Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Mi nadhani tusiwe na haraka sana, masaa 72 ni siku 3 tu, mbona sio nyingi? Tuwe na subira
ni sahihi, asante sana. kila kitu kiko wazi, uzuri kijana huyo sasa kachoka maana mwanzo alikubali jamaa achukue kila kitu kwa hofu ya kumuua, lakini alimwambia watapiga hesabu amrudishie ziada, toka june 14, 2022 jamaa hapokei simu, akienda ofisini anaambiwa jamaa yuko bize. sasa kasema hata kama ni kufa yuko tayari kufa, hivyo hakuna kitachofichwa hata jina lake litatajwa kuweka rekodi sawa, na kama wanasema wana uwezo wa kumuua basi wajue kwa sasa yuko tayari kwa lolote maana jamaa alichukua hadi mali za watu wengine na sasa ana madeni mengi sana na kuna watu wanamuwinda wamuue maana jamaa anawaambia alishachukua chake na kumrejeshea jamaa pesa zingine hivyo wakamdai yeye, kumbe hana kitu na hajapewa pesa zake.
 
RIP JPM ...kwa akili yangu ndogo ya kujua vitu...hivi kapuni ya silent ocean wanalipa kodi kabisa kabisaa inayostahili...moja ya udhaifu wa utawala huu ni kukumbatia hawa watu..JPM aliwabana hakuna rangi waliacha ona..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
hawa watu hawawezi kulipa kodi, sisi ndio tutalipa tozo na mikopo kibao ili serikali iweze kuendesha kazi zake.
 
Chuki zako binafsi tu na matajiri. Kama una ushahidi kwanini usiende mahakamani? huna mali anayoweza kuingangania salaa wala nini. Mwache stese hata nyie masikini wakati wa JPM mulijiona kama ma alst born wa Rais mukajipiga kifua na kujiita wanyonge na wazalendo
Tafuta ukweli kwanza kabla ya kutumia neno chuki zako tu. Penye ukweli, uongo hujitenga
 
Eleza mwanzo mpaka mwisho, sakata lilipoanzia mpaka kuja kuzulumiana mali, ikiwezekana weka na uthibitisho.

Ofisi ni kiti na meza
kila kitu kitakuwa wazi mkuu, usijali, itaenda kugusa mifumo yote ya ufanyaji kazi kariakoo, ndio maana unakuta mtu analipa kodi TRA kwa mwaka kiasi cha milioni tatu lakini ananunua jengo la Bilioni 8 kariakoo. na yote haya ni hii mifumo inayoendeshwa na hawa jamaa inawasadia na wafanyabiashara wengi wa kariakoo kukwepa kodi.
 
Tume ya haki jinai imeundwa kwa ajili ya kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuboresha taasisi za serikali zinazohusika na haki jinai kama vile Polisi, Mahakama, PCCB n.k kwa lengo la kuzidhibiti ili zitende haki. Haina mamlaka yoyote ya kisheria ya kuwashughulia hao Silent Ocean. Una nafasi ya kunikosoa.
sijasema tume itakwenda kuwashughulikia bali itapata kujua udhaifu, mfano wa watu kama hao ambao ukienda kwenye vyombo vya kutoa haki wanakuambia kuwa huyu hagusiki tumepigiwa simu na wakubwa.
 
wanajiita waarabu wa Yemen. ila mmoja alishakula tindikali za uso hivi sasa hata akiletewa mrembo haoni uzuri wake, chezea wabongo wewe. ukilindwa na serikali watu wanakuvizia unless waendelee kuishi kama Panya.
Jamaa wana roho mbaya sana hao, Mimi nina habari zao kutoka kwa jamaa wawili ambao walishawahi kufanya kazi kwa huyu Mfadhili wa Yanga, Yaani huwa inasikitisha sana mmoja alikuwa ni Mwalimu alidhurumiwa hela ambayo ilikuwa ni dola 300 maana huyo jamaa alikuwa ni anawafundisha watoto wa Tajiri Tuition, Jamaa akatafuta Mganga awaroge ili alipwe hela yake yule Mganga akamwambia ukweli hawa Wana Majini sana hii kazi ni ngumu we Muombe Mungu ili ulipwe hela yako. Na Mwingine alikuwa ni Fundi Umeme kwenye Kiwanda cha Magodoro kule Mikocheni huyo jamaa alikatwa mkono kimiujiza huyo ndio aliniambia hiyo story ya Kaka Mtu aliyemwagiwa Tindikali nayo ni hivyo hivyo dhuluma. 😢 😢 😢 😢
 
Back
Top Bottom