SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Nilitaka kuweka andiko sawa kwa sababu niliye mu-quote aliandika kuwa Aeshi ni Mwenyekiti wa PAC.

Nilisema kuwa Bunge limejaa wala rushwa nikiwa na maana, usishangae hata huyo Aeshi anaweza kujitokeza na kusema vyombo vya habari vilinielewa vibaya.

Kuhusu waandishi wa habari ninamaana wengi wao ni wachumia tumbo kwa sababu wanaandika habari kwa sababu wamekula rushwa au wamelipwa nje ya utaratibu/sheria na siyo kwa sababu wanaisaidia jamii kwa sababu wao ni muhimili wa nne katika Taifa baada ya Bunge, Serikali na Mahakama.

Rais kwa sasa hawezi kutoa maamuzi kwa sababu suala liko mikononi mwa bunge. Kazi ya Bungu kwa sasa ni kutoa ushauri kwa serikali kuhusu nini cha kufanya kuhusiana na suala hili.
 
 

Mkuu
Angalia utapigwa BAN..
Jecha wa jf hapendi hilo neno la Vi..wa..vi
 
Nimekudharau kabisa. ww ni bure bora angezalowa panya kuliko ww.
Sijawahi kukuomba usinidharau.

Kunidharau au kutonidharau ni uamuzi wako kama ulivyoamua kwa hiari yako kusoma comment yangu.

Ninashangaa kwa sasa unaniambia umenidharau wakati hujawahi kuniambia kama ulikuwa hunidharau. Wewe vipi?
 
Mkuu
Angalia utapigwa BAN..
Jecha wa jf hapendi hilo neno la Vi..wa..vi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] , nashukuru Mkuu kwa tahadhari! Hasira tu!
 
Kila nikitafakari naona watu wanaitwa majipu takribani walioshika nyazifa za juu serikalini.Serikali iliyopita imefanya mema na mabaya mengi ila dalili inaonyesha unataka kufanya mema na kuwadhibiti wanaofanya mabaya katika utawala wako.Kwa hali hii ya kutumbua wenye nyadhifa za juu serikali wa serikali iliyopita naona kama unawaonea tu maana huenda hata waliokuwa waadilifu walibadilishwa kwa kupokea VIMEMO kwa kila uamuzi walioufanya hivyo leo wanawajibishwa kwa makosa ya wengine.
Anza ukurasa mpya maana jinsi wewe unavyoona ugumu wa kutumbua majipu ndivyo na wao walikuwa wanaona kupinga uamuzi wa aliyeko juu yake.
 
Wewe si bunge wala Lugumi ama mmiliki wa polisi bali ni mtetezi wa kila kinachofanywa na serekali hii ya ccm hata hivi vituko.

Bunge kufanya hivyo si hisani ni wajibu wao huku wakijilipa hela zinazotukwaza tulio wengi wakati wana tija ndogo.

Kwani ni kipi kikubwa kilichofanywa na kamati ya PAC wakati wa bunge lililopita na serekali ikatoa msukumo wenye tija?

Mbona bila hata hiyo misaada bado tunaingia mikataba ambayo hata ni aibu kuiweka hadharani? Kwa hiyo ajenda zilizojificha sio kitu cha ajabu kwenye hiyo misaada kwani hata kwenye mikataba yetu ya hiyari bado tunapigwa tu bao.

Iwapo taifa litaendelea kuwa na mambo ya ajabu hivi kuendelea kutegemea misaada haitokuwa ajabu.

Kilichoua hivyo viwanda vingi mpaka leo imegeuka viwanda ni historia ni nini?

Yeye hanilazimishi ila nyie wapambe ndio kila siku kunyooshea vidole wale wasioimba mapambio.

Ndio nasubiri kupigiwa debe kwani yeye anatokea kwenye chama kilichotufikisha hapa yeye akiwa sehemu ya serekali hiyo kwa takribani miaka 20 sasa.


Kwani tuna marais wangapi mpaka nipate mwingine ambaye nina imani naye wa kumlinganisha? Simply sina imani na yeye, kama wangekuwa wengi kwa sasa ningekuwa na uchaguzi.

Kwa hili uko sahihi kwani nchi ya watu wenye uwezo wa kufikiri tunatarajia mgongano wa mitazamo

Wangalau anajitahidi, sina hakika kama tungepata mwingine mwenye uwezo wangalau wakwake, ila mimi ningeweza kwani sina mafungamano na hao walioko kwenye mfumo.

Nami nimalizie kwa kusema hivi vita vinaonekana kama jemadari wetu anaanza kupiga risasi kwa kuogopa kuua wajomba upande wa wale anaotakiwa kuwaangamiza. Hongera pia kwa kuchangia kiungwana hata kama mambo hayaendi kama ambavyo ulitaka yawe.
 
Sijawahi kukuomba usinidharau.

Kunidharau au kutonidharau ni uamuzi wako kama ulivyoamua kwa hiari yako kusoma comment.

Ninashangaa kwa sasa unaniambia umenidharau wakati hujawahi kuniambia kama ulikuwa hunidharau. Wewe vipi?
upuuzi mtupu. mjiongeze sio kila jambo la kutetea mchana kutwa. kuna mengine ni dhambi na laana.
 
Inasikitisha.... mtu anasafishwa hivihivi

Sasa subiri usikie jinsi walimu, madaktari na watu wa nafasi za chini wanavyopigishwa kwata... Ni balaa
 
Wacha warudi majimboni tuwaulize kama ndio tuliwatuma watuletee unafiki. Hivi naomba kuuliza, kama wapiga kura wanaweza kumwondoa mbunge kama hawana Imani naye!!?
 
igizo limeingia sehemu ya nne
1.Kamati ya PAC kudai Mkataba
2.Kamati ya Mambo ya nje kupewa jukumu la PAC
3.Said Lugumi kutoweka nchini
4.Bunge kudai kilicho takiwa na PAC si mkataba bali Maelezo
5....
Ndio maana mm huwa sipendi movie za series zinafanya unakuwa mtumwa nishachoka na hii movie
 
Leo nimejikuta namkubali na kuyakubali maono ya Pasco wa JF.
Duuh
 
sio lugumi mkuu wanasiasa ndo wenye nguvu kama wanasiasa wakiacha siasa na kutekeleza majukumu yao kwa taifa lugumi ni mweupe kama unga wa ngano!!!

Wanasiasa kwa upande wa pili nao ni watendaji Serikalini ,inawezekana nao wakawepo katika wizi huu wa mchana hivyo suala hili ni gumu kutumbuliwa.Ukitaka kujua hebu ona namna wanavyo rushiana mpira wakati kila kitu kipo wazi hapo.
 
Kama picha zinachezwa serikali hii zingetengenezewa move lingekuwa bonge la move la ki cia au mossad.
Magufuli big up mzee ye can
 
Mbona za sakafuni huishia ukingoni. Maana iweje pesa ilipwe karibu yote zifungwe 14? Dr John fantastic ziara lush tukiwa hapo mambo ya ndani
 

JM na humu yumo, hela wanatakatishia wapi, Bumbuli Corp?
 
Kama nilivyoandika hapo juu, siwezi kujibu hoja zako kwa sababu hazijakaa katika mpangilio mzuri.

Sorry.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…