Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Kama we ni mweupe ✔Mimi wapare siwataki, wakinga wabahili halafu niende kwa wapare tena si nitakufa njaa 😹😹
Mi nawataka wasukuma na hivi mweupe lazima ming’ombe ije mingi kwetu. 😹😹
Si eti shemeji Shimba ya Buyenze
Kama ni mrefu ✔
Kama una miguu mizuri ✔
Kama umesoma ✔
Kama una MTAKO ✔
Kama unajua kupika ugali wa Kisukuma ✔
Haki ya nani ng'ombe ni kuanzia 50+. Japo siku hizi ng'ombe wengi kiasi hicho hakuna, maelewano yatajikita katika kuamua gharama ya kila ng'ombe. Tukielewana kila ng'ombe ni 200,000 basi kwa ng'ombe 50 mahari itakuwa ni milioni 10. Au mnaweza kuchanganya. Ng'ombe halisi 10 na 40 waliobaki mkapiga mahesabu ya pesa kwa kila ng'ombe.
Karibu sana Usukumani shemeji. Hutajuta. Cha muhimu ujue kupika ugali tu basi 😂😂😂