Samatta ni mkubwa nje ya uwanja na kwenye vyombo vya Habari lakini ndani ya uwanja ni mdogo Sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema wakuu!

Mtanisamehe kwa wale wapenzi wa Mchezaji wa Mpira aitwaye Samatta. Lakini kiukweli tangu nimjue Samatta hasa akiwa ndani ya timu yetu ya taifa sijawahi kuona miujiza na ukubwa Wake.

Ukisikia matangazo ya kwenye Luninga na Redioni kumhusu Samatta amejengwa kwa namna ya mtu fulani mkubwa sana, mwenye mambo ya ajabu uwanjani lakini ukifika uwanjani ukatazama kile anachokifanya hakiendani na sifa anazopewa.

Ndugu yangu Samatta tunakuomba urudishe kile Watu wanachokuonà na wanachokusifia nacho.

Au je ni macho yangu tu?

Au je nimekuwa na chuki mpaka sioni uwezo wa Samatta uwanjani?

Au ni kweli hata ninyi mwaona kile nionacho?

Nawatakia jioni njema
 
Uonacho wewe hata mimi ndio ninachokiona juu ya huyu dogo. Jina kubwa Ila output ni ndogo sana
 
Wapuuzi ni wengi sana, hii inaashiria tuna vijana wa hovyo sana Taifa hili.

Mchezaji pekee tokea Tanganyika ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa Africa 2015 unapata wapi ujasiri wa kusema hawezi kandanda?.

Mpira hauchezwi na mtu mmoja pekee uwanjani bali ni ushirikiano wa watu zaidi ya 11.

Endapo wachezaji wawili wanacheza vema, kisha 9 wanacheza vibaya, hapo tegemea juhudi za hao wawili zitamezwa na hao vilaza 9. Hiki ndicho kinachomkumba Mbwana.

Nchi hii haijawahi zalisha mchezaji aliyeweza kuwa top scorer hata hapo burundi, sasa unapata wapi uthubutu wa kumtukana top scorer wa ligi ya DRC, CAF CL, ligi kuu ya Ubeligiji, amecheza ligi kuu Epl, Turkey, Greece na Tanganyika?.
 
Afcon ni mashindano makubwa na yanakusanya mastaa wengi wanaojua soka. Kama ulitegemea kwa viwango vya mastaa wetu vingeweza ku-outshine vipaji vya nchi zilizowekeza kwenye mpira basi umejipiga sana.

Fasihi + Mpira + Ujuaji = Uzi wa ovyo 😂😂😂 (Natania)
Guinea Bissau kaipiga ivory coast bao 4-0 Sisi Morocco tulijitahidi wakashinda 3-0 kwa mbinde kwanini tusipende cha kwetu? Hata km ndio hivyo tia maji tia maji Ila ndio cha kwetu
 
Wapuuzi ni wengi sana, hii inaashiria tuna vijana wa hovyo sana Taifa hili.

Mchezaji pekee tokea Tanganyika ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa Africa 2015 unapata wapi ujasiri wa kusema hawezi kandanda?.

Mpira hauchezwi na mtu mmoja pekee uwanjani bali ni ushirikiano wa watu zaidi ya 11.

Endapo wachezaji wawili wanacheza vema, kisha 9 wanacheza vibaya, hapo tegemea juhudi za hao wawili zitamezwa na hao vilaza 9. Hiki ndicho kinachomkumba Mbwana.

Nchi hii haijawahi zalisha mchezaji aliyeweza kuwa top scorer hata hapo burundi, sasa unapata wapi uthubutu wa kumtukana top scorer wa ligi ya DRC, CAF CL, ligi kuu ya Ubeligiji, amecheza ligi kuu Epl, Turkey, Greece na Tanganyika?.

Kwa hiyo mkuu kwa upande wako unaona ukubwa wa Samatta ndani ya uwanja akiaa na taifa Stars?
 
Afcon ni mashindano makubwa na yanakusanya mastaa wengi wanaojua soka. Kama ulitegemea kwa viwango vya mastaa wetu vingeweza ku-outshine vipaji vya nchi zilizowekeza kwenye mpira basi umejipiga sana.

Fasihi + Mpira + Ujuaji = Uzi wa ovyo 😂😂😂 (Natania)

Kwa upande wako unaona ule ukubwa wa Samatta alionao kwenye media akiwa uwanjani?

Mimi sijui mpira lakini sishindwi kuona Mchezaji akifanya maajabu licha ya timu yake kuwa mbovu
 
Kwa hiyo mkuu kwa upande wako unaona ukubwa wa Samatta ndani ya uwanja akiaa na taifa Stars?
Anacheza vema ila anaangushwa na kundi kubwa la wachezaji wa viwango vidogo.

Kuna nyakati anapambani hadi unashindwa kujua anacheza beki, kiungo au mshambuliaji.

Juhudi zake kwa sasa hazipimiki vema kwa vile;
a) Hana watu sahihi wanaomzunguka kama alivyokuwa TP Mazembe, KRC Genk na huko kwingineko Ulaya
b) Umri umemtupa mkono, hivyo ufanisi lazima ushuke.
c) Fitness ya wachezaji wa Taifa Stars wengi iko chini sana hali inayopelekea kushindwa kucheza kwa kasi ileile kwa dakika zote 90 kama afanyavyo Mbwana.

Kwa mazingira hayo usitegemee maajabu kutoka kwa Mbwana.

Simon kwa sasa ana bahati ya kufunga lakini hana uwezo wa kucheza zaidi ya dakika 45 kwa kasi ile ile tofauti na ICON wetu Mbwana.

Tumpe heshima anayositahili Mbwana kwa kazi kubwa aliyoifanya uwanjani hadi kuwa mfungaji bora kinara namba mbili wa muda wote hapo Taifa stars.
 
Sisi soka kiufupi hakuna kitu. Achana na Samata aliyejipambanua kivyake, juhudi zake zinakuwa dissolved na viwango ugali vya wachezaji wengine. Ukiwa kati ya wachawi vyuma arobaini na umejenga karibu na na una"hang out" nao na wewe u-binadamu unakutoka unakuwa mchawichawi tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Hizo ni tantarira tu, juhudi gani zinakuwa dissloved na viwango vya wengine wakati anapocheza Taifa stars yeye ndo kimeo kuliko wengine,angeonekana nafuu kuliko wenzake angekuwa na kiwango hicho, Samata hamna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samatta ni mchezaji wa klabu kwa sasa, sio mchezaji wa timu ya taifa. Huku anakuja tu ili akikataa asilaumiwe ila sio kwamba anatia juhudi binafsi. Hata ubishi wa Kibu pale mbele unaonekana at least asumbue mabeki hata kama hafungi.
 
Anacheza vema ila anaangushwa na kundi kubwa la wachezaji wa viwango vidogo.

Kuna nyakati anapambani hadi unashindwa kujua anacheza beki, kiungo au mshambuliaji.

Juhudi zake kwa sasa hazipimiki vema kwa vile;
a) Hana watu sahihi wanaomzunguka kama alivyokuwa TP Mazembe, KRC Genk na huko kwingineko Ulaya
b) Umri umemtupa mkono, hivyo ufanisi lazima ushuke.
c) Fitness ya wachezaji wa Taifa Stars wengi iko chini sana hali inayopelekea kushindwa kucheza kwa kasi ileile kwa dakika zote 90 kama afanyavyo Mbwana.

Kwa mazingira hayo usitegemee maajabu kutoka kwa Mbwana.

Simon kwa sasa ana bahati ya kufunga lakini hana uwezo wa kucheza zaidi ya dakika 45 kwa kasi ile ile tofauti na ICON wetu Mbwana.

Tumpe heshima anayositahili Mbwana kwa kazi kubwa aliyoifanya uwanjani hadi kuwa mfungaji bora kinara namba mbili wa muda wote hapo Taifa stars.

Mkuu kwa sisi tunaangalia kama yalivyo bila kupepesa macho tunaona uwezo wa Samatta uwanjani haulingani na promo na jina alilonalo kwenye Media.

Heshima anayo kwa juhudi za kucheza nchi za Ulaya lakini tukizungumzia kiwango chake akiwa Stars hapana mkuu
 
Back
Top Bottom