Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama

Inafikirisha sana kwamba wachezaji wote waliosajiliwa na simba wazawa wana migogoro kwa nn international players hawana shida na simba yanga wana roho mbaya.
Umeongea kama nilivyotaka kuongea.. ongezea hapo na wachezaji wengi wa nje wa Yanga wana kesi za madai FIFA.
 
Yanga wamechungulia wameona huu msimu ni mbaya kwao hivyo wanaona njia pekee kwao kutoboa msimu huu ni kwa Simba kukatwa point, lakini wajue mwaku huu wameuanza vibaya kwa dalili hizi.
 
Kumne hata hauelewi hili sakata lipoje? Kagoma hakua na mkataba na SBS alikua huru alicho fanya yeye ni Ku sign timu mbili kwenye dirisha moja la usajiri
 
Yanga mna mbwembwe sana.

Viongozi wenu wameshachachawa wewe unajifanya huna hofu.
Namba zinaongea wachezaji wa Yanga wote 14 wanakiwasha timu zao za taifa, ngoja warudi NBC premier league uone moto wao. Kwa uzoefu wanaopata huko Afcon ni dhahiri hii Yanga itazionea sana underdogs kama Simba, KMC, Azam na zingine!!

Mtani hiyo kuchachawa ni taarabu tu umeongea!!
 
Kumne hata hauelewi hili sakata lipoje? Kagoma hakua na mkataba na SBS alikua huru alicho fanya yeye ni Ku sign timu mbili kwenye dirisha moja la usajiri
Kama iko hivo inamaana atakayeadhibiwa ni mchezaji na siyo simba kupokonywa points
 
Yanga wamechungulia wameona huu msimu ni mbaya kwao hivyo wanaona njia pekee kwao kutoboa msimu huu ni kwa Simba kukatwa point, lakini wajue mwaku huu wameuanza vibaya kwa dalili hizi.
Huna timu ya kutamba msimu hiuu,shukuru umeanza na timu ambazo key players wake zaidi ya watano hawana vibali, yaani msimu huu Yanga anakubonda kama mwaka jana cha msingi jiandae kupunguza idadi ya magoli, ila unapigwa mechi zote.
 
Yanga bwana!!!
mradi kolo ashuke daraja tu...
 
Kwanza anatakiwa kuulizwa aliyetoa leseni kuwa mchezaji achezee Simba, sioni kosa la Simba hapo.

Hata hivo watu wanaongea kwa mihemko utafikiri hawaujui mpira wa Tz.
Simba na Yanga ndiyo wenye TFF hata zivurunde vipi maamuzi yatafanyika kwa busara tu hamna wa kukatwa point
 
Ushabiki mbaya Sana ndugu hivi unafikili Simba anaweza akapokonywa point Kwa ujinga wa Mchezaji mwenyewe na Nani alitoa kibali ili acheze na hata Shauli lililopo ni Kati ya Yanga na Mchezaji na si Simba
Utajua tuliaaaa moto unakaribia
 
Yanga bwana!!!
mradi kolo ashuke daraja tu...
Mbumbumbu hatakiwi ashushwe daraja, inatakiwa abakie tuwe tuna shuhudia Wanavyo teseka kwa makosa Yao wenyewe.
Sisi ni kuwa tia taharuki tu ili wawe wanakoseaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Hiyo kesi ya madai, waende tu mahakamani. Nao Yanga ni wajinga, watampaje hela mchezaji wakati bado hawajauziwa na mmiliki? Ni sawa na kumlipa dalali wakati hujamalizana na mwenye nyumba, kama imeshauzwa je?
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Yanga siyo wajinga, walishafanya naye pre-contract ambayo kisheria inaruhusiwa, pre contract hiyo ilishaanza kufanya kazi kwa Yanga kutimiza yale aliyotakiwa kuyatimiza. Mchezaji na viongozi wakadhani itakuwa rahisi tu wakipanga kuwarudishia Yanga hela yao.

Simba wakajitokeza na wao wakaingia naye makubaliano. Yanga wakaja kushangaa mchezaji anatangazwa kuwa ni mali ya Simba. Hapo timu ya mchezaji, Mchezaji tayari wamefanya kosa. Simba itakuwa muathirika tu kwa kupewa huduma na mchezaji huyo.

Kumbukeni, Yanga ina sign ya club na mchezaji waliyoingia kwenye pre contract.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…