wa mpira wa bongo! Wapiga kelele tu hao. Pia hakuna sehemu kocha wa simba amelalamika kuingiliwa majukumu yake ya ukocha so it’s either way kama ameamua kuingiliwa majukumu yake ya ukocha akakubali kupanga kikosi kama wanavyomwambia viongozi or hajawahi kabisa kuingiliwa majukumu ya ukocha na kikosi anachopanga ndicho anachotaka .

So mfano wako kidogo ni hauendani na hichi kinachojadiliwa humu. Sio mfuatilaji wa mpira wa bongo ila nimeangalia saivi siku za karibuni huyo phiri still hayupo first eleven so mfano wako ni batili.

Hatupapatiki na wazungu ila tunachofurahi ni kuona jamaa kasimamia taaluma yake kuliko kukubali kupangiwa kikosi na mtu ambaye hana hata taaluma ya ukocha .
 

Wewe umeandika kwa mihemko na hujui hata unachokitetea.

1. Hatujawahi kusema popote kuwa ameenda kutatua matatizo ya kifamilia. Hii umeitoa wapi?
2. Unauita ukweli kwa ushahidi upi? Au kitu akisema mzungu kwako ndio ukweli? Hasara.
3. Bado unaandika kikasuku kwa kurudia maneno ya tuhuma yasiyo na ushahidi.
4. Same as above. Tuseme ni ukweli aliulizwa hivyo, jibu lake ni lipi? Yaani wewe dereva unaendesha gari kuelekea sehemu kwa kupitia njia ngeni, ukiulizwa mbona unapita huku unashuka ndani ya gari na kuacha funguo badala ya kusema tunapita huku kwa sababu hii na hii?
5. Hakuna hoja hapa. Iwe ameitwa au hajaitwa hakuna mashiko kwenye tuhuma.
6. Hapa umeonesha udhaifu wa uelewa. Yaani mtu aache kazi kwa maneno matupu? Unazijua sheria za mikataba ya hawa watu wa football? Hawezi kuandika kwa sababu anajua atatakiwa kulipa fidia. Ukitetea uwe na uelewa wa mambo.
7. Hili sitakulazimisha kama una jibu lako tayari. Amini unachoamini.

Yaani mtu apewe timu, apate ushindi kwenye mechi ngumu na muhimu, halafu aje apangiwe kikosi? THINK.
 
Tatizo hasa nini kilichomuondoa kocha ,hatua zipi mtachukua asiporudi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…