Salma Kikwete ni Mwanamke wa Shoka, Mke, Mama, na Kiongozi. Ashusha hoja 10 za nguvu, aanza na Samia na kumaliza na Samia!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala hizi, "Kwa Maslahi ya Taifa" kuzungumzia jambo lolote lenye maslahi kwa taifa letu liwe ni jambo la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori stori yaani story teller, naomba nianze kwa mastory ya ilikuwaje nikaibukia Burundi na kwa wasiopenda mastori, una weza ku jump kwenye mada kuu ya uzi huu.

Mjue Mhe. Salma Kikwete kwa karibu zaidi na kwa undani zaidi, Mhe. Salma Kikwete, kwanza ni mwanamke, ili sio mwanamke tuu kama mwanamke wa kawaida, bali ni mwanamke wa shoka haswa!, ni mke kwa mumewe, Dr. Jakaya Kikwete, ni mama wa familia yake, ni pia ni former 1st Lady na ni Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wama, na kwa sasa ni mwanasiasa na mbunge wa jimbo la Nchinga akiwa ni mmoja wa wanawake wachache wa shoka ambao ni majembe ya ukweli kwa kuwa mbunge wa jimbo.

Zijue hoja zake 10 alizozishusha kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi Wanawake wa Afrika ambao ni wake wa viongozi wakuu wa Afrika uliofanyika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni

Kwenye hoja zake 10, Mama Salma Kikwete alianza na Rais Samia na kumaliza na Rais Samia. Andamama nami kwenye makala hii, sio tuu kuzijua hoja zake bali pia kuzisikia kwa masikio yako mwenyewe kwa kumsikiliza huku ukimtazama na kumshuhudia kwa macho yako mwenyewe ila hapa ni kwa wenye bundle
Hii hoja ya 11 ni ya ziada, baada ya mahojiano na hizo hoja 10, nikamuuliza kama ana la kuongezo, ndipo akashuka na hoja kubwa zaidi na muhimu zaidi kuliko zote!, ni hoja ya upendo kwa majirani, mpende jirani yako kama ndugu yako. Hoja hizi 10 za Mama Salma Kikwete, zimekuwa documented kwenye kipindi maalum cha TV, ambacho kitakujia hivi karibuni na kutangazwa kwenye vituo 6 vya TV, ITV, TBC, Star TV, Channel Ten, Clouds TV na Azam TV.

Ukiwa karibu na waridi lazima unukie!, mtu kukaa bennet na rais wa nchi kwa miaka 10, unakuwa na presidential qualities, ambazo unazipata kwa assimilation, mtu kama huyu akiwa groomed kidogo tuu, Tanzania tunaweza kujikuta tunampata Hilary Clinton wetu in near future!.

Nawatakia utazamaji mwema wa hoja hizi.

Natanguliza Shukrani

Paskali.
 
Amekulipa shs ngapi kumpromote?
 
FIRST LADY MSTAAFU MWENYE TAMAA YA UONGOZI/ULAFI WA MADARAKA.

MUMEO NI RAIS MSTAAFU ANALIPWA 80% YA MSHAHARA WA RAIS ILA WEWE BADO UNAKUWA NA TAMAA YA VIHELA VIDOGO VIDOGO!

SHAME!

Kwani ameenda Bungeni ili kuganga njaa au kuwakilisha na kutumikia wananchi wa jimbo lake!??
 
Amekulipa shs ngapi kumpromote?
Mkuu Bejamini Netanyahu , kwanza uwe na heshima, heshima kitu cha bure, huyu ni mke wa rais, ni Mhe. Mbunge, anahitaji promo yq nini?!.
Pili, tuko wote humu kwa zaidi ya miaka 8, mpaka leo bado tuu hatufahamiani vilivyo?!. Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi bure kwa kujitolea silipwi na mtu yeyote.
P
 
Umefanya kazi ambayo hujatumwa......
 
Umefanya kazi ambayo hujatumwa......
Mkuu airmax , kwanza karibu jf, kufuatia ugeni wako humu, na wewe kuwa ni mtumwa hivyo unadhani kila mtu ni mtumwa!, baadhi yetu humu sio watumwa, na mimi siku zote mimi sio mtumwa, huwa situmwi hivyo ni kawaida yangu kufanya kazi bila kutumwa, hivyo hongera, umepatia sana!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…