Sakata la Kocha: Singida tumechagua kukaa kimya, tuna kazi kubwa mbele yetu

Wewe ndo unajua unachokitetea sio? Wewe ni muongo na hatuwezi kusikiliza pande moja lazima tujue pande ipi ni kweli na pande ipi inasema uongo baada ya kufanya ivyo tumejua wewe ni muongo na hatukulaumu tunajua wewe ni maemaji na lazima useme wanayotaka kina mwigulu na wengine wakubwa wako.

1.” Tumeshtushwa na habari zinazoendelea mitandaoni kuwa tuna matatizo na kocha si kweli hatuna matatizo na kocha ni kweli ernest hayupo amepata dharura ameondoka kwa dharura akashughulikie changamoto zake binafsi ….” haya ni baadhi ya maneno ya msemaji wa timu ambaye ni wewe ;

1: kwanza kabisa umeanza kwa uongo kuwa hakuna matatizo na kocha wakati ukweli kuna tatizo kati ya kocha na timu , hili linatosha kusema wewe ni muongo na umedanganya umma au na hili pia unabisha.

2. Ukweli unajulikana baada ya kusikiliza pande zote mbili kati ya wewe na kocha tumejua yupi muongo na yupi mkweli. Swala la mzungu linatoka wapi si mmemleta wenyewe[emoji38] sema kawazidi akili alijua huyo ni kiwelu au mgunda.

3Ushahidi upi unaotaka wewe ? Kocha kitokuwepo tayariiii inaonyesha kuna tatizo na mgogoro kati ya kocha na wamiliki wa timu kina mwigulu, tumesikiliza upande wa kocha tayari haya upande wenu mnasemaje au ndo mnakaa kimya kwamba hamna tatizo lolote[emoji23]

4. Sio tuseme ni ukweli aliitwa , ukweli ni aliitwa au unataka kusema yote aliyosema kajitungia, unaleta mfano wa madereva humu kocha katoa sabau kwanini ameamua kufanya vile kutokana na mazoezi aliona wachezaji wanaofit ni hawa na hata huyo gadiel nafasi aliyocheza ndo alikuwa best na hio ndiyo mbinu aliyotumia as coach.

5. Unapoleta kitu humu usidhani wote wana uelewa finyu mkuu sema hatuwezi kukulaumu maana hata hicho kikao hukushiriki wewe ni msemaji tu wa timu unapewa maneno then unayasema hivyo hivyo kulinda kibarua chako.

NB: tumemsikiliza kocha upande wake kasema ameondoka kutokana na kutaka kupangiwa wachezaji sasa na nyinyi kwa upande wenu tuambieni kwanini kocha kaondoka sababu kubwa ni ipi?
 
Dogo anaona umetumwa kuzoa uchafu waliotema wakubwa.

Kuwa msemaji kwa mpira wa bongo daima utakuwa chawa upende usipende...pole
 
Nimependa tu hapo ulipoandika kwa Kukiri kuwa ni Kweli aliondoka Kwao bila Kuelezea sababu yoyote kwani kama umekamilika katika kufanya Critical ( Logical ) Thinking utakuwa umeshapata Jibu, hivyo ngoja na Sisi Wengine ( Watu wa Kawaida mno Maishani ) tuwaige Singida Fountain Gate FC Kunyamaza.
 
Ngoja na Sisi Wengine tuchague Kunyamaza kama wenye Singida Fountain Gate FC walivyochagua Kunyamaza.
 
Mmechagua kukaa kimya kivipi? Mbona ni kama mmemjibu tayari kwa bandiko hili? Anyway nilitaka kuuliza hivi hii timu yenu nani ni mmiliki wake?
Fedha zote za Wizara ya Fedha zielekezwe katka Kilimo cha Mafuta ya Alizeti kutoka Mkoani Singida.
 
Iwe ni kweli imemtokea huyu kocha ama la,huu mchezo upo sana hapa Tz ndio maana mimi nilikacha kushaabikia kabumbu.
 
Asipokuelewa kwa UKWELI HUU USIPOTEZE MUDA KUMUELEWESHA TENA.
 
Kwanini mnapenda Kumsumbua Msemaji wa Timu ( Singida Fountain Gate FC ) nyie Members?

Mmehajibiwa kuwa Mmiliki wa Timu ni Bwana Makau wa Fountain Gate na Sharti la Umiliki wa Timu alilopewa ni lazima Timu iishi Mkoani Singida na si Kwingineko sasa mnaendelea Kuhoji nini tena?

Hebu iacheni Singida Fountain Gate FC ijikite katika Maandalizi ya Mechi yao ya Klabu ya Futures ya nchini Misri ili ivuke na iipeperushe vyema Bendera ya Tanzania.
 
Hii ni shida ya kuamini makocha wageni, hivi Mgunder au Kally Ongala si anafaa tu lazima mchukue nje?
Japo Mimi ni Utopolo ila sipendi makocha wageni hawajui na hawapendi kutumia wachezaji wazawa hata awe na kipaji wanakiua kwa kumuweka benchi msimu mzima!
 
Usifanye watu watoto bro. Mna bahati Magufuli hayupo, asingeruhusu huu utakatishaji fedha
 

Sasa mbona unaleta blah blah na personal attacks? Haya yote ni marudio, bado hakuna ushahidi wa haya yaliyosemwa na kocha ndio maana anakuwa muoga wa kuweka claims zake kwenye maandishi na kutuma kwa uongozi. Ni media propagandist kama wewe.
 
Mmekaa kimya vipi wakati tayari tunaona jinsi mlivyojifunga Kanga na kumjibu tena huku mmebana pua na mkipeperusha vidole hewani?

Chambaneni na sutaneni wenyewe
 

Mimi kazi yangu ni kueleza ukweli na kuondoa upotoshaji unaoharibu image ya klabu. Wewe kazi yako ni kupiga blah blah mitandaoni kufurahisha nafsi. Sina majibu ya kukufurahisha mkuu na sipo hapa kukulazimisha chochote!
 
19 September 2023
Johannesburg, RSA

Kocha Ernest Middendorp mzaliwa wa Germany ndani ya studio za 947joburg South Africa aelezea yote katika Singida Big Stars, huku meseji nyingi zikimiminika studio kocha yuko wapi, tatizo nini ... yote hayo yapatiwa maelezo ya kina na kocha

Ernest Middendorp resigns after two weeks | Robert Marawa


View: https://m.youtube.com/watch?v=ilcjvpPOk0s
www.947.co.za

Nilikuta timu ya wachezaji 29 ambayo ilibidi mimi kama kocha mkuu na timu yangu ya makocha wasaidizi kufanya kazi kubwa kuiweka sawa ili ipambane na klabu ya Modern Future FC ya Egypt na hata matokeo yetu ya ushindi wa bao moja ktk mechi hii ya kimataifa ilibidi timu nzima na makocha kupewa sifa badala ya meseji za kubeza kutoka kwa mwenye timu ya Singida Big Stars kuwa fulani na fulani lazima wacheze .

Mfano wachezaji wetu kadhaa waliosajiliwa kutoka Togo, Kenya n.k waliopo Singida Big Stars hawakuwa tayari kimchezo maana ndiyo walikuwa wamewasili kutoka nje makwao hivyo walikuwa wachovu wasingeweza kucheza dakika zote 90 na hakika ushindi wetu dhini ya Modern Future FC ni wa kushangaza maana timu yetu ilikuwa bado haijaweza kuwafanya wachezaji kusomana kimchezo ili kupata ushindi, Kocha Ernest Middendorp anapigilia msumari uamuzi wake.

Kocha anaongeza kuwa tarehe 30 August 2023 nilisema wazi bila kupepesa macho kuwa kuelekea mechi yetu ya kimataifa timu ya Singida haikuwa ipo tayari maana wachezaji wake walikuwa bado kujua majukumu yao binafsi na kitimu. Halafu kama kocha unajutahidi kukabiliana na hali hiyo mwenye timu anaingilia majukumu yetu makocha nani acheze wakati suala hili ni la kiufundi siyo la kiushabiki.

Kuingiliwa kazi zetu makocha haitupi uhuru na kujiamini katika kazi zetu za soka hivyo nimeamua kukataa kuwa kikaragosi wa viongozi wasioheshimu utaalamu wetu katika soka, hili ni sawa na viongozi kukosa imani nasi hivyo siwezi kufanya kazi katika mazingira ya kuingiliwa kazi zetu huku mimi na benchi langu kwa asilimia 100 wiki zote mbili akili zetu tulijitosa kuiweka timu yetu katika nafasi ya kiushindani.

Katika kubalansi shutuma hizo 947joburg iliongea live na Hussein Masanza mmoja ya viongozi wa Singida Big Stars kuhusu sakata hilo, Massanza anasema bado Singida Big Stars wanamtambua ni kocha wa timu yao kwani taratibu za kimawasiliano ya kuacha kazi bado hazijatimizwa, Hussein Massanza anasema ni hayo tu kwa leo anaweza kuiambia 947joburg .co.za na wasikilizaji wa show hiyo ya sports.
 
Sasa mbona unaleta blah blah na personal attacks? Haya yote ni marudio, bado hakuna ushahidi wa haya yaliyosemwa na kocha ndio maana anakuwa muoga wa kuweka claims zake kwenye maandishi na kutuma kwa uongozi. Ni media propagandist kama wewe.
Kocha kaeleza sababu za kutokuwepo kwenye timu ni kutaka kupangiwa kikosi na wenye timu .
Sasa tukuulize wewe kama msemaji wa timu kipi kimefanya kocha kuondoka na kuiacha timu yenu ndani ya week 2 tu , tatizo haswa ni nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…