Sakho na Phiri waomba kuondoka Simba

Sakho na Phiri waomba kuondoka Simba

Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa nilizopata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili POS aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

Sakho alisaini kandarasi ya miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, akiwa ametumikia miaka miwili huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, tayari ameshaandika barua.

Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.

Mchezaji mwingine aliyeomba kuondoka Simba ni Mzambia Mosses Phiri, ambapo wanakuwa ni wachezaji watatu mpaka Sasa hivi baada ya Awali Joash Onyango kuandika barua ya kuondoka klabuni hapo.
Ebu thibitisha ili tuchangie, siyo kutuletea habari za vijiweni, sisi siyo wavuta bangi.
 
Ukiona mwenye nyumba analipiwa kodi kwa nyumba hiyo hiyo.. Ujue mapenzi hayo ni hatari.
Mapenzi yamenizidia, waweza nipikia msosi na nikaulipia wakati na mahari nishatoa.

Mapenzi tu
😍😍😍😍😍
 
Kabisa tu, ufurahi wewe kila siku, hiyo furaha umeiumba wewe..
Kikubwa ni kuendelea furaha hata siku za majonzi kwa kukubali uhalisia.

Msimu haukuwa wetu, kuna makosa yalifanyika, tumekubali hapo na tuko hapa kuchangamSha baraza(kuendelea furaha)
Faida ni kubwa sana kimaisha kukubaliana na hali yoyote hata kama ni nyakati ngumu, fikiri ile mechi mliyofungwa na Azam FC, kuna Shabiki kindakindaki mmoja wa Makolokolo aligongwa na treni sababu ya stress za kuzomewa na Mashabiki toka kibanda umiza [emoji30][emoji26]
 
Back
Top Bottom