Samia atikisa dunia akiwa Paris, akusanya zaidi ya dola bilioni mbili kwa ajili ya nishati salama

Samia atikisa dunia akiwa Paris, akusanya zaidi ya dola bilioni mbili kwa ajili ya nishati salama

kuzurula huku ndo kunatuletea ushoga watanzania tunajiweza sio omba omba "nishati safi ya kupikia" hili swala kutatuliwa mpka ndege ipandwe...
 
Hii haijawahi kutokea, najua unajua lakini nakujuza ujue zaidi. Rais Samia amekusanya mabilioni ya dola kwa ajili ya nishati salama.

Kwa hakika Samia ndiye Rais mwenye ushawishi mkubwa duniani akitokea Afrika, ni lulu, ni almasi, ni mwamba kutoka Tanzania.

Mitano tena!? ahahaha, na hapa ipoo.
View attachment 2993081
Ujinga ni mbaya jamani . Amekusanya nani kazisahau hizo dollar? Unaweza ukawa na akili timamu ukaenda ufaransa kujadili matumizi ya nishati Bora afrika? Hata hujui kama wamekopeshwa kwa masharti? Hata hujui kama waliowakopesha ndiyo wanawaibia nishati? Nani anasomba gesi ya songosongo? Unamjua? Wewe ni mjinga mno
 
Mbona Israel Imekuwa kwa misaada ya US?

Win win situation, huku Israel ikibebwa na Historia + maslahi ya USA and allies middle east.
Wakati huohuo akitegemea vichwa na maarifa ya mazayuni kwenye teknolojia jeshini.

Sisi tunampa nini USA kama sio rasilimari ambazo ndio urithi wetu? maana hatuna maarifa wala teknolojia yakumsaidia USA.
 
Hiyo Misaada na mikopo sanasana inakuja kuzidisha umasikini tu kwa vizazi vyetu maana ikija huku Kwa hawa mafisi inaliwa na nchi inabaki na madeni vizazi na vizazi.

Ndio maana ukifikiria sana kwa ueledi utagundua kuna watu wengi sana wanapaswa kuawawa na familia zao kufilisiwa ili Taifa lipone.
 
Nchi yetu Ina gesi na mkaa wa mawe lakini pia tuna dhahabu.
Mnakumbuka Mkapa aliwapa wazungu mgodi wa Tanzanite wachimbe bure tu watumikishe watanzania Kisha wakaondoka na madini.
Sisi vyetu vya thamani kubwa tunawapa wageni bure tu ilhali vijana wetu wanauza Figo kwa ugumu wa maisha.
Kama taifa hebu tukae chini tuone Ni namba gani gesi yetu itaokoa misitu yetu.
Tunaweza kuzalisha umeme wa Bei ndogo kutumia gesi Kisha kila mmama akatumia umeme kupikia.
Hii haihitaji tuwe na diploma au degree.
 
Sielewi mantiki ya mtoa mada, kwamba rais anajua kuomba pesa wazungu ndio wanamsifu ama?

Ukiwa rais wa nchi yenye rasilimali kama hii hata ukitaka dola bilioni 20 utapata lakini lazima utazilipa tu.

Wazungu wenyewe wana shida zao binafsi, kwani wangeshindwa kupeleka hizo pesa Ukraine?

Punguzeni uchawa.
 
Back
Top Bottom