Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Kama ni ya kushtukiza hayo makamera yametoka wapi? Mbona jamaa wa hayo matanki kama alikuwa na taarifa ndiyo maana emetoa desa mfukoni alilokuwa ameandaa?!!
 
Ziara ya ghafla na TBC wapo ! Humdanganyi mtu yeyote ! Halafu badala ya kukagua hivyo viwanda zaidi ya elfu 3 ambamo bila shaka vya mafuta ya kula vimo kwanini anaenda bandarini ?
Nice observation....hamna haja yakubembeleza wauza mafuta ya kula wa viwanda vya zamani wakati kuna viwanda zaidi 3020 vipya .......
 
Tatizo langu kubwa ni moja. Hata ukiwa nyumbani kwako unaweza kupima mafuta na kujua haya ni crude au refined kwa kigezo cha Free Fatty Acid. Unahitaji Sodium Hydroxide, Ethanol na Indicator(hivi unaunua kwenye maabara ya mtaani tu) na gram 10 za mafuta kufanya neturalization process ambayo kama itachukua muda mrefu sana ni robo saa. Hata mwanafunzi wa darasa la saba akielekezwa anafanya kwa ufanisi mkubwa tu hii kazi. Sasa hiki kilichokuwa kinaendelea kati ya TBS mara TFADA mara mkemia mkuu kwenye maPHD mara waziri yaani naona kizunguzungu.Siku zote hizo wameshindwa kujua kuwa haya mafuta ni crude au refined hadi mgogoro umefika bungeni hadi kwa rais. Kweli mtu akisema yupo frustrated ana haki. Labda niamini kuwa kulitegeshwa upigaji mkubwa. Unless kuna kitu sjaelewa vizuri
Nyie mlio soma kemia ndo shida ya nchi sasa mnajifanya mnajua mengi......aibu tu
 
Mzee anazidi kutupa makali ya maisha tu hana jipya viwanda vya ndani vyenyewe vimewashinda unategemea nini
 
Kazi za mawaziri hizo, anaenda Mh Rais, mimi bado nina wasiwasi na watendaji wa hii awamu, sijui kama wanamuelewa Rais. Kwa jinsi ambavyo Rais amekuwa akifuatilia mambo kwa kwenda sehemu husika, nilitegemea kwa kipindi tu hiki cha miaka miwili basi makatibu wakuu, mawaziri wangekuwa wanafuatilia sana mambo haya, lakini toka sakata hili limeanza si waziri wa viwanda, fedha au uchukuzi kuwaona wapo mstari wa mbele kufuatilia hili jambo, sasa leo katoka Rais mwenyewe, na kitu kinarushwa live, jamaani huyu Rais mtaazeesha kwa kufanya kila kazi peke yake!!
Atazeeka nani, Magufuli?
Subutu!
Yule mzee ni push up na hapa kazi tu!
 
​

Mhe. Rais Magufuli afanya ziara ya ghafla bandari ya Dar es salaam muda huu. Anakagua matanki ya mafuta ya kula. Fuatilia matangazo TBC1 muda huu.

Atembelea kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam na kupewa maelezo kuhusu Mafuta kukwama bandarini.

Rais Magufuli amesema...

Baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa kwenye matanki hayo kuna ambayo yalikuwa na 'crude oil', na mengine yalikuwa na 'refined oil' ambayo yalifichwa kwa makusudi.

Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei. Nawaomba tuwe wazalendo. 'Crude Oil' ichajiwe bei ya juu ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Haiwezekani 'crude oil' ukachaji sawa na 'semi refined', na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo. Wabunge walipitisha kitu kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupitishwa kuwa sheria kimebadilishwa kuwa kingine.

Hii 'crude oil' ichajiwe bei ya juu ili watu wengi wajenge viwanda hapa, tujenge nchi yetu.

====

UPDATES:

Rais Magufuli anasema;


=> Nlituma wachunguzi wangu waje kufanya analysis ya haya mafuta. Wote wameleta majibu sawa. MAfuta yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Nmesoma ripoti yote.

=> Ukitaka kutengeneza mafuta yoyote, kwanza mafuta yote yanatokea kwenye crude Oil, yakishatoka kwenye crude Oil..unafanya Neutralization na kwenda semi-refined oils au bridging kuchange coloue of oil. Viwanda vingi vya tanzania ni semi refined Oil. Double refined.

=> Tatizo tulilonalo;

*Crude inachajiwa 10%

*Semi refined inachargiwa kwa 10%

Sasa unakuta vyote vinachajiwa sawa.
Nakumbuka kuhusu makenikia
 
Nakumbuka mh,sugu aliwai kusema mwishowe wataitwa Mr bandari
 
Lissu alishawai kusema kitakachosaidi ni kubadilisha mfumo,na sio ziara za bandarini Kila siku
 
Hivi bandarini na haiana wafanyakazi?maana Kila siku itabidi aende bandarini
 
Mkuu wetu hapa anachemka kwa kutokua na imani na TBS na kuonyesha wazi kuwasifia TRA, hizi zote ni taasisi nyeti za serikali inabidi awe makini na maamuzi/matamshi yake.
Muda ni mwalimu mzuri
 
cheap public stunt.
create the problem, then come back in and offer the solution that the people demand.
Kwakweli,kwa maelezo yaliyotolewa hapo sijaona tatizo la kumfanya Rais kuingilia kati,maana kama kungekuwa na tatizo basi mtu angetumbuliwa hapo.halafu eti kuna waliyoficha hawajayadeclare!?halafu haohao ambao hawajadeclare mafuta wamekwepa kodi wanashikana mikono na Rais!?
 
Nampongeza kaimu Kamishina wa TRA aliyesimama kidete , maana imegundulika haya mafuta siyo CRUDE bali ni mchanganyiko yako Crude yanayotozwa 10% tax , Semi refined 10% na double refined yako Matanki 7 yaliyopaswa kulipiwa 25%. Hongereni TRA kusimamia ukweli huu
Yule mzungu kasema refined wali declare na report wanayo TRA walitaka yote kuwa refined ndio tulisikia bungeni kwa waziri. sasa kiliwazuia nini kuruhusu crude sokoni na kushikilia yenye mashaka wao wakaenda kuzuia yote ina maana ni kweli walikuwa wanasema yote refined. huyo mzungu kasema clear refined yalikuwa declared hakuna kipya hapo.
 
Back
Top Bottom