Salim Kikeke rasmi kwenda Crown TV

Salim Kikeke rasmi kwenda Crown TV

Maana ya kutumika, ni kwamba umaarufu na majina yao ndio yanatumika kukuza hizo media. Japo wana hisa. Mfano huyo Diamond unajua hizo hisa 45% kazipataje?
Kama anafaidika na hiyo media huwezi kusema anatumika? Kutumika maanayake hapati kulingana na namna jina lake lilivyotumika
 
Daah hii dunia haiko sawa kabisa..Kwanini Media hazioni new generation ya presenters tupo2 kitaa na tuna uwezo kabisa..wanachofanya ni kubadilisha popular presenter tu bac..wakumbuke hawa famous wanaowabadilisha umri unaenda na hadhira inataka kuskia sauti Mpya
 
Mbona sio tatizo mkuu as long as analipwa pesa anayoitaka? 50 Cent na udogo wake kumbuka aliwa sign Mobb Deep, sio jambo la kushangaza hata kidogo.

Pia Kikeke ni co founder wa hiyo radio na Tv, angalia bio ya social networks zake ujiridhishe.
Au Wiz Khalifa kumsaini Juicy J
 
wameacha wengi na makao makuu yamehamia kenya
Ila Kenya wanajitahidi sana kwenye kuvutia wawekezaji japo Nchi yao haina Utulivu kama tulionao Tanzania.

Maana suala la kupeleka Makao Makuu ya BBC Kenya itakuwa na positive impact sana kwenye Uchumi wao 🙌
 
Watanzania wengi hatuna exposure ya kutosha ndio maana tunashindwa kuelewa vizuri issue ya Kikeke.

Kwa uchache sana. Tufahamu haya kuhusu Kikeke;
1. Kwa mujibu wa Kikeke mwenyewe ni kuwa aliamua kuondoka BBC (hivyo inawezekana aliamua kuacha tu katikati ya mkataba au mkataba wake ulipoisha hakutaka kuomba kuongeza). Upande wa pili, tangu mwaka jana, BBC walibadilisha uendeshaji wa idhaa ya Kiswahili kutoka makao makuu UK, London kuja Nairobi, Kenya. Hivyo kama Kikeke angeendelea kubakia BBC basi ingebidi arudi Dar/Nairobi ili kutangaza idhaa ya Kiswahili ama angebakia London lakini kwenye majukumu tofauti ndani ya BBC, na hii ingefifisha brand yake ya umaarufu wa kutangaza. Upande mwingine (hizi ni hisia tu), mabadiliko ya kuileta idhaa ya Kiswahili ya BBC huku East Africa (Nairobi) huenda yalipelekea Kikeke akose nafasi ya kuendelea kuwepo BBC.

2. Wakati mimi na wewe tunawaza ukubwa na umaarufu wa BBC kama kitu cha ajabu, kwa Kikeke mkataba mnono wenye maslahi mazuri ndio kila kitu haijarishi ni media gani yenye jina. Kwanini? Kikeke anatafuta nini tena kwenye umaarufu wa kutangaza? Umaarufu utamsaidia nini kwa umri wake ikiwa atastaafu kutangaza na mfukoni hana hata senti kumi?

3. Mfumo wa maisha (kujichanganya na jamii), mitindo wa maisha (chakula, malazi, matembezi, familia),tabia binafsi za Kikeke (ucheshi) na kushindwa kupiga deals nyingine kupitia fani ya utangazaji ulikuwa hauwezi kumfanya Kikeke kuendelea kuwaza na kufikiri kuendelea kukaa London na kufanya kazi ya kutangaza habari (hard news) BBC maisha yake yote. Angeteseka sana. Bongo ndio kila kitu kimaisha kwa Kikeke

4. Kulingana na umaarufu, weredi wake na uzoefu wa kutangaza huenda Kikeke alitamani kuajiriwa na Media yoyote kubwa hapa nchini (iwe binafsi au umma), lakini kwa level ya juu zaidi (mkataba mnono sana au Cheo cha juu) na hilo halikuwezekana, hivyo njia ikafungukia kwa Crown media ambayo ni mpya, na kwa vyovyote vile vigezo hivyo huenda vimefikiwa.
 
Back
Top Bottom