Sakata la Lissu v Tigo: Serikali haitahusika kama hakuna barua za Serikali kwenda Tigo

Sakata la Lissu v Tigo: Serikali haitahusika kama hakuna barua za Serikali kwenda Tigo

..hata kama ikiwepo barua, bado mahakama itachambua ushahidi, ili kujiridhisha kama barua hiyo ilifuata taratibu za kisheria, zinazohusu masuala ya kampuni ya mawasiliano kutoa taarifa za mteja.
 
Njia rasmi ndio njia gani?

Uhalifu mwingi siku zote hufanywa kupitia njia zisizo rasmi na ndio maana hakuna sheria inasema uhalifu uliofanywa kwa njia rasmi pekee ndio uhalifu

Point ya msingi ni uhalifu umefanyika na sio umefanyika kupitia njia gani.

Kwamba ikithibitika ni kweli serikali imehusika ila haikutumia njia rasmi, hiyo itafanya serikali kuwa sio muhusika wa jaribio la mauaji?
Good questions..

Kilichofanyika dhidi ya Tundu Lissu ni uhalifu wa kidola kwa maana ya aidha dola kwa ujumla wake au baadhi ya watu wa dola kwa namna yao na kwa matakwa yao binafsi...

Bado huo ni uhalifu tu...

Robert Heriel Mtibeli jibu maswali hayo...
 
Kesi hii imesukwa katika muundo wa Kuua Ndege wawili Kwa jiwe Moja.
Kwa vile kuishtaki serikali na kuituhumu Moja Kwa Moja kuhusika na tukio la Lisu itakuwa na mlolongo mrefu katika Kutoa ushahidi na uthibitisho hivyo njia au upenyo rahisi NI huu WA kuanzia na wale waliotoa location ya kîla alipokuwa LISU. Alafu hao ndîo watatumika kama mashahidi katika Kesi ñyiñgine ya tukio la September 7
Kwa kauli yako hii, naona umelikana rasmi andiko lako kuu (uzi wako mkuu)..

Hongera sana kwa kuwa wewe ni mtu wa kuelewa haraka na kujisahihisha...

Si sawa na watu hawa comte na Joseph Ludovick ambao wakishikilia uongo, watakomaa nao mpaka kaburini...
 
Ghafla nimejikuta nampenda Lissu. Ni watanzania wachache sana wana akili na uwezo wa kumuelewa. Hawawezi kumuelewa lakini kwa akili zao ndogo wamejiaminisha wanamuelewa. Miongoni mwa waliojiaminisha hivyo wapo hadi maprofesa na madaktari wanaomuona kama mkurupukaji.. Hatari sana...kweli akili kubwa ni tunu.

Tik...tak...tik...tak...tik...tak...
"Maprofesa" wengine wa UVCCM wagumu kuelewa ni hawa comte, Joseph Ludovick, Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah etc
 
Mkuu umeweka vitu kama vitatu kwambo rasilimali kwakua niyaserikali moja ya sababu nianze kwanza na mtu anaetuumiwa kuratibu tukio uyu jamaa akuwa ktk mkoa wake na kisheria ukitoka ktk mkoa wako ww unamlaka yyte nje ya mkoa wako pili ikiwa sababu ni utumishi yani anawajibika mwajili kama ivi basi serikali inamadeni mengi mfano tu juzijuiz apa kulitokea polisi kupigana risasi kwasababu zao wenyewe.je ile famiria ya aliekufa inafaa kuishtaki serikali.na ikiwa ndio rasilimali lipo tukio la polisi kujipiga risasi mwenyewe kwasababu zake mwenyewe je nayo famiriayake iende mahakamani kuishtaki serikali sababu iyo bunduki ni Mali ya seeikali?
Ndugu huwezi kuandika vizuri ukaeleweka?

Na Kwanini usifanye proof-reading kila unachoandika kabla ya kupost kwa ajili ya kuliwa na umma (for public consumption)...?

Kama kuandika tu kwa kiswahili fasaha huwezi, kisha kuhakiki na kusahihisha makosa ya uandishi, unaweza vipi kuyaelewa haya mambo ndugu mdogoye...?
 
Kwema Wakuu!

Serikali haitahusika Kwa namna yoyote Ile Ikiwa haikuandika barua Wala Kûtuma email kwenda Kampuni ya Tigo kutaka kuingilia faragha na tàarifa za LISU.

Mambo ya serikali Kwenda Kwa makampuni au mashirika hufanywa kiofisi na barua lazima ihusike.

Mawasiliano yoyote àmbayo hayatahusisha njia rasmi huweza kuleta mkingamo wq kisheria.

Hivyo itasemwa kwamba kulikuwa na genge la Watu weñye Maslahi binafsi nje ya serikali àmbalo ñdilo liliwasiliana na Kampuni ya Tigo kutaka tàarifa za LISU.

Hii inatoa Somo Kwa wafanyakazi na Wamiliki WA makampuni kuwa Makini Wakati wanapata oda au maigizo Kutoka kwèñye mamlaka za kiserikali. Kwamba maagizo hayo yawe Kwa njia Rasmi ikiwemo kuandikwa Kwa barua kama ushahidi.

Haya
Mahakama za wenzetu si sawa na hizi Mahakama za mchongo.

Mnufaika wa taarifa unamwekaje kando !.
Tuliza mshono bado hapajapambazuka Jogoo halijawika unakimbilia wapi vuta subra.
 
"Maprofesa" wengine wa UVCCM wagumu kuelewa ni hawa comte, Joseph Ludovick, Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah etc
gentleman,
hakuna haja ya kujitabiria au kujiheshabia haki kwa kutegemea ramli, ushirikina, ushabiki wa mitandaoni, wala huruma au uchawi kwenye mambo muhimu ya wazi tena ya kisheria...

sichochewi wala kuongozwa na mahaba au hisia za kusiasa kujadili mambo ya kisheria... :pulpTRAVOLTA:
 
Nikikumbuka voice ya kina January, Nape na Kinana zilivyovuja wakimsema namba moja wa kipindi kile, huenda walimtumia mtu kinyume na utaratibu na kwa kificho kufanya kazi hiyo
 
Back
Top Bottom