Ushabiki Wa Kidini Uende Sambamba Na Michezo? Hiyo Haitakuwa Michezo Bali Dini Kujiingiza Na Kutawala Michezo. Bora Siasa Itawale Michezo Kuliko Dini, ndiyo maana kuna wizara ya michezo na inaongozwa na waziri wa michezo ambaye ni mwanasiasa, si padri, mchungaji wala sheikh. Michezo inaunganisha watu wa imani zote. Hivyo basi wanamichezo wanapaswa kuanzisha huduma za watu wote ili waendelee kunufaika kwa mafanikio yake bila ubaguzi wa kidini. Yule mchezaji ni wa wote siyo wa dini yake pekee, afanye vitu vya kunufaisha wengi. Hachezi Kwa Ajili Ya Imani Yake, Anacheza Kama Pia Kwa Ajili Ya sifa kwa taifa lake.Taifa lake halina dini