Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Hii inathibitisha kuwa mfumo wa ukaguzi bandarini ni mbovu na hata uandaaji wa nyaraka na upitishaji mizigo mipaka ya nchi jirani ni questionable
Mfumo siyo mbovu upo hivo ili watu wapate nafasi ya kula mzee unataka watu wafe njaa?
 
Yes inawezekana anataka azamishwe ili mmoja anayee uhusiano na kiongozi awe supplier Tanzania nzima. Kama wanavyopeana tenda za kuagiza mafuta. Kwani hatujui tenda wanachukua wenye meno.

Mbolea na pembejeo Ni biashara ya Nani kuagiza. Mbona sukari inakataliwa kuagizwa from Brazil na Bei iko chini kisa mmoja kunufaika eti viwanda vya ndani Basi wauze sawa na hao watakaoagiza ili kusiwe na haja ya kuagiza mzigo.

Afrika sijui Kama tutaendelea kwa uwazi aka transparency
 
Ukiona jambo kama hili limevuja jua kuwa watu wamechoma na mara nyingi shida huwa inaanza kwenye mgao wa pesa ya upigaji.

Unafikiri kuna akina mama bonge wangapi wanaopitisha mizigo kimagumashi hapo bandarini

Asante kwa taarifa hii chawa wa Nchemba
Kabisa mkuu,mama kibonge si wa kwanza na atokua wa mwisho kukwepa kodi,yote kutokana na misingi tuliyojiwekea
 
Bila 2025 kuweka JPM mwingine, Tz tumepigwa na kitu kizito.
Anajaribu kwenda Geita kila siku haisaidii , anatafuta kura za huruma ila hali sio shwari kwake kuelekea 2025
 
Mwendo wa kukamata dagaa tu. Kambale wanaogopwa. Wale wanaokula madini yetu kwenye migodi mbalimbali mbona hawaguswi?

Madela ukawamate wanaoingiza madawa ya kulevya nao walipe kodi kwani mmehalalisha waingize ngada bila kikwazo.
 
Jambo zuri ni kuwa TRA wameendesha Operesheni Maalum chini ya Kamanda na Jemedari Waziri wa Fedha Mwigulu Madelu Nchemba na amethubutu na kuweza kumdhibiti Mama Kibonge.[emoji23]

Connect Dots anaetaka kua supplier wa vitenge nchi nzima ni Boss wenu wa simba anaezaliwa singida anakotokea waziri wa fweza, yule jamaa anakiwanda na anazalisha bidhaa zisizo na kiwango kwahivo anawapiga figisu waingizaji vitenge wakubwa ili abakie peke yake tu, vitenge sawa na ngada tu zina figisu hatari
 
Yule mama ni koboko aisee...yule boss wa simba alitingishwa haswa...mwaka juz alinunua ghorofa tatu kkoo ndan ya mwez mmoja....afu akachukua mansion ya bil 8 osterby ...baada ya hapo akafunga maduka yake akaenda pumzika US mwez mzima....😂😂
 
Connect Dots anaetaka kua supplier wa vitenge nchi nzima ni Boss wenu wa simba anaezaliwa singida anakotokea waziri wa fweza, yule jamaa anakiwanda na anazalisha bidhaa zisizo na kiwango kwahivo anawapiga figisu waingizaji vitenge wakubwa ili abakie peke yake tu, vitenge sawa na ngada tu zina figisu hatari
Biashara bila Umafia huwezi toboa kirahisi, lazima uwe na watu, na hao watu wakusaidie na wewe uwasaidie
 
Back
Top Bottom