Pre GE2025 Samia ndio kiongozi pekee wa awamu ya 5 aliyeenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitalini lakini shukrani anayopata ni matusi na kumbagua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Achana na mambo ya kijinga ya kumtukuza mtu tumia akili yako, ulienda shule kufanya nini kama unaishi kwa kutegemea mawazo ya mtu? nipe faida 5 za huu muuungano fake kwa watu wa bara
Akili yangu ndio hii naitumia.Lisu anahubiri chuki Kwa maslahi ya nani? Mgawanyiko Ili nani afaidike? Matusi ilomkitikee nini?
 
Lakini si ni Samia huyu huyu kwenye kampeni alisema kuna mtu anajitembeza anasema kapigwa risasi! akaongeza kua askari wetu hawewezi kukosea na kama akipiga risasi tatu aspoua atawajibishwa. Umesahau mkuu?! CCM WANA UNAFIKI MWINGI SANA, USIPOKUA MAKINI UNAWEZA UKAWAAMINI.
 
Lissu inabidi afanye siasa lakini na utu pia auzingatie.

Mama Samia alimuonyesha upendo mkubwa sana wakati wa dhiki yake. Inabidi ampige spana za kisiasa lakini utu wake aulinde kwa unyenyekevu mkubwa!.

Nampenda Lissu mwenye hoja, Simpendi Lissu arrogant!
 
Kuitwa mzanzibar ni kosa? hana kitambulisho cha mzanzibar?
 
Lisu na Freeman Mbowe ni watu wawili tofauti kabisa.

Mbowe anakupiga spana bila kukuudhi, kwenye msiba wa Lowasa Mbowe alipewa nafasi kuongea kama mwanafamilia lakini alipiga spana kwa lugha ya kiungwana kabisa.

Ile nafasi angepewa Tundu Lisu huenda angezimiwa mic, hiyo ndio tofauti ya Freeman Mbowe na Tundu Lisu.

Ukweli mchungu Lisu ni mwanasiasa mzuri sana lakini siyo Presidential material hana tofauti na kina Magufuli.
 
Tumekusikia ewe mshauri wa mama a.k.a CHAWA SUGU
 
Nyerere hakuwa Mungu.... Tafakari
 
Lisu amenifundisha kitu kwamba majitu ya dizaini yake sio ya kusaidia Kwa lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…