GE2025 Samia Kuongea na wazee pamoja na wakuu wa Mikoa kesho 27 /08/ 2025

GE2025 Samia Kuongea na wazee pamoja na wakuu wa Mikoa kesho 27 /08/ 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kikao kiwe na wazee wapya siyo walewale na wazee wenyewe wajenge hoja za kuruhusu uwanja huru wa Siasa, wakatae chadema kukosa uhuru wa kufanya siasa wakemee Lisu kuwepo Gerezani hadi sasa hizo ndiyo busara sahihi za wazee, lakini wakienda kimyume na hapo watakuwa siyo wazee bali ni wanaccm wamekutana kwa kivuli cha wazee kuihadaa Nchi
 
Wazee halisi ni wale hukataa uhuni matendo maovu kwa uwazi ukiwa mzee kisha kuwa mnafiki unapoteza sifa ya kuitwa mzee
 
Kikao kiwe na wazee wapya siyo walewale na wazee wenyewe wajenge hoja za kuruhusu uwanja huru wa Siasa, wakatae chadema kukosa uhuru wa kufanya siasa wakemee Lisu kuwepo Gerezani hadi sasa hizo ndiyo busara sahihi za wazee, lakini wakienda kimyume na hapo watakuwa siyo wazee bali ni wanaccm wamekutana kwa kivuli cha wazee kuihadaa Nchi
Hao wazee wana chaguliwa na nani?
Kwani wanayo fursa ya kueleza chochote? Mzee Warioba atakuwepo, Butiku; na hata wazee toka vyama vya upinzani watakuwemo kwenye kundi hilo?

Hao wakuu wa mkoa wanao umuhimu gani kwenye kikao hicho; kama siyo kuja kupewa mwongozo wa kuharibu uchaguzi?

Hadi hapa haionyeshi kuwa na matumaini yoyote na kikao hicho.
 
Wazee wakishapewa bahasha nzito watahoji nini?
Ni bora akaongee na TLS ambao wamesoma na wanaweza wakauliza maswali au TEC.
 
Wakati wa Nyerere akiongea na wazee wa Dar es salaam ni Imani gani walikuwa wengi kwenye mkutano.
waislamu ndio walikuwa wengi, wazee. But siyo enzi hizi. Kariakoo yote muda ule ilikuwa ya Wazaramo, 100% moselems. Leo wakazi wa Dar wengi ni mchanganyiko say by 50/50, and those taking note of what is going on /caring for the politics of Tanzania, are not that many elders........ as you may think the situation to be.

nayasema haya kwa vile huyu mama anaonesha udini waz wazi .
 
Leo tutajionea wazee wakishangilia hovyo hovyo bila sababu za msingi.​
 
..hali hii imesababishwa na uzembe wake mwenyewe.

..wananchi walikuwa na matumaini makubwa naye.

..waliamini atakuwa mtenda HAKI, na atakomesha dhuluma.

..Na yeye aliwapa wananchi matumaini makubwa kwa kuleta falsafa ya 4R.

..Ni bahati mbaya sana ameachana na falsafa hiyo.
Ni kweli, baada ya SONGOMBINGO za Magufuli wengi tuliamini nchi imepata mtu sahihi...nadhani shida ilianza alipoanza kuwasikiliza WAHUNI
 
RAIS SAMIA HASSAN KUONGEA NA TAIFA KUPITIA MKUTANO WAKE NA WAZEE 27 AGOSTI 2025

Mh. Samia Suluhu Hassan kesho atazungumza na wazee pamoja na wakuu wa mikoa wote, mheshimiwa rais amebainisha jambo hilo leo tarehe 26 Agosti 2025 Ikulu.


View: https://m.youtube.com/watch?v=lGoDPZUMinE
Kihistoria utamaduni wa rais kuongea na wazee ni jukwaa mojawapo kuongelea mambo mazito nchini Tanzania na hivi hali ya kisiasa ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu kuna mambo na maswali mengi yanayohitaji kupatiwa mwongozo

Ikichukuliwa Wazee wameona mengi na wana uzoefu mkubwa. Labda ndiyo maana rais anataka kuzungumza nao ili mamlaka zione wazee wanasema nini na wataiambia mamlaka nini.

Ni utamaduni, toka tumepata Uhuru Viongozi wetu wamekuwa wakikaa na kuongea na Wazee.

Picha maktaba za 7 Mei 2021
View attachment 3453817
Rais Samia Hassan ktk picha maktaba ya mwaka 2021
View attachment 3453818

Wazee wa sisiemu
 
Tunatiki kama kawa
All the best ,mnashindana na upepo .Tanzania Raha sana.Kura zilishapigwa experience ya 2020 iko bado kichwani sidhani kama kuna mabadliko.Mkinionyesha kura za urais 2020 kwenye website ya tume ,napiga
 
vipi mzee
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. ILA AOMBE KWA IMANI, PASIPO SHAKA YEYOTE; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”
Kwenye maombi Kuna Imani ya kuomba na kuna Imani ya kupokea.
Mzee mpili nae atakuwepo?
 
Back
Top Bottom