Watanzania wengi hatuna exposure ya kutosha ndio maana tunashindwa kuelewa vizuri issue ya Kikeke.
Kwa uchache sana. Tufahamu haya kuhusu Kikeke;
1. Kwa mujibu wa Kikeke mwenyewe ni kuwa aliamua kuondoka BBC (hivyo inawezekana aliamua kuacha tu katikati ya mkataba au mkataba wake ulipoisha hakutaka kuomba kuongeza). Upande wa pili, tangu mwaka jana, BBC walibadilisha uendeshaji wa idhaa ya Kiswahili kutoka makao makuu UK, London kuja Nairobi, Kenya. Hivyo kama Kikeke angeendelea kubakia BBC basi ingebidi arudi Dar/Nairobi ili kutangaza idhaa ya Kiswahili ama angebakia London lakini kwenye majukumu tofauti ndani ya BBC, na hii ingefifisha brand yake ya umaarufu wa kutangaza. Upande mwingine (hizi ni hisia tu), mabadiliko ya kuileta idhaa ya Kiswahili ya BBC huku East Africa (Nairobi) huenda yalipelekea Kikeke akose nafasi ya kuendelea kuwepo BBC.
2. Wakati mimi na wewe tunawaza ukubwa na umaarufu wa BBC kama kitu cha ajabu, kwa Kikeke mkataba mnono wenye maslahi mazuri ndio kila kitu haijarishi ni media gani yenye jina. Kwanini? Kikeke anatafuta nini tena kwenye umaarufu wa kutangaza? Umaarufu utamsaidia nini kwa umri wake ikiwa atastaafu kutangaza na mfukoni hana hata senti kumi?
3. Mfumo wa maisha (kujichanganya na jamii), mitindo wa maisha (chakula, malazi, matembezi, familia),tabia binafsi za Kikeke (ucheshi) na kushindwa kupiga deals nyingine kupitia fani ya utangazaji ulikuwa hauwezi kumfanya Kikeke kuendelea kuwaza na kufikiri kuendelea kukaa London na kufanya kazi ya kutangaza habari (hard news) BBC maisha yake yote. Angeteseka sana. Bongo ndio kila kitu kimaisha kwa Kikeke
4. Kulingana na umaarufu, weredi wake na uzoefu wa kutangaza huenda Kikeke alitamani kuajiriwa na Media yoyote kubwa hapa nchini (iwe binafsi au umma), lakini kwa level ya juu zaidi (mkataba mnono sana au Cheo cha juu) na hilo halikuwezekana, hivyo njia ikafungukia kwa Crown media ambayo ni mpya, na kwa vyovyote vile vigezo hivyo huenda vimefikiwa.