Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Kwa hivi vigezo unaweza ukatafuta hadi unazeeka na usimpate huyo mke.

Ndoa ni maamuzi tu na mara zote huwa ni muunganiko wa watu wawili ambao si wakamilifu kwa maana huyu anamapungufu haya na huyu anayo haya ila kwa pamoja wote mnajifunza namna ya kuishi pamoja na hapo ndipo muunganiko mpya unapopatikana.

Mtazamo wangu:
Vigezo vingi ambavyo umevitaja hapa ni vya mwanamke ambae tayari alishaingia field na akajifunza so ako na uzoefu wa maisha hayo ila vinginevyo ni ngumu sana.

Ushauri... Kama kweli unania ya kuoa tafuta mwanamke ambae anakuheshimu kwa maana atakua anakuskiliza au mtakua mnasikilizana na hii hufanya kuwa rahisi kwenye kutengeneza awe kwa namna ile ambayo wewe unataka.
Umenena vema mkuu... Lakini katika pilika pilika zangu, nimegundua kuwa mwanzo huigiza wapo na adabu ya kutosha, lakini ukisha weka ndani tu mapicha picha yanaibuka faster.
 
Umemaliza kabisa.
 
Maisha ya mapenzi yamejaa comedy na stress kwa wakati mmoja, Naona ni ngumu sana kumpata mwanamke mzuri wa kuoa, Tayari ni takribani miaka miwili na miezi minne tangu nianze kuamua kutafuta mtu wa kuoa lakini bado sijafanikiwa.

. Safari hii imekuwa ya mizunguko na drama kibao hadi sasa, na kwa kweli naona kabisa nimeanza kuchoka kutafuta mke wa kuoa . Nahitaji mke ambaye tunalingana kitabia na kimtazamo kwa kiasi fulani. Sitaki mtu mwenye hasira za haraka au mwenye ukaidi au asiye na kifua( kilopo lopo). Nahitaji mke mwenye Uelewa wa maisha, mtunza siri za maisha na anayeweza kulea familia kwa ufasaha ikiwezekana kabisa asiwe anacheza VIKOBA.

. Kila uhusiano nitakaogusa naona kabisa huyu hafai kuwa mke bali anafaa kuwa mwanamke katika upande wa kiburudisho tu, ni ajabu sana aise,

. Cha kuchekesha kwa sasa ni kwamba nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi na rafiki yangu wa kike ambaye tumedumu naye kwenye mambo kadhaa ya biashara lakini bado naona hafai kuwa mke bali naona anafaa kuwa mwanamke tu. Wakati mwingine najihisi mjinga kwa kujaribu kuwa naye.

WanaJF, Inakuwaje kuwaje mpaka unafika hatua ya kusema yes huyu ndiye anafaa kuwa mke/mume wangu..??? 🤔🤔🤔
Kuoa kunataka uamuzi na ujasiri na kutunza ndoa kunataka:
1.hekima
2.busara
3.uvumilivu
4.kutimiza wajibu
 
Umenena vema mkuu... Lakini katika pilika pilika zangu, nimegundua kuwa mwanzo huigiza wapo na adabu ya kutosha, lakini ukisha weka ndani tu mapicha picha yanaibuka faster.
Ni sahihi ila wanawake nao wana moyo na machaguo yao kwahiyo hakikisha wewe ni chaguo lake isiwe kaja kwako kwa kua umetangaza ndoa.

Wadada wengi huwa wanauwezo wa kuwaacha watu wanaowapenda na kufuata ndoa huku wakiamini wanaweza kujifunza kupenda wakiwa ndani ila wakikuta ndoa ilivyo ni tofauti na matarajio yao basi hapo ndio mambo huwa tofauti.

Usikubali hili likukute so usiwe mwepesi wa kutangaza ndoa ila anzisha mahusiano na uache vitu viende venyewe mjikute mmeshaoana.
 
Back
Top Bottom