apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Vyanzo vinadai kuwa kulipeleka swala hili mahakamani, litanyima fursa ya Bunge kulizungumzia. Binafsi sitegemei jipya kupitia Bunge hili na kama ikitokea basi utakuwa muujiza wa kwanza wa Bunge letu katika Serikali hii "tata". Hoja ya "collective responsibility" ni changamoto katika mhimili huu mzito kuliko yote (Sauti ya Wananchi yenye Mamlaka kamili) kutokana na maslahi ya kivyama na hofu.
Nashauri mjadala huu ufungwe ama wenyekuhitaji kupata haki ama maamuzi sahihi yasiyo na shaka basi angalau waelekee kwenye mhimili wa "Mahakama"....kwa hoja kuu tatu:-
1. Kufungua shauri linalomtaka Makonda kuwasilisha vyeti vyake vya elimu hasa kidato cha nne (Wanasheria wapo na wanaweza kusaidia)
2. Clouds kumfungulia kesi ya jinai Ndugu Makonda kwa kuvamia kituo cha habari (Hili linahusu kituo cha habari chenyewe hasa katika wakati huu ambao Jamhuri inaona si kosa)
3. Nape kufungua shauri juu ya kutishiwa maisha na Askari kanzu (Hili lina muhusu Nape hasa ukizingatia mazingira ya Jamhuri kutokuona kama ni kosa)
Ndugu wanabodi, pamoja na madhaifu makubwa ya katiba yetu, bado katiba hii ya mwaka 1977 haijanyima haki kwa Wananchi wake. Bunge lina mamlaka kamili lakini aliwezi kutekeleza majukumu yake kikamilifu kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu. Mahakama kama chombo chakutoa haki, bado kina fursa ya kutafsiri sheria, kukutanisha pande zote mbili ama kuchukua hatua (kutoa hukumu ama kuachia huru).
Wito wangu: " Kwa Bunge hili tulilonalo, Mahakama ni bora zaidi"