Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Salute Kwa Wale Waliokwisha Oa Au Kuolewa. Tafadhali, Mliwezaje Kufanikisha Hilo.?

Unaeleweka eleweka lakini?

Sura , kazi , kujiamini

Wanawake wanaotaka ndoa wanaangalia zaidi ya elfu 50 unayompa.

Mwanamke kama anakupenda atajifunza tabia unazopenda ili tu muwe wote.

Ukiona hawajifunzi jua hawajakukubali.
Yote haya, haina shida kabisa mkuu, siyo kwamba siwapati wanawake, ila yule ninaye mtaka awe ndo kipengele kinakuwa hapo ( naweza kuingia kwenye uhusiano na mwanamke fulani ila ukifuatilia zaidi ukoo unamatizo kibao)
 
Kweli nimeamini unaloliona rahisi kwako kwa wengine ni gumu...Mbona mabint ni wengi sana waliotayari kuolewa?
Ugumu upo kwa upande wa wanawake kuolewa japo wengi wapo tayari, ila kwa upande wa wanaume ni rahisi sana kupata mke mwenye sifa zote za kuwa mke

Alafu kudumu na binti wa watu sana bila kumuoa sio sababu ya kumfanya kipimo kwa wanawake waliobaki maana mwanamke anapozidi kukaa mtaani peke yake ndivyo anazidi kuharibika kimwili na kiakili lakini anaimarika kiakili akiwahiwa kuolewa
Kwa utafutaji huo wa mke inaonyesha unataka mkamilifu, wakati ukamilifu upo mbinguni..kila mwanadamu ana upungufu wake kwa hiyo tafuta mwanamke umpendaye kwa kuwa na vigezo vichache vyenye kuufurahi Moyo wako uwapo karibu yake na yeye awe ni mwenye kukuheshimu yaani mwe ni wenye kuelewana..mengine ni kuvumiliana maana hakuna mkamilifu zaidi ya hapo utakuwa unamtafuta malaika.
 
Yeah mkuu , single mothers ni wengi sana huko mitaani.. 🙂
Kweli wengine ni ndugu zetu na namba yao inaongezeka kwa kasi.Kuna ex wangu moja ,aliondokaga kwa kashfa kurudi kwa ex wake. Baada miezi kama nane akampigwa chini na yule ex wake, karudi kwangu turudiane, nimempotezea mwaka wa nne huu ,mwaka jana akaniambia kama vipi anibebee mimba yangu kama ukumbusho nimemkatalia. Niliblock namba zake nyingi, ila baadae nikaamua ni muache so akipiga sometimes na chuna,sometimes na pokea.

Kuna mademu wengine wamekata tamaa ya kuolewa nao wanataka watoto,huu mtego niliuruka na wapo vizuri kiuchumi, hizi milioni milioni sio issue. Ila nikiwangalia naona bora ni nyuti.
 
Hapa nakusupport, mwanamke mdogo bado una uwezo wa kumfanya unavyotaka ila akizd kukaa mtanaani, na kuwa na multiple partiners ambazo hazijaeleweka anazidi kuharibika kisaikolojia.
Kweli kabisa. Mwanamke akipata sehemu sahihi kabla hajayajua mengi ya dunia anatulia kabisa kiasi kwamba hata huko baadae hawezi kusikiliza ushauri wa mtu mwingine zaidi yako. Ukiona tofauti ujue shida ipo upande wako
 
Kikubwa usitangulize sana pesa na umjali aste aste huku unasoma mchezo, usijitape na mali zako na ulivyonavyo..jaribu kumshirikisha ideas halafu umwambie natafuta hela tujaribu na uliza kuhusu familia yake kidgo kidogo mpaka uone mwelekeo na response yake. Out kidogo sehemu za kawaida pima upepo, siku nyingine chuna usimtafute uone response yake.
 
Maisha ya mapenzi yamejaa comedy na stress kwa wakati mmoja, Naona ni ngumu sana kumpata mwanamke mzuri wa kuoa, Tayari ni takribani miaka miwili na miezi minne tangu nianze kuamua kutafuta mtu wa kuoa lakini bado sijafanikiwa.


. Safari hii imekuwa ya mizunguko na drama kibao hadi sasa, na kwa kweli naona kabisa nimeanza kuchoka kutafuta mke wa kuoa . Nahitaji mke ambaye tunalingana kitabia na kimtazamo kwa kiasi fulani. Sitaki mtu mwenye hasira za haraka au mwenye ukaidi au asiye na kifua( kilopo lopo). Nahitaji mke mwenye Uelewa wa maisha, mtunza siri za maisha na anayeweza kulea familia kwa ufasaha ikiwezekana kabisa asiwe anacheza VIKOBA.


. Kila uhusiano nitakaogusa naona kabisa huyu hafai kuwa mke bali anafaa kuwa mwanamke katika upande wa kiburudisho tu, ni ajabu sana aise,


. Cha kuchekesha kwa sasa ni kwamba nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi na rafiki yangu wa kike ambaye tumedumu naye kwenye mambo kadhaa ya biashara lakini bado naona hafai kuwa mke bali naona anafaa kuwa mwanamke tu. Wakati mwingine najihisi mjinga kwa kujaribu kuwa naye.

WanaJF, Inakuwaje kuwaje mpaka unafika hatua ya kusema yes huyu ndiye anafaa kuwa mke/mume wangu..??? 🤔🤔🤔
Wazungu wanakaa courtship mda mwingi Ili kumpata mwenza sahihi. Zama zimebadilika, siku hizi watu hawaamini Tena, wanawajibika. Imani imeshapandwa mda mrefu, Sasa tupo kwenye stage ya kuwajibika.
Try to be a good man, usiangalie uzuri Wala rangi, urefu Wala ufupi, mwanamke mwema hutoka Kwa bwana, Ni mwanamke wa mithali.
 
Yote haya, haina shida kabisa mkuu, siyo kwamba siwapati wanawake, ila yule ninaye mtaka awe ndo kipengele kinakuwa hapo ( naweza kuingia kwenye uhusiano na mwanamke fulani ila ukifuatilia zaidi ukoo unamatizo kibao)
Yote haya haina shida.

Jibu linatoka kwako.... labda wewe unajiona hivyo ila wanawake hawakuoni hivyo.

Unaweza ukawa unajiona bongel la bwana kumbe wanakuwa nawe kwa wanachokipata kwako. Jitathimini.

Angalia aina ya wanawake unaovutia.....
Dunia hii kuna kila aina ya viumbe mara nyingi unakutana na ambao umepanga [unconsciously] kukutana nao.
 
Back
Top Bottom