Sakata la Richmond: Lowassa amjibu Mwakyembe, asema asitafte mtaji wa kisiasa

Kama mnawajuwa watuhumiwa ni kwa nini hamuwakamati? Hivi na ile mahakama ya mafisadi vepeeee!?
Ni aibu sana leo mtu unajua kama mfumo wa nchi ulivyo alafu unakuja unamtetea Lowassa hapa kisa kahamia upande wako, wakati walioathirika na ule ufisadi wa richmond ni mama, baba, bibi na ndugu zako wengine kule kijijini.
 
Huyo mungumtu wenu hasafishiki
 
Serekali ya CCM ndiyo yenye serekali pekee duniani kuwahi kutokea,wananchi wameibiwa,wao kama serekali wamemubaini mwizi aliyewaibia wananchi ni nani,badala ya kumpeleka mwizi mahakamani wao ndiowamekuwa wa kwanza kumkimbia mwizi,kadri mwizi anavyokazana kuwafukuzia wampeleke mahakamani kwa kuwa wamembaini kuwa ndiye mwizi aliyewaibia ndiyo kwanza wanaongeza speed kuelekea kichakani kusaka maficho ya kujificha,kama simba aliyegeukwa na swala aliyekuwa anamkimbiza ili amtafune badala yake kibano kimemugeukia mwenyewe aliyekuwa anataka kumtafuna.
 
Ni aibu sana leo mtu unajua kama mfumo wa nchi ulivyo alafu unakuja unamtetea Lowassa hapa kisa kahamia upande wako, wakati walioathirika na ule ufisadi wa richmond ni mama, baba, bibi na ndugu zako wengine kule kijijini.
Mahakama ya mafisadi si ipo? Sasa porojo za nini?
 
Hili ndilo wazo langu sana. Hii richmond ndio symbion kwa sasa. Mzinduzi wa symbion allikuwa Obama alipokuja tz. Na kweli Bush na viongozi wengine waandamizi wa USA wamewahi tembelea mitambo ya symbion na kuisifu kazi yake. Ndio hapo naona si Lowasa wala Kikwete bali shinikizo la mashetani wa dunia USA. Halafu nasikia Pombe amedhamilia kuuvunjilia mbali huo mkataba. Tahadhali, namuomba awe anatembelea jukwaa la JF intelegence hasa makala The Bold. Ni vema akamjua adui huyu wa dunia kabla hajafanya maamuzi.
 
Mtavumilia lakini kama EL akishtakiwa na kukaa ndani bila dhamana kwa kipindi chote cha kesi yake. Make fisidi hana dhamana! Msije kulia lia hapa.
Acheni kuweweseka fisadi anasema mpelekeni mahakamani na siyo akanyimwe dhamana,akafungwe kabisa na ikiwezekana mkampe adhabu ya kunyongwa.
 
Kama kuna MTU anaamini maneno ya mwaki,akapimwe akili!
 
Watu wajinga sana. Kwani issue hapa ni Lowassa kausika au kausika nani na nani?nyika nimemtoa thamani sana na chadema kwa ujumla. Tupeni jibu kwanza lowassa kausika hajausika alafu mambo mengine baadae.
 
Wapi Lowassa ameitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia ufisadi,au unaliamini hilo gazeti la Mbowe la kufungia utumbo
 
Polonium ndio inamsumbuwa Mwakyembe ubongo umeshaoza umejaa fungus.

Mwakyembe na marehemu Samuel Sitta ni watu wa ajabu sana kuwahi kutokea hapa duniani.
Ajabu unawasifia wauaji waliotaka kumuua Mwakyembe kisa uraisi na uraisi wenyewe hawakuupata,kamwe wauuaji hawataongoza nchi hii
 
Ajabu unawasifia wauaji waliotaka kumuua Mwakyembe kisa uraisi na uraisi wenyewe hawakuupata,kamwe wauuaji hawataongoza nchi hii
Mahakama ya mafisadi mliofunguwa ya kazi gani?

Bastola ya nini tena? Weka vyeti acha porojo.
 
Chadema kweli misukule,walianza kutekwa,mara Bashite na sasa Richmond utadhani wao hawakuhusika wakati Richmond ikinguruma Bungeni ,pale kuna Hansard na wangekuwa werevu wangerejea kujikumbusha waliyoyasema wakati wa mjadala kuhusu Richmond,kweli nimeamini mchawi mpe mwanao akulelee ,Chadema washajisiriba mavi wananuka na hawatoki kwa kubadili gia angani,kila watakapoenda uvundo unawafuata nyuma.
 
Serikali kupitia kwa AG inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi rasmi kuhusu sakata la Richmond na kuchukua hatua mwafaka. Siasa ikae pembeni sasa. Inafaa Serikali ifanye hivyo sasa ili kama kuna hoja, lipelekwe kwenye mahakama ya mafisadi iliyokosa wateja!
Ukweli ujulikane isiwe miaka nenda rudi, kupiga stori kuhusu Richmond!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…