Hawa walitumwa kukaa chadema kama kitila mkumbo, ni aina hiyo ya wanachama.
Bora Kitilya Mkumbo.
Hao akina Mkumbo hawakuunda Chama ndani ya Chadema.
Hawa wakina Mrema waliunda chama tena baada ya uchaguzi kuisha na uongozi mpya kupatikana .
Demokrasia ni kukubali kushindwa na kusubiri uchaguzi ujao 2029 . Kama Lisu atashindwa chama basi 2029 atakosa kura na Mrema atapata fursa ya kugombea na kundi laki litawashawishi wajumbe .
Lakini hii ya kuanzisha chama cha upinzani ndani ya chama ni jambo baya sana la uasi na usaliti mkubwa . Yaani kundi la watu linaanzisha chama na kukiita G55 na kuweka agenda yao na uongozi wao na kuuheshimu uongozi wao na kupuuza uongozi halali wa Chama ni jambo la kijinga na kipumbavu na toto sana wa kisiasa na siasa za hovyo kabisa kuwahi kutokea duniani?
Hata huko Ulaya wanatofautiana ndani ya chama lakini kila mmoja anajitokeza kwa sababu zake na sio azimio la kuvuruga maazimio ya chama . Mtu anasema wazi kuwa katika hawa wawili mfano Samia na Lisu mimi nitamuubga mkono Samia japo ni wa CCM kutokana na sera zake nzuri na rikodi yake?
Lakin huu upumbavu wa kina Mrema ni utatoto na ulevi na ubinafsi na roho mbaya sana .
Yaani kwa miaka 32 CCM ,imeteka watu , imefunga watu na wengine ni yatima mpaka leo , imefilisi watu , imevuruga biashara za Mbowe , ilipora ushindi wa wabunge wengi wa upinzani kwa nguvu na kuumiza watu imenunua wapinzani na kudhalilisha wapinzani eti leo kwa sababu ya No reform no Election basi Chadema imekua mbaya kuliko CCM iliyoketa maumivu makubwa sana kwa Wapinzani ? Haiingii akilini kabisa ?
Hawa watia hawakua wapinzani bali vibaraka wa matajiri ndani ya CCM ndio MAANA JPM alitaka kuvifuta vyote ili vizalaliwe upya maana kwa yanayotokea ndani ya Chadema ni wazi kuwa kuna watu walikua wanawaza mifuko yao